Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Habari za leo wazazi / walezi katika mada hii....

Kuna dhana ilijengeka miaka ya nyuma na ninasikia kuna jamii bado inaendelea kupractice hii kitu.

Ilisemekana watoto wanaoanza kuota meno huwa wanaanza kuota meno ya plastic na yale meno yalikuwa yanang'olewa.

Mbona siku hizi hili jambo halivumi sana? Ina maana watoto wa siku hizi hawaoti hayo meno???

Karibuni

C.c. mshana jr, Evelyn Salt, angel nylon, Lizzy na wazazi / walezi wote.
Hizi zilikuwa ni imani tu na kukosa elimu yale yanayoitwa meno ya plastic ni meno ya utotoni ambayo huja kung'oka baadae, binafsi sijawahi kukutana nayo
 
Hatujui chochote kuhusu yeye kwakuwa hata hivyo hakuwahi kuwa kwenye mahusiano yoyote
Bible inasema kuwa Mungu anatuwazia na yeye ni mwema

Hivyo kama kibamia sio jambo jema basi Bible ingekataa tohara siku ya nane mtoto kuzaliwa!

Anyway ni mtazamo wangu tu!

Turudi kwny mada!

Nimeipenda sio siri kuhusu watoto
Nimejifunza mengi mno
Ahsante
 
dah!!!!! huu uzi nimekazana kuufungua tangu siku nying hatmae nimeweza!!!!!! asante kwa idea yako mkuu!!,.
 
Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.

Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.

Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2

Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.
Ndo maana binafsi mzazi anaempeleka boarding mtoto mdogo eti sababu hana muda wa kulea ama kwa kuamini huko ndo kuna malezi bora mzazi huyu ni mjinga mbumbumbu limbukeni na mshamba wa kichwa,na hafai kuitwa mzazi bali foroma ya kufyatulia watoto,samahani kwa nlowakwaza kwa kusema haya,mkitaka fafanuzi niulizeni nipo tayari kutetea nsemalo
 
Yesu alitahiriwa siku ya nane!
Nae ana kibamia?

Hizi huwa ni imani tu!
Bro wianisha jina lako na huyo unaetoa maneno na mfano wa kutusi,YESU ni kitu kingine kabisa haukupaswa kusema hivo maana unaeza chuma maana kubwa sababu tu ya mashindano ya kijinga ya humu jf,Fanya utubu mkuu,take it or leave it,
Ila MUNGU akusamehe sana hujui ukuu wa YESU
 
Habari za leo wazazi / walezi katika mada hii....

Kuna dhana ilijengeka miaka ya nyuma na ninasikia kuna jamii bado inaendelea kupractice hii kitu.

Ilisemekana watoto wanaoanza kuota meno huwa wanaanza kuota meno ya plastic na yale meno yalikuwa yanang'olewa.

Mbona siku hizi hili jambo halivumi sana? Ina maana watoto wa siku hizi hawaoti hayo meno???

Karibuni

C.c. mshana jr, Evelyn Salt, angel nylon, Lizzy na wazazi / walezi wote.
Nami nikiskia tu miaka hio ya nyuma ila hata sijawahi kukutana na case kama hii live.

Pengine ni hizi milk teeth, wakiita hivyo. Au pengine yapo kweli lkn ndo wanayaondoa kwa njia za kienyeji kama alivosema Evelyn.
 
Msaada wenu wana jamii.
Mwanangu wa miezi mitatu ana kitu kama mafua lakini hayatoki na anahema kwa shida sana. Tulienda hospitali walisema ni mafua tukapewa dawa ya mafua, ametumia lakini hakuna mabadiliko na zimebadilishwa nne bila nafuu yoyote na kwanza ndio yanazidi. msaada wenu jamani
 
Tulienda hospital nyingine iliyopo eneo la Kwamndolwa, wilayani Korogwe Tanga. Baada ya Dr kumuangalia mtoto akabaini ameota vinyama puani ndivyo vinavyompa shida ya kuhema, na tumeambiwa twende jumatatu kwa ajili ya kupata barua ya rufaa kwenda Muhimbili. Hata sasa bado mtoto anapata tabu sana kuhema licha ya kupewa dawa mbadala ya kufungua poa kama kuchemsha maji ya vuguvugu kuweka chumvi kidogo alafu tunamuweka puani.
Mtoto ana umri wa miezi mitatu, naomba msaada kwa wote wanajua. Je, mtoto wa miezi mitatu anaweza kufanyiwa surgery? Je kuna dawa ya kuweza kuvikausha? Je kuna dawa za asili zenye kuweza kutibu? Msaada wenu ndugu zangu.
 
Nadhani inawezekana kabisa kwakuwa kuna baadhi ya upasuaji hufanyika chini ya umri huo
 
Mada nzuri sana.....ngoja nisome kwanza posts zote kisha na mimi nichangie au kuuliza maswali. Isijekuwa maswali yangu yameshajibiwa
 
Hapo kwenye lishe ya mtoto wa siku moja mpaka miezi sita, maziwa ya mama peke yake hayatoshi. kuna haja ya kuongezea uji mwepesi kadiri mtoto anavyokuwa, maana watoto wengine jinsi anavyokuwa maziwa ya mama hayamtoshelezi. utakuta mtoto hapati usingizi vizuri sababu ya kutokushiba vizuri
Asante fatimata nimeongeza kitu hapa
 
Mada nzuri sana.....ngoja nisome kwanza posts zote kisha na mimi nichangie au kuuliza maswali. Isijekuwa maswali yangu yameshajibiwa
Mada ni nzuri sana kwa kweli na mimi imenielimisha vizuri ingawa sijamaliza kusoma post zote
 
Kuna vikohozi vikavu visivyokoma hapa dawa yake ni Kijiko kidogo cha asali na kama una maziwa fresh unaweza kumchanganyia humo...hii haina madhara kabisa na kama ni mdogo zaidi humpi kwenye Kijiko bali unamlambisha
sorry mkuu unampa huo mchanganyiko kwa muda gani ..namaanisha mara ngapi ili dozi ikamilike
 
sorry mkuu unampa huo mchanganyiko kwa muda gani ..namaanisha mara ngapi ili dozi ikamilike
Hizi ni remedies kwahiyo hazina muda maalum lakini huyo angefanya kwa siku saba kwanza
 
mimi mke wangu amejifungua lakini maziwa hayatoki kabisa akinyonyesha labda mwezi mmoja tu baada ya hapo mtoto hashibi inabid aanzishiwe maziwa mbadala, je tatizo liko wapi na ufumbuzi wake ni upi?
 
Back
Top Bottom