Kwa yanayoendelea, napoteza imani na Idara ya Usalama wa Taifa, napoteza imani na CCM kama inaweza kutuvusha kiuchumi na kimaendeleo. Uzalendo hamna

Umasikini wa kutupa ndio maana hata malezi yanakuwa ni shida !
Watoto wanalelewa na majirani au na wadada wa Kazi !
Baba na Mama wako kwenye mishemishe ili mkono uende kinywani !
Hapo utamlaumu nani ??!
Kwa Wazungu zipo pesa maalum za kulelea watoto wanapewa Mama zao wawalee vizuri !
Unaona tofauti yetu ??!
 
Pole sana mkuu kwa kuvunjika moyo kiasi hicho.Ila mi naona JWTZ ni chombo ambacho nchi nyingi za Africa znaweza kujifunz kwao.Mengne ni mapungufu ya wachache miongoni mwao na syo ya kimfumo kama ilivyp kwa idara zngne.
May be. Thank you
 
Vichwa vya dizel ni kwa ajili ya dharura ikitokea umeme umekata, ni sawa na kuwa standbye generator kwenye hospitali.
 
Ni kweli kwa baadhi ila pia taifa linaangamia kwa hao wanaoliongoza kwa kuiba mali za umma
Na ni kweli umasikini unasababisha mengi lakini kuna masikini sio waizi pia
Hao wanaoenda kufanya shughuli za utafutaji wana uwezo pia wa kuwafundisha watoto nidhamu maana nidhamu haihitaji hela bali akili tu
Mzazi huoni anatoka na watoto au mtoto hata masaa mawili kutembea nae
Wazazi wengi ni maadui kwa watoto sasa mtoto anakuwa hata nyumbani anapaona pachungu

Akienda nje anakutana na watukutu huko maana hawezi kukutana na wema wakizurura hovyo
Basi nae anakuwa kibaka tu
Hata Ulaya watukutu wapo tena wengi wameingia kwenye kuuza madawa ya kulevya wakiwa wadogo kisa wazazi.wameachana
Kila leo kuna mauwaji hapo nilipo, vijana wadogo wanachomana visu sana
Lakini hawana fursa kwingine
 
Well said
 
Wakuu, mi nashauri Hawa watu ni kuwapiga risasi au sumu, bila hivyo inchi itapotea hii.
 
Kila siku vijana wana graduate course za logistics, wapewe KAZI, Kadogosa aende shamba akalime
 
Usipoteze imani na muda kutegemea kuvushwa na Chama Cha Machawa (CCM).
 
Tiss ipo kuakikisha ccm inakaa milele,
Idara ya usalama ni overseer wa yote, mshauri wa yote, mkemeaji wa yote na mzuiaji wa hujuma zote, hilo ndio jukumu lake la msingi

Ni lazima wabadilishe Mifumo yao yote kabisa, ikiwemo na kubadilisha utaratibu Wao wa RECRUITMENT ya Maafisa wao.

Hili ni jambo la lazima kabisa ambalo haliwezi kuepukika kwa Sasa katika Idara hiyo.
Ni Lazima Wabadilike ili kuendana na Mahitaji halisi ya Dunia ya dunia ya Sasa.

Mamlaka Kuu ya Ujasusi ya Marekani ya CIA Baada ya Mashambulizi makali Sana ya kigaidi yaliyofanyika katika Kituo Kikuu Cha Biashara Cha Dunia (WTC), Pentagon, n.k hapo tarehe 11 Septemba 2001, CIA walikiri kwamba kulikuwa na Mapungufu makubwa Sana kwenye Mifumo ya Utawala, Mifumo ya Kuajiri Maafisa wa Taasisi hiyo na kwenye Mifumo ya Kiutendaji ndani ya CIA hali ambayo ilisaidia Sana kutoa mwanya kwa Magaidi wa Al Qaeda chini ya Osama bin Laden kuweza kuishambulia Marekani kwa urahisi Sana.

Baada ya mashambulizi hayo ya kigaidi ya September Eleven, CIA ilifumuliwa na kisha kusukwa tena upya. Kwa sasa, Maafisa wa Idara hiyo ya CIA Wanaajiriwa kwa utaratibu wa kutoa Matangazo ya Ajira zao kwenye vyombo mbalimbali vya Habari. Hii inawasaidia kutoa wigo mpana zaidi wa kuwapata Watu/ Waajiriwa mbalimbali walio sahihi zaidi, wenye weredi katika fani tofaufi tofaufi wakiwa na mitazamo tofaufi tofauti kinyume na hali ilivyokuwa hapo awali kabla ya mashambulizi ya 'September Eleven.'
 
Hapa tatizo ni mifumo miwili ya nchi iko na ganzi
1. Bunge
2. Mahakama
Mfumo wa Excutive unajipigia upendavyo unaweka bunge na mbunge yule wanataka na msimamizi au mtofasri sheria yule unataka.
Hivyo mifumo yote kazi nikupigia makofi excutive chini ya chama cha siasa.
Totalky rubbish
 
Kila kamba inakula urefu wa mbuzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…