Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

KKweli
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

  • Mtoto anapolialia
  • Mtoto anapopata gesi tumboni
  • Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
  • Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
  • Umeme
  • Maji
  • Moto
  • Mwanga wa Tv
  • Simu, mawimbi yake
  • Vyombo na vitu mbalimbali
  • Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
 
Kwa kawaida hua unafunga miezi 18 mpaka miaka miwili,
Nashauri akamwone dactari kwa evaluation zaidii
 
Bado unasumbuka na mtoto asieongezeka uzito karibu Lily lishe kiboko watoto wasioongezeka uzito unga wetu ni msafi umezingatia uwiano wa nafaka usisumbuke kukabana na mtoto Karibu uone tofauti tupo magomeni Dar mikoani tunatuma uwaminifu mkubwa kg tsh 5000..0789319941
IMG_20211010_204430_807.jpg
 
Huku Tanga Kuna kitu kinaitwa Zongo, mtoto anapigwa yeye ni kulia tu na kuharisha, na tumbo kuuma, unaweza kumpa kila aina ya dawa lakini wapi, ila ukienda kwa hao wataalam wenyewe wa kutegua mabomu, unakuta mtoto anapona kwa Tsh 5000 tu, mimi nilikua mbishi ila mwisho wa siku nuliamsha mkono, unakuta mtoto anadhoofika mpaka unamuonea huruma,
 
Huku Tanga Kuna kitu kinaitwa Zongo, mtoto anapigwa yeye ni kulia tu na kuharisha, na tumbo kuuma, unaweza kumpa kila aina ya dawa lakini wapi, ila ukienda kwa hao wataalam wenyewe wa kutegua mabomu, unakuta mtoto anapona kwa Tsh 5000 tu, mimi nilikua mbishi ila mwisho wa siku nuliamsha mkono, unakuta mtoto anadhoofika mpaka unamuonea huruma,
Halafu ukimpima hospital hana tatizo lolote
 
Back
Top Bottom