Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Ni kawaida kwa kocha yeyote kulinda heshima yake baada ya mafanikio makubwa kwenye carrier ya kazi yake.
Kocha Nabi amelifanya hilo jambo kwa uweledi mkubwa sana akiwa na klabu ya yanga, kapata mafanikio kuliko kocha yeyote yule kwenye mpira wa Tanzania, kavaa medali ya caf confederetion cup, kavaa medali ya ligi kuu, kavaa medali ya FA cup, kavaa medali ya ngao ya hisani, ni mafanikio ya kiwango cha juu kabisa.
Kwa mantiki iyo ilikuwa ni ngumu sana kumbakisha kutokana na vilabu vingine vikubwa vyenye misuli ya kiuchumi kumwekea ofa nono ambayo ni ngumu kuikataa.
Kwa mantiki iyo tunamtakia kila la heri kutafuta changamoto mpya!
Pia napenda kuwajuza mashabiki na wanachama wa yanga kuwa watulivu kwa kuwa aliyemleta Nabi wasisahau bado yupo, Nabi uyu wakati analetwa alipondwa sana but waliomponda leo ndio wanafurahi kuondoka kwake kwamba amewapa ahueni! Kwangu mimi ahueni aiwezi kuwepo hata akija kocha mwingine.
Yanga hii mpaka inafika hapo ilipofika imejengwa na vitu vingi sana kuanzia menejimenti, mashabiki,wanachama, squad ya timu husika, umoja na mshikamano vimechangia pakubwa kuifanya kazi ya Nabi iwe rahisi sana!
Kwa maana hiyo kocha anaekuja ataanzia pale alipoishia Nabi na kuendelea kuuwasha moto kutokana na ubora wa kikosi kilichopo na maingizo machache yenye ubora yatayoingizwa msimu ujao!
Nabi kaacha msingi na jengo tiyali kinachofata ni kuezeka tu kwa kocha anayekuja aitokuwa kazi ngumu zaidi ya mbinu tu za kiufundi kwa kuwa kikosi kimekamilika kila idara,
Na uongozi ulishatambua kuondoka kwa Nabi mapema kabisa na walishaanza mchakato wa kumpata kocha mpya ata kabla ya kuitimishwa kwa mechi za ligi ivyo muda si mrefu kocha mpya atatangazwa rasmi!
Aluta continua mapambano yanaendelea!