Wanajamvi!
Enzi za medani ni medani kweli, nazungumzia enzi zile "Jumba jeupe" kuna watu wenye akili timamu, weledi, maarifa, wivu na uzalendo mkubwa sana kwa watu na nchi yao.
Enzi ile kabla ya "vetting" haijabadirika ya kuingiza "vilaza" kwenye medani bila vipawa.
Naam, enzi ile ambayo Spy Chief/Spy Master iliweza kufahamu yajayo kwa usahihi kabisa, huku ikishauri namna bora ya kukabiliana nayo kiweledi na kimkakati bila kuliumiza taifa, wala kulitia doa.
Kwa yaliyotokea nchi ya Zimbabwe, katika mji mkuu wa Harare, kuanzia tarehe 29/10/2025 ni wazi kwamba ofisi ile na vijana wale walipwaya, walishindwa kutekeleza moja ya jukumu lao kubwa, la kutazama (foresee) yajayo yasiyotizamika wala kufikirika "The unthinkable". Ofisi ile haikutimiza wajibu wake wa kuwapa taarifa sahihi na kuwashauri " Waamuzi". Ukishindwa kupanga, umepanga kishindwa. Na huwezi kupanga bila kuwa na taarifa sahihi. Utadesa tuu.
Waamuzi "Decision Makers" wa nchi ya Zimbabwe, kuelekea tarehe 29/10, walikuwa hawana taarifa sahihi "Information gap", kulikuwa na kulishana matango pori, kufanya mambo kwa mazoea, propaganda za kitoto, kiburi na ghilba, ubabe na "taarabu".
Wa kulaumiwa sana na kuliwa kichwa kwa haraka, kwa doa lile, ni bosi wa "Jumba jeupe" na vijana wake. Nimetaja wajibu wake huko juu.
Mpaka kufikia tarehe ile, Zimbabwe kulikuwa hakuna "picha" halisi ya nini kinaenda kutokea, kivipi, namna gani, wapi na itakuwaje. Ni kawa nchi ya Zimbabwe ilikuwa likizo hivi.
Na ndipo utaona pakawa na taharuki (Panic) pale Zimbabwe, na namna bora ikaonekana ni kuus bila kubagua yeyote, mwanamke, mtoto au Mzee. Wanawake na watoto kweli wakauwawa nchini Zimbabwe.
Wazee wa kazi, Medani zinabadirika, kizazi kinabadirika, mmeshapeleka watoto shule, na wamekuwa wengi sana mtaani, hamuwezi endelea na namna ile ile ya kudeal nao kwa ubabe, mkono wa chuma na vitisho kama ambavyo mlivyokuwa mnakamata baba zao enzi za Oparesheni vijiji na Maazimio yale.
Kijana aliezaliwa mwaka 1998,2000, akasoma shule kufikia kidato cha nne, hajui kama taifa la Zimbabwe lina utamaduni wa ubabe, kujenga hofu, kuteka, propaganda, kuumiza na kuwekwa kizuizini kam njia ya jadi na ya siku nyingi ya kutawala.
Kijana huyu haogopi, hajajengewa hofu ya enzi za "chama kushika hatamu". Hajaishi zama hizo, hazijui ana dunia yake. Mnamlazimisha aishi zama ambazo hazijui, na elimu mliyompa inamwambia sio sawa. 😁
Mkiendelea kutumia mbinu (Za Uwimbombo na Ulindi) ambazo hawazijui kuwadhibiti vijana hawa, mtajikuta mpo nao barabarani mnapigana, na watakuwa wanajifunza taratibu kupigana na nyinyi, na ipo siku watajua namna ya kupigana na nyie, na silaha hizo hizo mnazowapigia, watazitafuta au kuchukua za kwenu hizo hizo. Mtawashindwa na kuwaua kwa muda fulani, lakini hamuwezi kuwashinda na kuwaua muda wote. Ipo siku watafahanu namna nzuri ya kupambana na nyie, na hakuna rangi mtaacha kuona.
Kama ilivyokuwa tarehe 29/10. Mtajikuta mnapigana na watoto wenu wenyewe, na mtaanza kuambiwa mataifa ya magharibi mnawaua watoto wenu wenyewe. Hakuna atakae kuwa upande wenu, itaonekana ni baba/mama ameshindwa kulea watoto wake mwenyewe. Mfano mzuri ni wakati, mnajiapiza, mlijikuta mpo wenyewe wenye akili wamewafungia vioo.
Mtapewa kila aina ya majina kwa kuua watoto wenu wenyewe, madikteta, wauaji, shumileta, na mabepari yataanza kuona namna ya kuchukua rasilimali zenu kupitia ugomvi wenu wa kukosa akili, kuwashitaki na kuwapa hao hao vijana mbinu ya kukabiliana na nyie siku za usoni. Ujinga ni gharama.
Kijana huyu hajashuhudia zama za "Mchonga" wala zama za "Ruksa". Zama za Ma RC na Ma DC wanatembea na viboko kwemye Land-rover zao! 😁. Zama ambazo Mkuu wa mkoa anaweza amrisha uchapwe viboko, wewe na mke wako na mkachapwa kweli. 😁
HOJA YANGU: Taarifa sahihi na ushauri sahihi wa kukabiliana na hali ile ilipaswa kutoka "Jumba jeupe" siku nyingi, kungekuwa shwari tuu. Nitashangaa sana kama ataendelea kuwa ofisini!