Kwa yanayoendelea Bara na Visiwani bado una hamu na Siasa za Tanzania?

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,451
Reaction score
2,466
Sina muda wa kuandika magazeti.

Bara kuna kundi limechukua pesa ili wasaliti wenzao waende bungeni. Bado mna imani nao? Kutokana na figisu za uchaguzi bado una imani na siasa?

Visiwani Kulikua na vurugu kuliko bara. Mara uchaguzi tar 27 mara tar 28 changanya na kura fake sijui watu kupiga na wanajeshi mara wanajeshi wa Burundi sijui viongozi kupigwa wa upinzani wengine kutekwa n.k

Leo kuna wale walalamikaji wameungana na walalamikiwa sasa hapo wafuasi wanabaki upande gani? Zile tuhuma zitafutwa ama?

Hivi inawezekanaje kuendelea kushabikia siasa? Kwanini watu wasishabikie mipira kuliko siasa? Swali kwa kila mtanzania una imani na watu gani Tanzania?

Bora tuendelee kuomba na kusubiri ufalme wa Mungu uje ili utimize mapenzi yake na sio kutegemea falme za wanadamu.
 
Tatizo siasa ni maisha ya kila mtu, ushabikie usishabikie siasa itaendelea kuwa maisha ya mwananchi.

Ccm na vyombo vyake wanajua udhaifu wa washindani wao. Kadhalika hawako tayari kuachia madaraka kwa njia ya kura. Labda njia ile nyingine wasioipenda watu . Pia vyombo vya dola na vya maamuzi havijawahi kutenganishwa .
 
Kabla ya demokrasia na chaguzi za marais watu walikuwa wanaishije? Kwanzia mwanzo wa uimbaji hadi mwisho wa utawala wa Roma? Kulikua na chaguzi? Watu hawakuishi?
 
Tatizo Tanzania ilipokea mfumo wa vyama vingi ki nafiki. Walibadili baadhi ya sheria za uchaguzi kuruhusu mfumo wa vyama vingi, lakini katiba ikabaki sehemu kubwa ktk mfumo wa chama kimoja kushika hatamu.

Na walipogundua hilo walihiari pesa za mabadiliko ya katiba zipotee bure. Mradi wasiwe sawa mbele ya vyombo na vyama vingine.

Angalia Ghana iliyorekebisha katiba kuendana na mfumo huo kama kuna fujo za hovyo, hasa kwa wapinzani !!. Sisi bado tuko ki communist zaidi
 
Kiufupi mabeberu ndo walilazimisha tuhamie kwenye huu mfumo bila matakwa yetu mwisho wa siku ndo mambo kama haya
 
Tatizo Tanzania ilipokea mfumo wa vyama vingi ki nafiki. Walibadili baadhi ya sheria za uchaguzi kuruhusu mfumo wa vyama vingi, lakini katiba ikabaki sehemu kubwa ktk mfumo wa chama kimoja kushika hatamu.

Na walipogundua hilo walihiari pesa za mabadiliko ya katiba zipotee bure. Mradi wasiwe sawa mbele ya vyombo na vyama vingine.

Angalia Ghana iliyorekebisha katiba kuendana na mfumo huo kama kuna fujo za hovyo, hasa kwa wapinzani !!. Sisi bado tuko ki communist zaidi
Basi ndugu yangu kama walijua hilo #katiba ni ile ile mambo ni yaleyale badi tuyapishe kwanza afu siku yakirekebishwa ndio mfumo uanze wa vyama vingi
 
Ukijitoa, nani atarekebisha hali kama si wewe na mimi ?!. Viongozi wengi hasa wa Africa hukubali kukaa mezani kwa shinikizo si kwa hekima. Trump angelikuwa Africa angelifia madarakani kwa hulka yake. Lakini wenzetu taasisi zina nguvu kuliko viongozi. Africa viongozi wana nguvu kuliko taasisi.
 
Utatumia njia gani kuhakikisha mawazo yako yanakubalika? Au taasisi inakua kubwa kuliko kiongozi?
 
Back
Top Bottom