Kwaheri Hans, Yanga tuache na vichaa wetu

Joined
Nov 13, 2015
Posts
34
Reaction score
37
Kwaheri Hans hii ndio Tanzania, Kichwa cha mwendawazimu, wamekuletea kocha bila kuvunja mkataba na wewe, ni dharau kubwa, ukienda kwenu ulaya kawaambie kwanini mpira wetu haukui, kocha aliyeaminiwa na taifa kama kocha mkuu leo amekubali kuwa kocha msaidizi wa Yanga,

Hans ukienda Ulaya kawaambie mpira tunaupenda kwa sababu tunaangalia sana wazungu lakini si kipaji chetu na ndio maana tulifungwa magoli 7 na waarabu, hawakutubahatisha bali ndio uwezo wetu, ukienda Ulaya kawaambie tunajua zaidi siasa na fitna za mpira kuliko kuucheza mpira wenyewe. Nitafurahi sana ukienda Azam ili uwaprove wrong management ya Yanga.

Kinachouma zaidi si wewe kuondoka bali njia iliyotumika kukuondoa. Wamekudharau sana kwa heshima uliyowajengea. Walichokufanyia Hans ni sawa na kuoa mke halafu amekuchoka na kuanza kukuingizia wanaume ndani halafu anakuambia ukalale sebuleni. Historia itawahukumu. Kabla hujaondoka subiri mechi tano za Yanga, kama mzambia akiharibu ataondoka yeye na Manji wake just wait n see.

Kila la Kheri Hans usisahau ule utafiti wa wizara ya afya wa kila watanzania 4 mmoja kichaa, Yanga tunafika watu milioni 10 wanachama na mashabiki sasa utafanya hesabu mwenyewe

========
UPDATE:

Kocha Hans van Pluijm leo October 25 2016 amewaaga rasmi wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini ambao alikuwa akiwafundisha kabla ya kujiuzulu.
 
Tatizo bongo hawajui mpira na timu zao simba, yanga ni timu za hovyo tu.
 
Huyu alikuwa kocha sahihi. Sasa formula zilizotumika kumfanya aondoke hatuzielewi labda viongozi watatuelezea.
 
Nasikia Azam wanamtaka kwa udi na uvumba, na tayari wameisha anza kuzungumza naye
kuna uwezekano mkubwa timu kutetereka ktk kipindi hiki cha mpito!
Pluijm alikuwa bado ni chaguo sahihi kwa Yanga kwa kipindi hiki cha matatizo
 
Hapa me sijaelewa taarifa zinasema kajihudhuru means yanga hawajamfukuza sivyo?
 
Tena yanga naifananishaga na Chama cha Bwana Yule!Nataka niihame Yanga.
 
Klabu za urithi hzi unadhani sitakuwa na lipi jipya, club inamilikiwa na akina akilimali, watu ambao sijui kama hata ukimpa penseli mkononi anaweza ishika, kama sio kugeuza ufutio chini ncha juu, eti ndio wasemaji wa mwisho wa club.

Nchi hii ni ya wenda wazimu ndio maana katika kila wanne mmoja ni zeeee
 
Nasikia Azam wanamtaka kwa udi na uvumba, na tayari wameisha anza kuzungumza naye
kuna uwezekano mkubwa timu kutetereka ktk kipindi hiki cha mpito!
Pluijm alikuwa bado ni chaguo sahihi kwa Yanga kwa kipindi hiki cha matatizo
Akienda azam maumivu kwa sisi wanayanga yataongezeka. Bora aifundishe star's.
Ee MUNGU pitishiambali huo mpango wa azam usifanikiwe'
 
Yanga mmezingua hapo kwa kweli.naimbea sahivi ibolonge kabisa
 
Kajiuzulu bhana ajafukuzwa na anaenda kua mkurugenz mkuu kamati ya ufundi yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…