Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Hii elimu
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia
-Mtoto anapopata gesi tumboni
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Hii elimu imekuwa ufunguo kwangu nina mtoto naumri wa miaka miwili kasoro nimejifunza mengi humu
 
Habari zenu wadau,mtoto Wangu analia lia sana toka akiwa mdogo na sasa hivi ana mwaka mmoja,sio kwamba ni mgonjwa,tupeane uzoefu jamani mwenye kujua
 
Habari zenu wadau,mtoto Wangu analia lia sana toka akiwa mdogo na sasa hivi ana mwaka mmoja,sio kwamba ni mgonjwa,tupeane uzoefu jamani mwenye kujua
Wakati wa kulala mwogeshee maji vuguvugu uliyochanganya na chumvi kiasi ya mabonge

Jr[emoji769]
 
***MUHIMU***
IMG-20200814-WA0096.jpg

Jr[emoji769]
 
Habarini wakuu,

asante sana kwa mada hii nzuri ya watoto. mimi naomba ushauri nna mtoto wa miaka 10 wa kike. ameanza tabia za kuonyesha interest kwenye mambo ya mapenzi km kubusiana na wenzie kucheza kimama na mtoto mmoj kuwa baba then mambo ya kukumbatiana. nimekuwa mkali sana kwake. sasa naogopa hata kumpeleka bording school nahofia asije akaendeleza zaidi hiyo michezo, ila sasa kwa darasa alilopo na ratiba ya shule yao ni afadhali akae bording.

Najua kuna wazazi mna watoto wakubwa zaidi stage hii kwa watoto mlifanyaje. maana nimejaribu kuuliza naambiwa natakiwa kuwa mkali lkn ni stage za watoto, naombeni mnisaidie mbinu za kufanya aache hizi tabia na zisije endelea zikawa mbaya zaidi huko mbeleni.

Asanteni
 
wana Jamvi watoto ni Malaika . Mimi nimezaa mmoja Mungu kaniletea wengine watatu . Ameniletea ndio kwa sababu niliwapata tu barabarani . Wawili niliwapa Ubungo Dar karibu na Landmark Hotel . Mmoja ndio nilimpata Lumumba kariakoo. Nina vidume wanne ndani .

Ni hivi nilipowapata nilisukumwa kuwachukua na kuwalea ila niliogopa sana kuwachanganya na kitoto changu . Roho ya ubinafsi ilinishika nikahofia makuzi yao na wa kwangu nikaogopa nikajibana nikawasukuma bording school wangu akabakia day school . Kule mmoja aliingia la kwanza wenzake waliingia darasa la tatu baada ya kurudi home likizo ya kwanza niliwagundua kuwa sio tishio kwa mwanangu
Kwanza wakageuka walinzi kwa mwanangu walimlinda asionewe mtaani . Nikawapenda
Walipendana sana hata sasa ukiwatazama wanafanana wote Wanne . Age yao inatofauti ndogo sana usiniulize wana umri gani kwa sababu walikuwa hawajui hivyo niliwakadiria tu yaani.
Wana akili tu za maana kule shuleni (ya wasabato) wanajifinza neno la Mungu wakirudi likizo wanakuwa wanyoofu sana .

Nimefikiria kama naweza kuongeza mmoja wa kike wacha niendelee kutazama huko mtaani . Ila
Haikuwa kazi rahisi na sijui huko siku zijazo itakuwaje . Maana mimi ni single mother so nabadilisha tu masauti ila malezi sio lelemama najitahidi kuvimba ndani ila upendo wangu kwao na wao upendo wao kwangu umetuweka kwenye uwiano mzuri

Nimesema watoto ni malaika haswa tangu niwapate hawa viumbe sijawahi kupungukiwa hata huwa nashangaa sana zinatoka wapi njia zakukamata mshiko maisha fresh kabisa. Watoto ni baraka uwe umezaa au umebeba mtaani kama nilivyobeba mimi . Yaani heri tupu 🙏🏽🙏🏽
 
habarini wakuu,
asante sana kwa mada hii nzuri ya watoto. mimi naomba ushauri nna mtoto wa miaka 10 wa kike. ameanza tabia za kuonyesha interest kwenye mambo ya mapenzi km kubusiana na wenzie kucheza kimama na mtoto mmoj kuwa baba then mambo ya kukumbatiana. nimekuwa mkali sana kwake. sasa naogopa hata kumpeleka bording school nahofia asije akaendeleza zaidi hiyo michezo, ila sasa kwa darasa alilopo na ratiba ya shule yao ni afadhali akae bording. najua kuna wazazi mna watoto wakubwa zaidi stage hii kwa watoto mlifanyaje. maana nimejaribu kuuliza naambiwa natakiwa kuwa mkali lkn ni stage za watoto. naombeni mnisaidie mbinu za kufanya aache hizi tabia na zisije endelea zikawa mbaya zaidi huko mbeleni. asanteni
Ni hatua katika makuzi na hayo mambo kwa sasa kutokana na utandawazi hayaepukiki ..muhimu sio kuwa mkali sana bali kumfundisha kujitambua na madhara ya kuwa kwenye mahusiano kwenye umri mdogo
Mfanye awe karibu yako utampa confidence kubwa na atakuambia mengi..ukali utaficha mengi
Kubwa kuliko yote hayafanyi hayo na jinsia yake bali jinsia pinzani hivyo yuko normal
 
wana Jamvi watoto ni Malaika . Mimi nimezaa mmoja Mungu kaniletea wengine watatu . Ameniletea ndio kwa sababu niliwapata tu barabarani . Wawili niliwapa Ubungo Dar karibu na Landmark Hotel . Mmoja ndio nilimpata Lumumba kariakoo. Nina vidume wanne ndani .

Ni hivi nilipowapata nilisukumwa kuwachukua na kuwalea ila niliogopa sana kuwachanganya na kitoto changu . Roho ya ubinafsi ilinishika nikahofia makuzi yao na wa kwangu nikaogopa nikajibana nikawasukuma bording school wangu akabakia day school . Kule mmoja aliingia la kwanza wenzake waliingia darasa la tatu baada ya kurudi home likizo ya kwanza niliwagundua kuwa sio tishio kwa mwanangu
Kwanza wakageuka walinzi kwa mwanangu walimlinda asionewe mtaani . Nikawapenda
Walipendana sana hata sasa ukiwatazama wanafanana wote Wanne . Age yao inatofauti ndogo sana usiniulize wana umri gani kwa sababu walikuwa hawajui hivyo niliwakadiria tu yaani.
Wana akili tu za maana kule shuleni (ya wasabato) wanajifinza neno la Mungu wakirudi likizo wanakuwa wanyoofu sana .

Nimefikiria kama naweza kuongeza mmoja wa kike wacha niendelee kutazama huko mtaani . Ila
Haikuwa kazi rahisi na sijui huko siku zijazo itakuwaje . Maana mimi ni single mother so nabadilisha tu masauti ila malezi sio lelemama najitahidi kuvimba ndani ila upendo wangu kwao na wao upendo wao kwangu umetuweka kwenye uwiano mzuri

Nimesema watoto ni malaika haswa tangu niwapate hawa viumbe sijawahi kupungukiwa hata huwa nashangaa sana zinatoka wapi njia zakukamata mshiko maisha fresh kabisa. Watoto ni baraka uwe umezaa au umebeba mtaani kama nilivyobeba mimi . Yaani heri tupu [emoji1431][emoji1431]
Mh whitehorse barikiwa zaidi na zaidi ...simulizi yako imenigusa kwa namna ya pekee mno...si kila mmoja wetu ana moyo kama wako...hicho chako ni kipawa
 
Mimi kijana wangu niliyempata katika umri wa ujana hapendi shule kabisa Yuko darasa la nne, haandiki Wala hakusanyi madaftari kwa walimu, ameshapigwa Ila wapi, najaribu kuangalia tatizo litakiwa Nini maana alikuwa anasoma shule ya mbali nikamhamishia ya karibu Ila shida iko palepale.

Mitihani anafanya na anapata wastan mzuri Sana najiuliza nimfanyeje aweze kupenda shule.? Ni mbinu gani nitumie ili asome kwa utulivu?
 
Mh whitehorse barikiwa zaidi na zaidi ...simulizi yako imenigusa kwa namna ya pekee mno...si kila mmoja wetu ana moyo kama wako...hicho chako ni kipawa

Asante Mshana Jr . Ni Mungu alinipa nguvu ya pekee. Ninashukuru amenisaidia mno kuniongezea familia yaani wala sitamani tena kuzaa nikimalizia kujitafutia wa kike mmoja nakuwa nimemaliza 🙏🏽🙏🏽
 
Mimi kijana wangu niliyempata katika umri wa ujana hapendi shule kabisa Yuko darasa la nne. haandiki Wala hakusanyi madaftari kwa walimu,ameshapigwa Ila wapi.najaribu kuangalia tatizo litakiwa Nini maana alikuwa anasoma shule ya mbali nikamhamishia ya karibu Ila shida iko palepale. mitihani anafanya na anapata wastan mzuri Sana najiuliza nimfanyeje aweze kupenda shule.? Ni mbinu gani nitumie ili asome kwa utulivu?
Anahitaji counseling kubwa...lakini kwanza la muhimu kabisa jiweke karibu naye
 
Asante Mshana Jr . Ni Mungu alinipa nguvu ya pekee. Ninashukuru amenisaidia mno kuniongezea familia yaani wala sitamani tena kuzaa nikimalizia kujitafutia wa kike mmoja nakuwa nimemaliza [emoji1431][emoji1431]
Mungu akubariki na kukupigania sana sana
 
Back
Top Bottom