Kwaheri Dkt. Magufuli, karibu uonevu

Kwaheri Dkt. Magufuli, karibu uonevu

View attachment 1732341

Mambo ya John Pombe Joseph Magufuli yakitajwa yanawauma eeeee

Na mjue kabisa ameacha misingi imara...... Poleni kwa maumivu ya wivu na chuki
Hata ukiambiwa utaje alichofanya wewe mwenyewe huwezi, taja mambo 5 ambayo wewe yanakugusa moja kwa moja, ndege toka zimenunuliwa huwajawahi kupanda, flyover mimi mtu wa Usseri zinanisaidia nini? Ajira hakuna, vifaa vya ujenzi vinapanda kila siku
 
Tufanye kazi kwa bidii zote tuondokane na hili lindi la umaskini jaman...yaan mnaona bila yeye mambo yatabounce..why
My friend, tatizo kubwa ni kuingilika kwa mtu anayekuwa Rais. Mfano misamaha ya kodi, JPM alijitahidi na kuhakikisha haingilii TRA katika kukusanya kodi unlike JK alivyowapa uhuru wamiliki wa silent ocean.

Kuhusu umeme wa bwawa la Nyerere, kama hatarubunika kuingiza ufisadi, itakuwa jambo la kheri maana kama ufisadi utajumuishwa basi dhamira ya kupungua kwa bei ya unit ya umeme itayeyuka. SGR tunatumia hela za ndani na tunaamini hakuna ufisadi kiasi ikikamilika nauli na gharama za usafirishaji zitakuwa za chini. Ikiingizwa ufisadi, itakamilika lakini nauli na gharama za usafirishaji mizigo zitakuwa juu nayo kukosa maana kama ya Kenya.

Jiulize ni kwa nini Reli ya TRL ilishindwa kufufuka hata wakati wa JK; ni kwa vile wenye malori waliikalia juu ili mizigo wasipokonywe. Makampuni kama Lake Oil yakatamalaki. Sasa baada ya JPM; siamini Samia ataweza kuwakatalia wasihujumu hiyo reli ili waendelee kupeta ingawa wanaleta uharibifu wa barabara. Mabasi ya mikoani pia.

Samia anaweza iwapo atafumba macho kwa kukataa kutoa FADHILA kwa waliomsaidia kama JPM alivyo jitahidi kuwakwepa hata akina Kitwanga. CC mama D
 
Uonevu ndani ya Ccm labda ila sio kwa nchi yetu tunayoipenda Tanzania.
Mushaanza kujuta wanaCcm kwa sababu munajua fika chama kinarudi kwenye connection ya wazee wa chama.
Mkuu watu watakosa haki zao hata mahakamani, wenye nazo watakuwa juu sana. hili linanitisha sana. miradi,sijui kama itaenda kwa spidi tunayoijua
 
Kila siku tulikuwa tunahubiri kuwa show ya Mtu mmoja ni pata potea nguvu ya soda hamkutuelewa,kinachotakiwa ni mifumo imara ya taasisi. Sasa hivi mnaanza kulia kulia kana kwamba huyo mungu wenu angeishi milele
 
Kikwete amecha Udom, Mandela, daraja la Nyerere, Chuo cha mipango, chuo cha mwalimu Nyerere, Benjamini Mkapa Hosp, JKCI, ajira kibao, mishahara kupanda, barabara kibao, n.k lakini huwezi kusikia anasifiwa hata siku moja.
Vitu hivyo thamani ya hela zake ni mradi wa SGR basi. Mwamba ametoka huko.
 
Kila siku tulikuwa tunahubiri kuwa show ya Mtu mmoja ni pata potea nguvu ya soda hamkutuelewa,kinachotakiwa ni mifumo imara ya taasisi. Sasa hivi mnaanza kulia kulia kana kwamba huyo mungu wenu angeishi milele
Amini Mkuu umenena.
Magufuli alikua very individual alijikita katika kujenga nchi akasahau chama akakiacha kulekule alisahau kwamba atapita hata kama sio kifo mda wake ungeisha pia,saiv chama kinarudi kwenye asili yake na ndio kinachowaumiza wengi haswa wale waliopelekwa na Mzee na wale ambao hawana connection kwenye chama walikuepo kwa nguvu ya mtu mmoja.
 
Bi-Kidude-Biography.jpg

From Bi. Kidude
samia-suluhu-hassan.png

to Bi. Kidede
Tanzania inasonga mbele, Zanzibar fyatua Viongozi
 
View attachment 1732341

Mambo ya John Pombe Joseph Magufuli yakitajwa yanawauma eeeee

Na mjue kabisa ameacha misingi imara...... Poleni kwa maumivu ya wivu na chuki

Na bado watakapo kuja kujua kuwa JPM kilicho kufa na kuzikwa ni Mwili wake tu. Bali maono na utendaji wake unaishi katika nyoyo za Watanzania

Mrithi wake hataweza kukimbia ama kukitoroka kivuli cha JPM. Kitamuwinda kwa kila aendoko na kila atendalo.

Msiba wa JPM umeweka wazi kilichokuwa kinafichwa na kupigwa vita kuhusu kupendwa kwake zaidi na watu wa maisha ya hali za chini.

Ungeona body language ya wale wanausalama waliokuwa wakikaa pembezoni mwa jeneza lake kila liendako pale walipokatazwa kuandamana nalo likuzungusha Jamhuri stadium na mshehereshaji mwana mama jana.

Kutengeneza ama kubomoa Urais wa mrithi wake hakuko mbali. Kutaamliwa na nani atakuwa Naibu wa Rais na team ambayo itaundwa kufanyakazi na Mama.

Kumbuka viongozi wengi waliofanyakazi na JPM mpaka anakutwa na kifo, machoni pa Watanzania wengi wanaonekani ni Watu safi na wachapakazi. JPM hakupepesa macho wala kuchelewa kutumbua. Ni hapo sasa tutakapona sura za watubuliwa baadhi kwenye pengine Umakamu na Uwaziri.
 
Tafiti za kupendwa uraiani ulizifanyia wapi? Au kwa kuangalia umati na waliokuwa wanalia kwenye TV?
Ndugu hili kama ulikuwa unafuatilia malalamiko ya wananchi wenye shida ,humuhumu mitaani na tv zetu hizihizi za yuuchub ,kila mwenye shida kuonewa ulimsikia akisema ....kama baba Magufuli raisi wangu mpendwa unanisikia sikiliza hiki kilio chetu ,hapa mtaani huyu anatutesa,huyu ametuzika hela zetu na malalamiko ya aina hio ukisikia mrejesho unaona jambo limetatuliwa japo si na Raisi lakini mhusika alikwenda mbio kabla mkuu hajaingilia,kwa maana viongozi wa wananchi wakuu wa mikoa na wila na wahalmashauri walikuwa wapo karibu sana na wananchi kwa hofu lisije likavuja jambo akapokea simu ya kuwa huna kazi subiri utapangiwa kazi nyengine,wewe mkuu hapo tafuta mtu akamate kazi yake huyu hafai...Hilo Mheshimiwa magu aliliweza kwa kutumia ile sentensi ya mwalimu Nyerere usimuonee haya mtu.
 
Back
Top Bottom