Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Je mtoto humchukua miezi mingap kuanza kuota meno?

Je mtoto anatakiwa aongezekea kg kwa mwezi?

Je mtoto anapolalala muda mfupi na kustuka ana tatizo?

Je mtoto anatakiwa kuanza kupewa uji baada ya miezi mingapi?

Kweli kulea ni kazi ila kuna raha yake sometimes

Grow up my babygirl, Mungu anilindie hii roho yangu

cc mshana
 
Habari wakuu... Mwanangu ana miezi 6 anasweat saaana, hata kama mvua inanyesha akila au akinywa anasweat mpaka naogopa. Je anaweza kuwa na tatizo?
Do not worry about your child’s sweating as it is quite common in young children and is usually a direct result of the environmental conditions.
 
Ni nyingi kwa kweli. Ila sijui hata nikwambiaje I remember my son akiwa na umri before 6 months alikuwa hataki kulala na anakomaa kwelikweli nikaamua kumpa uji wa kuchuja after that akawa analala vzr tu. My be factor ya c section
Sawa
 
Mtoto wangu ana miaka 2 ana kilo 12 haongezeki uzito kwa zaidi ya miezi 5 nimejaribu kubadilisha aina tofauti ya vyakula lakini haongezeki naomba kujua kama ni tatizo
 
Hivi kwanini watoto huwa hawapendi kufunikwa wakilala teh sio tatizo ila nataka kujua
 
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia
-Mtoto anapopata gesi tumboni
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Very sure mkuu, uko very intelligent na mwenye kujali, tuelimishe kuhusu hayo km una ufaham nayo
 
me sijui labda joto wangu nalazimika kumvisha nguo za joto usiku sababu ukimfunika kama kanasumbua
Sio joto tu hata kukiwa na baridi, atarusha rusha miguu hadi atoe shuka ndio alale, mara nyingi sana huwa naona kwa watoto
 
Back
Top Bottom