Kwaheri Dkt. Magufuli, karibu uonevu

Kwaheri Dkt. Magufuli, karibu uonevu

As if hakuna mtu mwingine anayeweza kuongoza tena vizuri sana Mara elfu ya Jiwe , mataga ni empty set .
 
Kwako wewe ameleta...ujinga, upumbavu na ushenzi wa kusherehekea kifo Cha JPM...ujuha wa kutoona kuwa mtu huyu alikuwa anapendwa na Watanzania...ujuha wa kudhani kuwa JPM alikuwa anachukiwa na Watanzania..
Happy ulipo una hofu kubwa kabisa kuwa mnaweza mkafanyiwa revenge kwa kifo...wewe una hofu hiyo, Lissu Ana hofu hiyo...Lema ana hofu hiyo...wewe ukiwa ndani kwako ukisikia tu kelele za mjusi kwenye paa la nyumba yako unapatwa na hofu kuwa pengine unatafutwa kwa comments...kwenye mijadala mitaani unashindwa kuchangia mada kuhusu Magufuli kwa hofu kubwa...ila kwenye mitandao umejificha nyuma ya keyboard kuweka comments zako kiuoga...huwezi kutamka hadharani kuwa Magufuli alikuwa mbaya...utafanya hivyo tu kwa mkeo au mumeo ambaye huna naye...Yaani hivi Sasa mnaishi kwa hofu...kwenye daladala mnakuwa wanyonge kwani mkifanya fyofyoko mtafinyangwa Kama udongo na umma...maishi Bila raha...mmekosa amani...you are cowards...
Hata shetani anakuwaga na wafuasi wengi kwa hilo usiwe na shaka kumbuka alikuwa mkuu wa nchi ambayo ina watu kwa hiyo hilo lisikupe shida.
 
Ni mengi yatakimbia na kuonekana kama ndoto iliyootwa usiku na kusimuliwa na baadae kutoweka.Inaeleweka wazi na bila ya chenga zozote kuwa Mheshimiwa marehemu Raisi John Pombe Magufuli alikuwa kioo cha utawala bora Tanzania, kwa maana mema yake yalionekana na mabaya yake hayakujificha.

Kwa mtazamo huo yeyote yule atakaechaguliwa atasoma kutoka kwa marehemu na ataelewa Watanzania walipenda kitu gani na walichukizwa na jambo gani, vyombo vingi vya serikali vilikaa sawa kwa wananchi na vyombo hivyohivyo vilitumika kuikiza haki.

Wananchi wanaosemekana ni wanyonge walitumika kama ukuta mkubwa unaozuia kuona yaliyo ndani na ndio hivyo hivyo sifa zilipatikana nyingi kwani maovu yalikuwa machache na yanahesabika japo kuna yasiyofutika na yanayotia huzuni kwa wachache.

Kuna vyombo au viongozi wa Serikali waliokuwa wameficha makucha yao hili ni kundi lenye hasira sana ,maana wakati ule wakiogopa hukumu za papo kwa papo ,zinazotka kwenye mamlaka na sio mahakama.

Sasa tuelewe mazuri yote yalitokana na Raisi mwenyewe yeye kama yeye na ukichunguza mabaya yote yalitokana na Chama chake kwa ujumla wake na ujumla wao.

Rais alikuwa na roho nzuri sana lakini chama chake kimejaa walio na roho mbaya, Rais aliweza kuwadhibiti hawa katika mamlaka yake na kwenye zile njia zitakazompaisha kama ni mpenda maendeleo na mpenda kuona mwananchi wa chini hadhulumiwi anahakikisha anawasaidia hata kwa kutoa hela zake mfukoni, akiwajengea mazingira rafiki ya kufanya kazi, si bodaboda, si mamantilie si wamachinga na wengine wengi.

Hili ndilo lilompa uthubutu wa kupendwa huku uraiani, mambo makubwa ambayo yaliutia doa utawala wake yapo na yataendelea kuwepo. Rais aliepo madarakani anaweza kuyatumia hayo yakazidi kumpa respect kwa upande wake.
Kwaheri uonevu karibu mama Samia.
 
Kitika awamu ambayo watu wamenyanyasika ni hii ila kwa vile alipenda sana vyombo vyote vya habari vielezee mazuri tuu ndio maana mabaya hamyajui

Ningemuona fair sana kama angekuwa ameruhusu watu wawe wawazi kusema yote mazuri na mabaya pia, lakini kwa mfumo wake alivyo kuwa kauweka HAPANA hastahili sifa hizo.
 
Watu mnaona raha kuitww wanyonge?
Mdomo unaumba mtaendelea kuwa wanyonge maisha yenu yote
 
Back
Top Bottom