Kwa Wazazi: Utapeli wa English Medium upo katika maeneo yafuatayo

Kwa Wazazi: Utapeli wa English Medium upo katika maeneo yafuatayo

Mimi English medium nilimpeleka mtoto ili awe salama tu kwa sababu care kuleipo afadhali na walimu wanawajibika Kama atapata tatizo. Lakini kwa upande wa elimu ni uongo. Mwaka huu nampelekakayumba then hela niliyokuwa nalipa kule nitakuwa namnunulia assets Kama mashamba. Maana naona watoto wa kiarabu hawasomi lakin ndo wanamiliki uchumi. Elimu yetu Haina msaada kwa future ya watoto
 
English medium ya 1.5 haiwezi kufanana na ya 3M; na sio kwamba wanakula hela hapana, bali ndio kiwango cha pesa walichonacho, hivyo wazazi ndio wanaosababishia watoto wao mateso huku wakinufaisha biashara za watu bila kuchuja ninaweza kuchagua kilicho bora (EM za bei ghali) au kilichopo (Gvt)

english medium za watu binafsi za mtaala wa necta ni magumashi hata wakikulipisha ada kubwa
 
Mpo Salama!

1. Waalimu kulipwa mishahara Duni
Unapopeleka mtoto English Medium au shule yoyote Jambo la Kwanza Kabisa lazima uulize mishahara ya waalimu. Wanalipwaje?

Mshahara wa Mwalimu ni kiashiria namba Moja kuonyesha mtoto wako atapata Elimu Bora. Matokeo ya mitihani huweza kupokwa.

Mtu Anayelipwa vizuri huwa na moyo wa kutoa kilichobora.

English Medium wengi mishahara yao inawanyonya waalimu.

Mwalimu analipwa Laki mbili, Laki tatu. Hivi huo mshahara unategemea mtoto wako ajue kingereza au apewe Elimu ya kueleweka?

Halafu wakati huo wewe umetoa Ada kubwa lengo ni mtoto wako apewe Elimu nzuri

Lazima ufuatilie waalimu wanalipwa pesa Zao kwa wakati, lazima ufuatilie wanapewa kiasi gani ili ujue watajituma kwa kiwango gani.

Lakini utakuwa mpumbavu na mjinga ambaye unatoa pesa lakini hujui Yule anayemfundisha mtoto wako atakuwa analipwa kiasi gani.

Ni muhimu wakati wa unamuandikisha mtoto uulize uongozi wa Shule mishahara ya waalimu na uwaambia unaruhusiwa kuwauliza waalimu kuhusu malipo Yao.

Kwa sababu wewe ndiye boss WA wote, mwenye shule na waalimu na wafanyakazi.

2. Umahiri wa Waalimu wa kumfundisha mtoto wako
Waambie shule kuwa unaomba nakala za Profile la waalimu watakaoenda kumfundisha mtoto wako.

Je wako qualified.

Kazi hiyo usiiachie serikali pekee. Serikali haitoi Ada ya Mwanao🤓🤓.

Ni jukumu Lako kujua wasifu WA waalimu wanaomfundisha mtoto wako sio kwa mdomo Bali wakupe nakala za Profile Zao.

Lazima ujue waalimu wapo wangapi

Waalimu wengi wa hizi English Medium hawana quality ya kueleweka.

3. CHAKULA
Shule ya serikali huwezi ulizia suala la chakula Kwa sababu labda serikali itakulipia. Si unajua chakula cha kupewa huwezi ulizauliza.

Pesa ya chakula unayotoa English Medium inaendana na chakula anachokula mtoto Akiwa shule.

Usilete akili za kitumwa kuwa mtoto hajaenda Kula shule ilhali umetoa pesa yako.

Ni lazima ulinganisha pesa yako na kile unachopewa.

4. Hutakiwi kumsaidia mtoto Homeworks anazopewa shule
Ndio maana ulitoa Pesa
.

Ni jukumu la shule kumfundisha mtoto wako aelewe kile ambacho wamemfundisha. Homeworks ilenge kujenga kumbukumbu na bangua bongo ya mtoto.

Sasa hizi English Medium wanakuandika maswali Mia moja ya Likizo alafu ukimwambia mtoto afanye hafanyi hata robo ya maswali.

Mengi ya maswali Mpaka umsaidie. Huo ni Utapeli.

Sasa mtoto anakuwaje wakwanza, au anapataje Wastani wa A Alafu Homeworks za Likizo alizopewa maswali Mia hawezi kufanya hata robo ya maswali. Huo ni Uhuni

Karibuni
Ila Walimu wananyonywa sio Serikalini au Binafsi
 
Juzi nimepeleka mtoto wangu wa Ke, shule Moja hapa jirani na Jiji njia ya kwenda Rufiji, pre form 1, wamemaliza group la wazazi likacharuka Kwa feedback mbovu mbovu, kunguni wa kutosha, maji shida kuoga mara Moja au hakuna kabisa, mtoto anachapwa akifumwa anaoga Kwa siri, kuosha chombo maji Kwa beseni na hakuna kumwaga utaoshea tena na tena. Watoto walikubwa na dhamama ya kuhara na kutapika Uongozi uka mute as if nothing happened. Nimehamisha mtoto sababu kuu maji, kunguni wanatibika japo kisingizio watoto wasilale wasome.
Kwa mzazi anaempeleka mtoto kusoma kwenye shule kama hiyo ndiye anaepaswa kushauriwa kumrudisha tu mwanae kwenye shule ya Kayumba.
 
Hela natafuta lakini siwezi kupigwa kifala kwenye shule za EM..

Siwezi kutoa hela yangu kumpa Bwana Mugetta mmiliki wa Muggeta Nursery and Primary School
The vice versa is true.

Watafika hadi chuo
 
Mimi nianze kufuatilia profile ya mwl, unisaidie nini, mshahara wa mwalimu mm unisaidie ? Nisipopewa ushirikiano maana yake nisipopewa ushirikiano nimfundishe mimi mtoto wangu?

Mamlaka za elimu zinafanya kazi gani zisikague hayo yote, haya mwl analipwa laki mbili, kwa hiyo Mimi nikamuongezee,?
Poor
 
3. Hapo namba 3 kwenye chakula siku ya kuku huwa wanalishwa kuku broiler. Kuki broiler ni kansa promax
Hio cancer inakuja baada ya muda gani? Maanake nina miaka zaidi ya 40 nakula broiler.
 
Tatizo mnafanya generalisation, kwenye nyuzi zote sijaona mnaongelea shule zipi, shule za private zinatofautiana ubora kwa vigezo mbali mbali, kuanzia kiwango cha elimu, malezi ya tabia pamoja na ada
Zipo shule nyingi sana za EM zinazotoa elimu bora ukiacha hizo mnazosema za kimataifa, ni milioni zako zinaongea acheni porojo
Hapa wanaongelewa wanaolazimisha kusomesha EM hawa obviously wako kwemye shule za ada chini ya 3m kwa mwaka.
 
Mimi nianze kufuatilia profile ya mwl, unisaidie nini, mshahara wa mwalimu mm unisaidie ? Nisipopewa ushirikiano maana yake nisipopewa ushirikiano nimfundishe mimi mtoto wangu?

Mamlaka za elimu zinafanya kazi gani zisikague hayo yote, haya mwl analipwa laki mbili, kwa hiyo Mimi nikamuongezee,?
Poor
Hujaelewa hoja ya mtoa mada
 
Muongo wewe kwanza broiler zenyewe zimeanza miaka ya elfu2
Pole sana. Broiler zipo miaka mingi sana. Wewe ndio umeanza kupata akili miaka 2000 unaona kila kitu kimeanza miaka ya 2000. Unaijua interchick ilianza kufanya kazi lini hapa Tz? Biashara yao kubwa unaijua?
 
Pole sana. Broiler zipo miaka mingi sana. Wewe ndio umeanza kupata akili miaka 2000 unaona kila kitu kimeanza miaka ya 2000. Unaijua interchick ilianza kufanya kazi lini hapa Tz? Biashara yao kubwa unaijua?
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻

Hazikuwa mtaani kivile
 
Back
Top Bottom