Ni mengi yatakimbia na kuonekana kama ndoto iliyootwa usiku na kusimuliwa na baadae kutoweka.Inaeleweka wazi na bila ya chenga zozote kuwa Mheshimiwa marehemu Raisi John Pombe Magufuli alikuwa kioo cha utawala bora Tanzania, kwa maana mema yake yalionekana na mabaya yake hayakujificha.
Kwa mtazamo huo yeyote yule atakaechaguliwa atasoma kutoka kwa marehemu na ataelewa Watanzania walipenda kitu gani na walichukizwa na jambo gani, vyombo vingi vya serikali vilikaa sawa kwa wananchi na vyombo hivyohivyo vilitumika kuikiza haki.
Wananchi wanaosemekana ni wanyonge walitumika kama ukuta mkubwa unaozuia kuona yaliyo ndani na ndio hivyo hivyo sifa zilipatikana nyingi kwani maovu yalikuwa machache na yanahesabika japo kuna yasiyofutika na yanayotia huzuni kwa wachache.
Kuna vyombo au viongozi wa Serikali waliokuwa wameficha makucha yao hili ni kundi lenye hasira sana ,maana wakati ule wakiogopa hukumu za papo kwa papo ,zinazotka kwenye mamlaka na sio mahakama.
Sasa tuelewe mazuri yote yalitokana na Raisi mwenyewe yeye kama yeye na ukichunguza mabaya yote yalitokana na Chama chake kwa ujumla wake na ujumla wao.
Rais alikuwa na roho nzuri sana lakini chama chake kimejaa walio na roho mbaya, Rais aliweza kuwadhibiti hawa katika mamlaka yake na kwenye zile njia zitakazompaisha kama ni mpenda maendeleo na mpenda kuona mwananchi wa chini hadhulumiwi anahakikisha anawasaidia hata kwa kutoa hela zake mfukoni, akiwajengea mazingira rafiki ya kufanya kazi, si bodaboda, si mamantilie si wamachinga na wengine wengi.
Hili ndilo lilompa uthubutu wa kupendwa huku uraiani, mambo makubwa ambayo yaliutia doa utawala wake yapo na yataendelea kuwepo. Rais aliepo madarakani anaweza kuyatumia hayo yakazidi kumpa respect kwa upande wake.