Kwa yanayoendelea CHADEMA, na suala la Abdul bado mnaamini saini kwenye barua ya kuwaidhinisha kina Mdee ilifojiwa?

Mnyika na Mbowe walihusika kwa asilimia 100, hakuna saini iliyokuwa forged, baraka za Mbowe zilitolewa.N

Nami naunga MKONO HOJA tena nahisi aliyesaini na kuandaa hizo minutes za kikao kwa niaba ya CC ni huyo cha Ujanja Kigaila..nadhani Lissu ameamua kufunua kapeti yenye UOZO na inaonekana amejipanga...amewatupia hili kombola la ABDUL ngoja wahangaike nalo,kabla hajatupa jingine ..WATAIBIKA
 
Tuacheni unafiki, ni nani angeikataa pesa kwa malipo ya kuanguka Saini na kugonga muhuri tu?? Binafsi ningeichukua vinginevyo hujui duniani umekuja kwaajili ya nini.
Selfish and low thinking altogether
 
Selfish and low thinking altogether
Natamani siku Moja watoto wako wapokee Hela mahala alafu wakuuze. Na kwa ufahamu wako nadhani utawashukuru na kuwasifu, maana wanajua kilichowaleta Duniani.
 
Inaumiza sana, hiki chama sisi wafuasi na wanachama tuliamini ndio mkombozi pekee aliyebaki kutuvusha watanganyika. Toka tukiwa vyuoni tume risk maisha yetu kwa kuwa wafuasi wa chama huku maofisini kuna watu nawafahamu wameachishwa kazi sababu ya kuwa wafuasi wa CDM, leo hii tunapokuja kuona kumbe na wao ni ganga njaa inaumiza sana. Itoshe kusema CCM watatawala hii nchi kwa miaka mingi mbele labda utokee muujiza toka Mbinguni ccm ife bila hivyo hakuna wa kukitoa.
 
Pascal Mayalla aliwahi kuleta uzi humu kwamba CHADEMA kuna kirusi kinawatafuna na kipo ndani kabisa kwenye chombo chao cha maamuzi.
Mkuu Krime, Crimea , hii
ndio naiona leo CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind? Na CHADEMA kuna kirusi! Je, unajua kirusi hiki ni nani?! Na the motive behind?
Tuliambiwa sain za kwenye barua ya kuwaidhinisha kina Mdee kuwa wabunge wa viti maalumu ilifojiwa. Lakini kwa haya yanayoendelea pale chadema Naamini ile barua haikufojiwa bali ili toka kwa kiongozi mkubwa probably Mbowe kwa maslahi yake.
Hili niliuliza humu Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
P
 
Kuna mtu kauliza, kwanini hakwenda kushitaki forgery?
 
Mbowe hajang'ang'ania madaraka
Kang'ang'ania ndio maana alitumia ushawishi wake kuondoa ukomo wa madaraka, ambapo viongozi wengi walio mchallage CDM kwenye suala la uwenyekiti waliishia kufukuzwa au Dola kuwaondoa Ili kumlindia kiti chake TISS mkuu wa upinzani.
 

Paschal week hii umeamua, very thoughtful subject and content!
 
Mnyika na Mbowe walihusika kwa asilimia 100, hakuna saini iliyokuwa forged, baraka za Mbowe zilitolewa.
Unayosema yana mashiko.

Kama sahihi zao zilighushiwa, tungeliona wanauza sura kwenye viunga vya mahakama kwenda kushitaki, lakini kimyaaaa, mpaka kesho!
 
Kila chama kina mapungufu yake, haya ya CHADEMA yana nafuu kubwa kuliko kwingineko
wengine hata uchaguzi hawana Mwenyekiti huteua na kutengua muda wowote.
 
Pesa za Abdul zimeichafua Sana chadema na mbowe wake kiujumla
 
kwahiyo kwa ujumla yote hayo,
ni kwamba nyote mna nimani haba, lakini pia hamuaniani kabisa? right?

Jibu ni moja tu, Amini Mungu πŸ’

πŸ’
Bosi tulia basi kwanza, unaonekana una hoja nzuri lakini umekosa utulivu kwenye kuandika. Binafsi sijapata muunganiko wenye kuleta maana kwa namna ulivyowasilisha maoni yako.
 
Bosi tulia basi kwanza, unaonekana una hoja nzuri lakini umekosa utulivu kwenye kuandika. Binafsi sijapata muunganiko wenye kuleta maana kwa namna ulivyowasilisha maoni yako.
Legeza mindset yako gentleman, ni rahisi mno kuelewa jambo hili πŸ’
 
Kwa kweli sasa tushajua chair aliwazunguka wenzake.🀣🀣🀣🀣
 
Unayosema yana mashiko.

Kama sahihi zao zilighushiwa, tungeliona wanauza sura kwenye viunga vya mahakama kwenda kushitaki, lakini kimyaaaa, mpaka kesho!
Hakuna aliyeenda shitaki mahakamani kwamba saini zimefojiwa, mahakamani ilienda kesi ya uanachama wa covid 19 na sio kesi ya jinai ya kufoji.

Kigaila Mke wake ni Covid 19, its not a concidence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…