Kwaheri Pele: Kumbukumbu Yangu ya Kombe la Dunia 1966

Kwaheri Pele: Kumbukumbu Yangu ya Kombe la Dunia 1966

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KWAHERI PELE: KUMBUKUMBU YANGU KOMBE LA DUNIA 1966

Kombe la Dunia mwaka wa 1966 nilikiuwa na miaka 14 kwa umri huu niliweza kutambua kuwa kulikuwa na mashindano makubwa Uingereza.

Hivi ndivyo nilivyokuja kumjua Pele.

Mwalimu Mkuu wa Kinondoni Primary School Mr. Reveta alikuwa akija darasani na kutusomea gazeti la Tanganyika Standard na kutupa matokea ya mechi za Kombe la Dunia na kututajia wachezaji mashuhuri.

Miaka hiyo hakuna televisheni wala internet.

Habari tulizokuwa tunapokea zilikuwa zimepitwa na muda sana.

Lakini hatukujali.

Gazeti la Shoot lilitosha kutupa habari zote za mpira duniani.

Mwalimu Reveta akituhadithia habari za Pele wa Brazil na Eusebio wa Ureno huku akisisitiza kuwa Eusebio ni Mmakonde kutoka Mozambique.

Mashindano ya mwaka wa 1966 yalikuwa mabaya sana kwa Pele na Brazil na sote tulisikitika.

Katika club yetu ya Everton Mtaa wa Narung'ombe kulikuwa na Vava na Garincha katika timu yetu.

Tukijipa majina ya wachezaji wa Brazil na wa nchi nyingine mashuhuri.

Tulikuwa na Mazola.
Mazola alikuwa mchezaji wa Italy.

Kulikuwa na Danny Blanchflower wa Uingereza, George Young, Distefano wa Italy.

Baadhi ya majina haya yaliua majina yetu ya asili.

Ukimuuliza Jamil Hizam utamaliza Kariakoo yote hutompata.

Lakini taja Denis Law.
Kila mtu anamfahamu.

Leo hivi ninavyoandika wengi wa hawa wametangulia mbele ya haki.

Lakini sura zao na sauti hazijanitoka naona kama jana tuko Mnazi Mmoja Tuwa Tugawe tunacheza mpira na wachache saba wamevuka miaka 15.

Jina la Pele tuliliogopa na kulistahi.

Katika timu zote za watoto Dar-es-Salaam nzima hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kujiita Pele.

Hii Everton ndiyo 1967 ikawa Saigon ambayo ipo hadi leo ingawa club haina timu ya mpira.

Pele siku zote alikuwa sehemu ya maisha yetu katika mpira.

Kitabu hicho hapo chini nilipata kukinunua Dar es Salaam Bookshop katika miaka ya 1970 na kulikuwa pia na tafsiri yake ya Kiswahili.

321506431_1467139200446043_4001599909343092079_n.jpg
 
Ahsante jongwe tunashukuru Kwa Maisha ya kheri mola kakujaaalia
Mtwa...
Alhamdulilah.

Leo asubuhi katika kunyoosha viungo nimepita nje ya nyumba waliyokuwa wakiishi rafiki zangu wawili na tukicheza mpira pamoja.

Mmoja keshatangulia mbali ya haki na mwingine yu hai lakini yuko kitandani karibu miaka 5.

Niliingiwa na simanzi sana.
Unapotazama nyuma kuna mengi...
 
Tumepishana miaka miwili na mzee mohamed Said
 
Asante sana kwa kutufunza mengi mungu akujaalie afya njema na uwe na mwisho mwema. amen
 
Back
Top Bottom