Kwa yanayoendelea Arusha na RC Makonda, ni dhahiri watumishi wa umma wengi ni wazembe na hawana sifa!

Kwa yanayoendelea Arusha na RC Makonda, ni dhahiri watumishi wa umma wengi ni wazembe na hawana sifa!

Ukweli ni kwamba, watumishi wengi ni wavivu wa kufikiri na hawajui kujieleza.

Kuna muda wanafanya mambo mtu unaliangalia unasema hili linaweza kufanywa na mtu mpumbavu tu. Uvivu wa kufikiri ni tatizo kubwa sana
Tunaposema mfumo mzima wa Utumishi wa Umma umekwama ni pamoja na HIRING PROCEDURES kwenye Utumishi wa Umma. Maneno tu ya mtumishi yanakushangaza! Kwani hukuwahi kusikia mgonjwa wa kufanyiwa upasuaji wa mguu alifanyiwa upasuaji wa kichwa na yule wa upasuaji wa kichwa akafanyiwa upasuaju wa mguu kwenye hospitali kubwa tu ya taifa! JPM alipokuja na zoezi la vyeti fake mbona wengi mlipiga kelele! Civil service needs total overhaul.
 
Je umewahi kuona mwanasiasa yeyote akifanyiwa kama huyo RC anavyofanya?
Huko tulikonakili huu mfumo wa uongozi kwa asilimia kubwa uwanja upo sawa, huyo RC naye anahitaji chemsha bongo hadharani.
Raisi, wazuri ..... akimaliza kuongea anaingia kwenye ndinga anaondoka, hakuna maswali
 
Kuna umuhimu gani zoezi hilo kufanyika mbele ya kamera? Kwa hakika ni udhaifu wa mfumo mzima wa Utumishi wa Umma. Wanataka kuaminisha umma kuwa ni udhaifu wa mtumishi mmoja mmoja kitu ambacho ni uongo. Uongo ndiyo kawaida yao. Waongo tu.
Camera ndio wanamfuata makonda kupata habari na hawezi kuwafukuza
 
Je umewahi kuona mwanasiasa yeyote akifanyiwa kama huyo RC anavyofanya?
Huko tulikonakili huu mfumo wa uongozi kwa asilimia kubwa uwanja upo sawa, huyo RC naye anahitaji chemsha bongo hadharani.
Raisi, wazuri ..... akimaliza kuongea anaingia kwenye ndinga anaondoka, hakuna maswali
Hapo ndipo wanasiasa wanaonekana wapo juu ya kila kitu, ndomana Matajiri mfano akina Shabiby, Mo walikimbilia Bungeni ili kujiweka Salama zaidi.

Siasa zetu zina mfumo kandamizi sana ziko Biased mno
 
Camera ndio wanamfuata makonda kupata habari na hawezi kuwafukuza
Na Clips zao zinapata Views lukuki huko Youtube, na wavyoandika Headings za kusisimua lazima wapate trends
 
Huyu makonda anapaswa kuwa wa kitaifa na si wa mkoa. Rais ana nafasi zake za kuteua wabunge kumi, kwani zimeisha? Amteue kuwa mbunge na kisha ampe uwaziri, wizara nyeti aondoe uzembe na ubadhirifu kwa watumishi nchi nzima.
 
Back
Top Bottom