Kwa Yanga hii,Kaze utakosolewa na kushutumiwa sanaaa

Kwa Yanga hii,Kaze utakosolewa na kushutumiwa sanaaa

Baada ya sare kadhaa kwenye ligi wachambuzi wa soka walimshutumu na kulaumu mbinu za Kocha wa Yanga hali iliyopelekea Kaze mwenyewe kutoka hadharani na kueleza kusikitishwa na namna wachumbuzi wa soka nchini wanavyomsema na kukosoa mifumo yake.

Kwa mtu mwenye ufahamu na uelewa mzuri wa mpira ataungana nami kwamba kocha Kaze ameshindwa kuitengeneza timu. Kila mchezaji anacheza kivyake. Viwango vya wachezaji vimeporomoka sana.

Mashambulizi yanayotengenezwa na washambuliaji wa Yanga ni rahisi kuyatabiri.Wachezaji hawana ubunifu kabisa katika eneo la mwisho.

Kwangu timu inapokosa mbinu,mtu wa kwanza kulaumiwa ni kocha na Kaze ajiandae kisaikolojia. Endapo timu itaendelea na mwenendo huu basi atakosolewa sanaa.

Kama hataki kusemwa basi lazima abadilishe kitu kwenye timu.
Mtashangaa,yanga hii hii ndio itachukua ub8ngwa wa nchi
 
Wewe ni shabiki halisi wa Yanga! Hakika wachezaji walio wengi wa Yanga ni wa kawaida sana! Hasa wale wa kikosi cha pili.

Hata wakati wa usajili, baadhi tulilamikia humu usajili wa wachezaji kama Waziri Junior, Zawadi Mauya, nk. Huwezi kulinganisha na Mikia Fc! ambao hata wachezaji wasio na namba kwao, bado wakipewa nafasi wanafanya kitu. Sisi timu yetu asipokuwepo Mukoko pale nyuma, ndiyo basi tena!

Washambuliaji wetu ni butu! Usajili wa mwalimu nao ni majanga tu! Huyo Saido ni spana mkononi! Fiston nae anaruka ruka tu uwanjani! Hana kabisa match fitness!! Kiukweli tunatia huruma kwa kiasi fulani.
point of correction,sijawahi kuwa shabiki wa Yanga!!!😀😀 kiukweli nawasikitikia sana Yanga kwa jinsi wanavyolalamikia kila kitu. watalalamikia marefa, watarudi kwa tff, wataenda kwa kocha, mara Morrison yaani ni mwendo wa malalamiko kila uchwao bila kuangalia ishu ya msingi.
labda kwa kuwasaidia tu, hakikisheni mna wachezaji wenye quality kisha hakikisheni mnawa-train wachezaji wenu wajue kwamba ushindi ni uwanjani na waachane na kutegemea kupata ushindi kwa janja janja!!
Mashabiki wawajibisheni viongozi wenu na sio kuanza kunyoosha vidole kwa wasiohusika na kucheza uwanjani. hivi kwa mfano timu uwanjani haitengenezi nafasi za wazi hata 2 kwa dakika zote 90 kisha ikipoteza points mnaanza kulalama mara refa, mara tff. Hebu hao wachezaji watengeneze nafasi zaidi ya 5 uone kama kuna malalamiko mtayapeleka kwa marefariii.

kwa sasa acha sisi mikia fc tutambe😛 maana tuna focus zaid kuwaandaa wachezaji kupata matokeo uwanjani kwani wana hiyo quality
 
Ni Tanzania tu kocha ambaye hajafungwa hata mechi moja kwenye mashindano yote aliyocheza anaimbwa kua mbovu. Shida ni ushabiki, simba akishinda tatu, basi na yanga ashinde tatu ili kijiweni story zibalansi.

Simba ipo pale kwa zaidi ya miaka 3, wachezaji wengi wamekaa kwa mda mrefu na usajili wao ni wa kuziba gap ndogo ndogo... Yanga msimu huu karibu kikosi chote cha kwanza ni kipya! Kocha ana struggle kutafuta mfumo na chemistry, ndio maana anabadili na kununua wachezaji kwa mikataba mifupi mifupi ya miezi 6 ili kupata watu wa uhakika. Mafanikio ni suala la mda and not an overnight process!!! Ila bongo nyosooo

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
tatizo la Yanga ni pamoja na wachezaji tusimlaumu kocha peke yake. kwa ukubwa wa Yanga kuna lundo la wachezaji hawana hadhi ya kuwepo kikosini. wajitathimini wachezaji wao kama wana hiyo quality ya kuwa 'Wananchi'
Ukubwa gani wa Yanga?
 
Kaze sio kocha kabisa yani Hua hajiongez yani nchimb sijui anampanga kwa nn pia kocha angekua na akil angeweza kujua kua kila calinho anavyo ingia basi team mbele Hua inacheza mpira wa kutulia Sana angalia mechi zake zote calinho lazima awe ametengeneza pasi au kafunga

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
kwani huyo Nchimbi alisajiliwa ili afanye nini zaidi ya kucheza? ndio mshambuliaji tegemeo wa timu sasa kocha alaumiwe kwa lipi,,, 😀
 
Timu daraja la nne kaweka full squad... na wanashinda kwa kabao kamoja ka Penalty...

Yanga bila Penalty....

Angefungwa na Simba kwenye derby
Asingeingia nusu fainali kombe la Mapinduzi
Asingecheza fainali kombe la mapinduzi
Asingeshinda mechi ya Azam FC na timu daraja la nne
Asingetishia kujitoa kwenye ligi kama angefungwa na Mtibwa...

Yani litimu linapambana lipewe penalti ili lishinde...

No penalty No Utopolo...
Tunakamiwa mno
 
umen
Ni Tanzania tu kocha ambaye hajafungwa hata mechi moja kwenye mashindano yote aliyocheza anaimbwa kua mbovu. Shida ni ushabiki, simba akishinda tatu, basi na yanga ashinde tatu ili kijiweni story zibalansi.

Simba ipo pale kwa zaidi ya miaka 3, wachezaji wengi wamekaa kwa mda mrefu na usajili wao ni wa kuziba gap ndogo ndogo... Yanga msimu huu karibu kikosi chote cha kwanza ni kipya! Kocha ana struggle kutafuta mfumo na chemistry, ndio maana anabadili na kununua wachezaji kwa mikataba mifupi mifupi ya miezi 6 ili kupata watu wa uhakika. Mafanikio ni suala la mda and not an overnight process!!! Ila bongo nyosooo

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
umenena ukweli mtupu...yani timu haijapoteza mchezo wowote wa ligi lakini hawana uhakika wa kuchukua ubingwa! inabidi wawe wavumilivu
 
Lamini ana mpira, pasi kwa Mwamnyeto , pasi kwa tonombe halafu pasi ndefu kwa Kisinda. Ndiyo mfumo wa uto.

Raha yao na mbinu zao zote ni kumwona Kisinda anatimua mbio.
 
Timu daraja la nne kaweka full squad... na wanashinda kwa kabao kamoja ka Penalty...

Yanga bila Penalty....

Angefungwa na Simba kwenye derby
Asingeingia nusu fainali kombe la Mapinduzi
Asingecheza fainali kombe la mapinduzi
Asingeshinda mechi ya Azam FC na timu daraja la nne
Asingetishia kujitoa kwenye ligi kama angefungwa na Mtibwa...

Yani litimu linapambana lipewe penalti ili lishinde...

No penalty No Utopolo...
Penalty ni part ya mpira kaka,
Ukifanya kosa unaadhibiwa
 
Back
Top Bottom