Kwa yeyote aliyewahi kuagiza gari online with SBT Japan.

Kwa yeyote aliyewahi kuagiza gari online with SBT Japan.

Gari ya kwanza nimeagiza enhance auto tena bila hata kufika ofisini kwao, nikatumiwa invoice nikalipia crdb, gar imefika poa kabisa. Ya pili hivyohivyo ilikuwa ka polo tena kalikuwa kamoja. Sasa imeagiza ist auto jp nimelipia wiki iliyopita nasubiri ije mjini nipige bei
 
Sbt wako poa sema magar yao sio makali, mileages kubwa. Nenda enhances auto hawa wako poa, wana gar chache lkn zimesimama

Mi nimeagiza gari nyingine kupitia autojp, wana discount ya dola 300. Nimeng’oa ist kali matata, mpk inafika itakula 10.6m

Huko Autocomjp nimeikosa gari nayotaka. Nikaipata SBT. Ni IST ncp65 (yenye 4WD). Huko SBT nimepata ya mwaka 2004, mileage 98,000 KM.

Ila pia kuna nyingine nimeipata Enhance Auto, ila umri wake sasaa... ni ya mwaka 2002, mileage 81,000 KM. Hii pia bado naifikiria. Lakini kwenye auction Inspection Sheet yake ina Dents (D1) kama tatu hivi.
 
Gari ya kwanza nimeagiza enhance auto tena bila hata kufika ofisini kwao, nikatumiwa invoice nikalipia crdb, gar imefika poa kabisa. Ya pili hivyohivyo ilikuwa ka polo tena kalikuwa kamoja. Sasa imeagiza ist auto jp nimelipia wiki iliyopita nasubiri ije mjini nipige bei

"Auto Jp" unamaanisha autocom Japan?
 
Uzoefu wangu na SBT:unachoona kwenye picha ndicho hicho kitakachokuja. Nimeshadeal nao zaidi ya mara 3. Na huwa ni wafuatiliaji wazuri kwa mteja ili uwape feedback

Shukrani mkuu kwa mchango wako. Picha zao kwakweli zinaonesha very nice condition!
 
Shukrani mkuu kwa mchango wako. Picha zao kwakweli zinaonesha very nice condition!
True. Hata kama gari limechubuka sehemu flani, hawana ile kupiga rangi kuficha hiyo kitu maana hii inaweza kuleta mashaka gari ikifika. Wana gari quality zote. Ni wewe tu kuchagua based on the amount you want to spend kwenye gari. Kitu kingine nimenotice: gari zao nyingine say ya 2001 unakuta inasoma 120,000km wakati company nyingine same year eti gari zinasoma 45,000km. Hapa unaweza kukuta speedmeter imechezewa

Harafu nadhani pia wana trusted agent(s) wao Bongo wanaoweza kusaidia kuclear hapo bandarini
 
Katika kununua mnayapenda haya makampuni kwasababu ndio yaliotangulia na kujitangaza ila yapo mengine sio maarufu kwa huku kwetu ila yana magari mazuri
Nilisha nunua SBT na BE-FORWARD na kwingine

Kwa hakika BEFORWARD is BEST.. FULL STOP
 
Katika kununua mnayapenda haya makampuni kwasababu ndio yaliotangulia na kujitangaza ila yapo mengine sio maarufu kwa huku kwetu ila yana magari mazuri
huko kwenu ni wapi mkuu ? na hayo mengine ni yapi ?
moja ya sifa za BEFORWARD ni picha zake ziko wazi vyakutosha pili wana wateja wengi sn gari halicherewi, tatu clearing charge hakuna longo longo kila kitu wazi wazi sio SBT inabidi kujadili na mtu mwingine tena baki mbaya wanakuletea wao bora km wangekuwa wanakujulisha wewe uchague mtu wako. Nne hakuna kabisa udokozi....
ni mengi na nina uzoefu sana na BEFORWARD mwisho utanidhania mm nawafanyia Promotion hapana kabisa mm ni mteja wao tu la mwisho wanazo discount point kwa wale wanaonunua magari mengi wanalijua faida yake.
 
True. Hata kama gari limechubuka sehemu flani, hawana ile kupiga rangi kuficha hiyo kitu maana hii inaweza kuleta mashaka gari ikifika. Wana gari quality zote. Ni wewe tu kuchagua based on the amount you want to spend kwenye gari. Kitu kingine nimenotice: gari zao nyingine say ya 2001 unakuta inasoma 120,000km wakati company nyingine same year eti gari zinasoma 45,000km. Hapa unaweza kukuta speedmeter imechezewa

Harafu nadhani pia wana trusted agent(s) wao Bongo wanaoweza kusaidia kuclear hapo bandarini

Mkuu Consultant , kwenye 'consignee' na 'notify party' panajazwa nani?
 
Mkuu, nami nimejaribu pia kucheki beforward. Nilichogundua.... naona kama beforward ni wawazi zaidi kuhusu ubovu/defects kwenye gari... yaani picha zao ni kila angle ya gari na sehemu zote zenye ubovu wanaonesha wazi. Hili sijaliona kwa SBT.

Gari nayohitaji beforward nimeikosa. Nimeipata SBT.
SBT Wako vizuri na bei zao ziko chin8 kidogo kuliko hao befoward,mimi niliagiza Rav 4 yenye engine ya 1ZZ toka sep 2016 gari bado inapiga mzigo vizuri,battery,tairi ni hizo hizo zilizikuja na gari,sijawahi badilisha chochote zaidi ya kufanya service na linapiga masafa sana tu
 
Wako vizuri na bei zao ziko chin8 kidogo kuliko hao befoward,mimi niliagiza Rav 4 yenye engine ya 1ZZ toka sep 2016 gari bado inapiga mzigo vizuri,battery,tairi ni hizo hizo zilizikuja na gari,sijawahi badilisha chochote zaidi ya kufanya service na linapiga masafa sana tu

Mkuu naomba unifahamishe, kwenye kuandaa documents za kupokelea gari kutoka nje, ni nini maana ya 'consignee' na 'notify party'?
 
Mkuu Consultant , kwenye 'consignee' na 'notify party' panajazwa nani?
Consignee: ni wewe mnunuzi ambaye mwisho wa siku card ya gari itaandikwa jina lako

Notify Party: ni mtu ambaye documents zitatumwa kwake. Mfano kama wewe mnunuzi upo mkoani na kuna mtu mwingine anakusaidia kupokea documents, then unajaza details zake. Otherwise ka utapokea docs mwenyewe, then Consignee na Notify party utajaza same details
 
Mkuu naomba unifahamishe, kwenye kuandaa documents za kupokelea gari kutoka nje, ni nini maana ya 'consignee' na 'notify party'?
Hiyo consignee name ni huyo mwenye gari,mfano kayanda ukawa unamwagizia gari kaka yako,notify ni wewe unayelishugulikia hilo gari so watakua wanakupa update
 
Documents Processing Center (cargo & freight company) ikiwekwa kama 'Consignee' pia ni 'Notify Party'.... ni sawa?
 
Back
Top Bottom