Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
- Thread starter
- #21
Nimekuelewa sana.Mkuu Lord Denning, nimeelewa maana ya unachokisema kuhusu Tanzania kupeleka jeshi lake Congo ili kuwazima waasi wa M23 au hao wanaowasaidia.
Ni kweli,ili Tanzania inufaike katika mnyororo wa biashara na uchumi na Congo DRC utategemea zaidi utulivu na hali ya amani ndani ya Congo na nchi jirani zake.
Hata hivyo kwa hali ilivyo siyo rahisi kwa Tanzania kuingilia kijeshi waziwazi kuisaidia DRC kulingana na siasa zetu za Africa mashariki zilivyo. Kama Tanzania itaingilia ,iwe kwa makubalino na masharti ya Congo kugharimia kwa namna fulani baadaye....lazima hayo makubaliano yatakuwa ya siri,na jeshi la Tanzania halitaingia kwa uwazi.
Tanzania iliingia kwa uwazi kipindi cha Jakaya kwa mara ya kwanza huko Congo na kuwakimbiza M23,lakini ilikuwa ni kwa mgongo wa azimio la AU. Japo huo uamuzi wa Tanzania kukubali kupeleka jeshi Congo ukafanya Kagame amkasirikie Jakaya.
Lakini hili ulilosema kwamba Kagame akichekewa,mwishowe atavamia Tanzania ni jambo la kufikirika sana kuliko hali halisi.
Pengine watu wengi hawaelewi jambo moja, jeshi la Rwanda la sasa kimsingi limetokana na kile kikosi cha waasi cha RPF ambacho wanachama wake wote walikuwa katika jeshi la Uganda. Wanachama wote wa RPF pamoja na Kagame walikuwa katika kikundi cha waasi kilichoongozwa na Yoweri Museveni,NRM ambacho kilipewa mafunzo ya kijeshi na JWTZ na baadaye kujumuishwa katika jeshi la Tanzania kuisaidia Msumbiji na baadaye katika vita ya Kagera.
Fred Rugyema na akina Kagame ..na kama ilivyo kwa waanzilishi wa RPF kule Uganda, wote walikuwa ni zao la wakimbizi toka Rwanda waliongia Uganda na wazazi wao wakiwa wadogo. Rugyema na Kagame mathalan,walikuwa na miaka 2 tu...huku wengi katika RPF walizaliwa na kukulia Uganda.
Baada ya kuingia maarakani mwaka 1986, Museveni akatimiza ahadi ya kugharimia akina Rugyema kuanzisha RPF ili kikaiondoe serikali ya Rwanda madarakani.
Nnachotaka kusema hapa ni kwamba jeshi la Uganda kwa kila kitu ni zao la JWTZ,kama ilivyo hata kwa jeshi la Rwanda na M23 yenyewe. Nyimbo za kuhamasisha wakati wa mafunzo jeshini zinzoimbwa na majeshi ya Rwanda,M23 na Uganda ndo hizo hizo walizofundishwa na JWTZ....wanaimba kwa kiswahili japo hawakielewi.
Kwa muundo huu, pamoja na masuala mengine...jeshi la Kagame ni mtoto mdogo sana kufikiria kuipiga Tanzania.
Ila kama ulivyosema, na umeeleaeka kwamba ni muhimu mno wachokozi eneo hilo wakatulizwa. Lakini kwa uwazi....,no way.
My point here ni kwamba, it's high time kwa Tanzania kubadili sera yetu ya Mambo ya Nje hasa kwenye eneo la engagement zetu za maeneo ya migogoro. Inawezekana mwanzoni tulikuwa tunaingia kwa nia za kusaidia au baada ya resolutions za UN au AU ila kwa sasa tuanze kuingia kwa maslahi yetu ya kiuchumi.
The goal of Kagame and Museveni ambao umekiri pia ni mazao yetu ni to put a lot of pressure by all means possible ili yale maeneo baadae yajitenge na kuwa annexed kama sehemu ya mataifa yao.
Contrary to 2012 ambapo kulikuwa na viongozi wanaojua hii migogoro vizuri na kufanya maamuzi ambapo nia zao hizo hazikutimia ila saivi wanaonekana wako determined kweli na kwa namna dunia inavyowabembeleza it's seems they are going to achieve this goal.
Congo kwa sasa ni kama ameachwa. Hakuna anayemsaidia kweli. Na it's obvious anahitaji sana msaada saivi kuliko wakati wowote ule.
Swali ni Je hatulioni hili kama fursa? Kwa nini tusiitumie hii kama fursa rasmi? Alafu kumbuka if we do it in Congo today tutakuwa tumefanikiwa ku set a very good precedent na kesho mwingine akiwa na shida atakuja kutu engage na pia tutamsaidia on the same terms za kuangalia maslahi ya kiuchumi.
Ni bahati mbaya sana saivi Viongozi wetu wanaangalia maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa ila if ningekuwa Rais wa Tanzania leo mpaka muda huu ningekuwa nimesha saini makubaliano na Rais wa Congo na vijana wangu wapo kazini tena kwa Tangazo la wazi.
Congo anachokosa ni support ya uhakika kwenye kupambana na ule uharamia ila when it comes to fedha, anazo za kutosha sana.
Saivi Congo analipa vikosi binafsi kutoa ulinzi kwenye maeneo yake. What if hizo hela zote angetulipa sisi tukaweka Military Base zetu hata mbili kule Mashariki mwa Congo na vifaa vya uhakika?
Unadhani tukifanya hivi na wananchi wa Congo wakaona na waka experience matunda yake, Kesho wawekezaji wetu watakuwa na influence kiasi gani nchini Congo?
Niliandika uzi jana kuuliza kuhusu ni kina nani Think Tanks wetu?
Niseme ukweli, umaskini wa Tanzania ni wa kujitakia maana fursa zipo kibao ila tunaongozwa na vilaza ambao hawawezi kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.