Hahahaha mimi kitu nilichofanya nikaja kujutia lkn sasa hivi majuto yameisha ni kwamba ktk biashara zangu nilifanikiwa kuwa na saving kubwa. Sasa nilipokuwa nimepanga nyumba watoto wa kike wa mama mwenye nyumba walikuwa waanichokonoa sana kwa kero za kila namna sijui ilikuwa ni wivu maana nilikuwa dogo nina shughuli zangu wao wanashinda home tu!
Siku moja kero zikanizidi rohoni nilikuwa na kiwanja nikatafuta fundi ujenzi nikamwonyesha ramani akafanya quotation, bila kufikiria nikajenga nyuma nzima hadi ikaisha nikahamia na visent vyangu benki navyo vikaisha na biashara ikayumba halafu sikuwa na hela za kuisave biashara, nilitamani kuchanganyikiwa na jumba nilliliona kama kaburi, watu walikuwa wananipa hongera wanasema mambo yako supa lkn walikuwa hawajui rohoni nilikuwa na crisis!
NAMSHUKUU JEHOVA HIRE AMENIVUSHA NA SASA NAENDELEA VIZURI TENA lkn nilijifunza mambo mengi kutokana na kosa hilo.