Kumbe na sisi humu ndani tunanunulika? Nimekudharau umekua bidhaa cheap!!Kwaheri Dkt. Mkamilo, tunaomba Rais Dr Samia utuletee Mkurugenzi mpya wa TARI
11/6/23 tulimuomba Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan atuletee Mkurugenzi Mpya wa TARI. Tunataka kusema ukiyaona ya Mussa utayaona ya Dr Mkamilo na watetezi wake. Kuna baadhi ya watumishi wake wachache sana ambao wanakubaliana na mfumo mbovu walijitokeza kumtetea. Baadhi wanasema kafanya mengi badala ya kusema kabomoa mengi mazuri na kuanzisha mabaya yasiyokubalika katika utumishi wa umma na Serikali ya awamu ya 6 haiyakubali. Huyu mzee ana madudu mengi sana ambayo wahusika wakiyafuatilia wao watapigwa na butwaa kabla yenu ninyi wananchi ambao mpo humu kwenye mahakama yetu ya wananchi. Ngoja leo nitolee maelezo mfano mdogo wa kuajiri watu wa familia yake ambao hawana sifa wala uwezo na kuwa watumishi wa Taasisi nyeti, muhimu na ya kisayansi kama TARI inayoongozwa na Dr Mkamilo.
Hebu wenye nia njema na Taifa na kutetea ajira kwa vijana wanaohotimu vyuo fuatilieni lengo la kuanzishwa kwa TARI. Hii TARI hii ni taasisi ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kufanya Utafiti kwenye masuala ya kilimo. Tunapozungumzia TARI ndio msingi wetu mkubwa kwenye kilimo. Watumishi wengi wa TARI ni wale ambao wamesoma sayansi ya kilimo na watu ambao wana akili nzuri isiyotiliwa shaka kwenye mambo ya kitafiti. Hali hii imekuwa tofauti kwa familia ya Dr Mkamilo.
Utaratibu wa Vyuo vya Ngazi ya Kati ya Elimu za Sayansi ya Kilimo, ni kwamba vyuo hivi huwa vinadahiri wanafunzi ambao wana ufaulu kwenye masomo ya sayansi kwa kidato cha nne au kidato cha sita.
Dr Mkamilo kama Mkurugenzi mkuu wa TARI alimuajiri mke wake ambaye ana ufaulu wa div 4 ya pointi 33 kwa masomo ya kidato cha nne. Huyu mke wake huyu ana ufaulu wa D mbili tu nazo ni kwenye masomo ya kiswahili (D) na historia (D). Masomo mengine ya civics (F), hesabu (F), biology (F), English (F), Geography (F), Literature (F) na mengine yote unayoyafahamu ni F. Kumbukumbu za ufaulu huu zipo TARI na zipo chuo Cha MATI Tumbi. Mnaohusika na ufuatiliaji haiitaji kwenda kwenye Taasisi hizi, mpigie Mkurugenzi Mkuu wa TARI na Mkuu wa Chuo Cha MATI Tumbi watume vyeti hivi mtacomfirm wenyewe. Sasa tunauliza iweje mtu huyu akawa muajiriwa ndani ya TARI? Je hicho chuo alichosoma stashahada ya kilimo kinazingatia ufaulu gani? Nauliza juu ya Chuo kwa sababu ili mwanafunzi kujiunga na masomo ya Kilimo Kwa elimu ya kati anahitaji kuwa na ufaulu wa chini ambao ni D physics, D Kemia, D biolojia, D hesabu au geography na D kiingereza (Hivi ni vigezo ambavyo vimewekwa na Wizara ya Kilimo na unaweza kutembelea website ya Wizara ili kujisomea vigezo hivi) lakini chuo cha MATI Tumbi hawakuzingatia vigezo hivyo. Huyu mama masomo muhimu yote yanayohitajika kuwa mtumishi wa TARI ana F lakini haikuwa na shida kwa mme wake kuchomeka jina la mke wake kwenye Taasisi yenye wasomi wakubwa ndani ya Taifa hili. Lakini vijana wenye weledi na ufaulu mzuri wanakosa ajira ila huyu mama anapata faster ajira ndani ya TARI Taasisi ya kisayansi ambayo lugha zake ni za kisayansi.
Nimefanya kazi na huyu mama TARI Makutupora tangu 2018. Sasa iko hivi watafiti wanapomuelekeza kufanya kazi kwa lugha ya kiingereza anashindwa kuelewa maelekezo ya kisayansi anayopewa, wakimpa sampuli za maabara anazimwaga kwa kutetemeka mikono kwa sababu hajawahi kutumia vifaa vya maabara, wakimwambia apange jaribio anasahau mapema hayo mambo mazito ya majaribio, wakimtuma kazi haelewi nao wanamuogopa ni nke wa boss wao. Taifa linapata hasara kubwa kupitia ajira za mchongo za namna hii. Nalo tunasubiri watu wa Dubai watuletee utaalam wao kwenye eneo hili ?
Halafu huyu mama sio kosa lake, kosa ni kwamba ufaulu na masomo yake hayamruhusu kufanya kwenye Taasisi ambazo sayansi zake zinahusu Biolojia, Kemia, Fizikia na hesabu ambayo hana msingi nayo. Kosa ni la Mkurugenzi Mkuu ambaye kwa makusudi alitumia akili yake vibaya na kuingiza mambo ya kifamilia kwenye Utumishi wa umma.
Huyu mama Mkamilo amekuwa technician kwa kipindi cha miaka 5 ndani ya TARI tena akiharibu majaribio na watafiti kumuogopa nke wa boss wao. Bado kwa nguvu za mme wake, huyu mama amepandishwa cheo kutoka kuwa Technician na kuwa mkufunzi mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha usambazaji Teknolojia za kilimo kiitwacho Agri Hub kilichopo jijini Dodoma eneo la Nzuguni. Hiki Kituo kinamilikiwa na TARI Makutupora.
Kama hujui ndugu yangu kilimo ni uti mgongo wa nchi yetu. Zaidi ya asilimia 70 ndio watanzania wanaojihusisha na kilimo. Na isitoshe kilimo kwenye nchi yetu ni sekta ambayo ina asilimia 26 kwenye GDP ya nchi. Hivi ni kwanini watu wanaichukulia nchi yetu kama shamba la bibi? Basi Dr Mkamilo asiiheshimu TARI basi awaheshimu watanzania ambao wanategemea kilimo katika nchi hii. Ni vijana wangapi wenye ufaulu mzuri kwenye masuala ya kilimo na hawana ajira kwa sababu ya watu wachache wenye ulafi kwenye madaraka?
Hali ilivyo sasa, wakulima nao wameanza kulalamika kwamba wakifika pale Nzuguni huyu mama anashindwa kuwaelezea vizuri wakamuelewa. Vijana wa BBT nao wamelalamikia hili. Yaaani wakulima wa sasa wana uelewa mkubwa sana na wengine wamehitimu vyuo na kujiajiri kwenye kilimo. Hawa wanahitaji watu wenye weledi na uwezo mkubwa kuwapa maelezo. Mkulima mwenye C ya biolojia na B ya agricultural science kwenye kidato cha 4 unahisi atamuelewa huyu mama? Rais Dr Samia amefanya kazi kwenye shirika la World Food Programme (WFP), siku mama anatembelea eneo hili kujua Teknolojia zinazotolewa na akaongozana na wageni wa kimataifa hali itakuwaje pale ?
Hii inatufanya kumuomba Rais wetu mpendwa Dr Samia atusaidie mzigo huu mzito. Tunaamini Rais ana malengo mazuri na nchi yetu hasa kwa Sekta ya Utafiti wa Kilimo lakini kuna watu wachache kama Dr Mkamilo ambao wanataka kumuangusha. Elimu ya Dr Mkamilo ni nzuri mno lakini anatumia elimu yake kwa ajili ya maslahi yake binafisi. Huyo ni mke wake ambaye ni muajiriwa ndani ya TARI lakini ni failure wa kidato cha nne.
Wakati mwingine watu hatuna shida binafisi na watu kama Dr Mkamilo lakini shida inatokea baada ya wao ubinafisi wao kuuingiza na kuuhusisha na masuala ya umma. Kuna kijana wake alifeli chuo kikuu cha SUA 2015 lakini kijani huyo alimuweka kusimamia mradi mkubwa wa Utafiti wa mihogo humo TARI🥹. Mradi huu ulishindwa kutoa matokeo. Huu uzi umeletwa kuonesha wale wanaomsifia Dr Mkamilo kwa maslahi yao binafisi kwamba wanakosea sana. Tulinde Taifa letu na tumsaidie Rais. Mkiendelea kumtetea teba tutaleta mengine mengi ambayo tunayafahamu. Tunaomba Mhe Rais ateue mtu mwingine mwenye kujali misingi imara ya Utafiti na kuheshimu sayansi ili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TARI. Huyu Dr Mkamilo apangiwe majukumu mengine ambayo anayaweza na mke wake atafutiwe eneo sahihi analoliweza na kuondolewa kwenye Taasisi ya kisayansi inayoheshimika kikanda na kimataifa ya TARI
TARI TARI TARI utafikiri ndo roho ya nchi. Ndo maana wabongo mnarogana kwa sababu ya vyeo. PUUMBAVU