Kwa wenye diesel pumps za kuvuta maji naombeni ushauri wenu

Kwa wenye diesel pumps za kuvuta maji naombeni ushauri wenu

Paddy

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2010
Posts
473
Reaction score
341
Habari za leo wanaJF!

Ninahitaji diesel pump ya maji yenye uwezo mkubwa wa kutoa maji kutoka mita 200 kwenye bwawa na kuyaleta kwenye tank lililopo mita nne juu (limejengewa mnara wake).

Naombeni ushauri wa aina ya pump na horsepower (HP) zake.
 
Kujua horsepower peke yake haitoshi! Nafikiri kitu cha msingi kabisa ni kujua discharge rate au ujazo wa maji unayohitaji kwa saa!

Horsepower ya pump inafuata ukishajua kiasi cha maji unachohitaji kupump na kwa rate gani na umbali unaotoa maji mpaka unapoyapeleka (hapa itakubidi uzingatie tena head loss due to friction)

Ukiniambia uhitaji wako wa kupump maji kwa saa ninaweza kukushauri pump gani itakufaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshapata suluhisho, kuna pump inao huo uwezo mkubwa sana nimeshanunua lakini ni ya petroli inayolingana na bajeti niliyokuwa nayo. Nimeipata kutoka kwa kampuni ya Davis & Shirtliff.
 
Back
Top Bottom