Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa , na kueleza madudu ya TTCL , Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu , lachane na biashara ya mawasiliano ya simu .

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani .

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani , tutafidiwa chochote au ndio vile tena ?

Tunaitakia kila la heri .
Pole mkuu, hiyo line fanya kuihifadhi tu na kuwa kumbu kumbu kuwa kuliwahi kuwa na line za TTCL
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa , na kueleza madudu ya TTCL , Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu , lachane na biashara ya mawasiliano ya simu .

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani .

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani , tutafidiwa chochote au ndio vile tena ?

Tunaitakia kila la heri .
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
 
T-Pesa biduuu
Gawio la serikali chifwile
Wafanyakazi karibuni kitaa
 
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa apigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa , na kueleza madudu ya TTCL , Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu , lachane na biashara ya mawasiliano ya simu .

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani .

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani , tutafidiwa chochote au ndio vile tena ?

Tunaitakia kila la heri .
Cha kuongezea, nchi hii inakwamishwa kwa kila Rais kuja na maamuzi yanayokinzana na aliyepita kana kwamba wanatoka vyama tofauti.

Magufuli (R.I.P) alipigania kuifufua TTCL, huyu wa sasa anakuja na maoni tofauti, tuelewe nini!?

Kingine, vipi kuhusu ATCL? Imepiganiwa sana kiasi cha kuletewa ndege mpya, je, ina ufanisi wowote mpaka sasa!? Au imekuwa ni kaburi la pesa za mlipa kodi!?
 
Hasara Bil 35 .
 
Shirika hili likinunuliwa na serikali kwa asilimia 100 kutoka Barthi Airtel.

Mwaka 2016 Waziri Kindamba akateuliwa kuwa CEO wake.

Leo hii nadhani ni afisa tawala mahala.

Aibu na fedheha sana.
 
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa anapigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
Jamaa mwenyewe ndio yule Waziri Kindamba!? Kuna taasisi yoyote ambayo aliwahi kuwa CEO akaiongoza vizuri kabla ya kukabidhiwa TTCL!? Au alikuwa anaongoza kwa maelekezo ya JPM!?
 
Mimi ni mtumiaji mkubwa wa TTCL na hii ni zengwe iliotengenezwa kwanzia JPM aage dunia, leo itakuwa hitimisho tu.
Kipindi cha Magu 2gb kwa 500 na 10gb kwa kitu kati ya 1000 mpaka 2000 nadhani usiku kucha! Shusha torrent za kufa raia. Hizo ni za usiku tu achilia zile za kawaida.

Kwa wanaotumia landline (simu za mezani) wanajua usumbufu walioupata kipindi hiki cha awamu ya sita. Nilikuwa nikihisi kuna kitu kinapikwa na kweli leo kimeiva!

Sekta ya mitandao ya simu kwa sasa inaendeshwa kibepari kwa tafsiri yaba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!!!
 
Alitokea Diamond Trust na kabla ya hapo alikuwa NBC kama meneja aneshughulikia na masuala ya wizi wa kughushi.

Amesoma ana CV ilotulia kwenye masuala ya biashara hivyo JPM akaona afaa kuwa hapo asimamie TTCL ambalo sasa lilikuwa lamilikiwa na Serikali 100%
 
Mimi ni mtumiaji mkubwa wa TTCL na hii ni zengwe iliotengenezwa kwanzia JPM aage dunia, leo itakuwa hitimisho tu.
Kipindi cha Magu 2gb kwa 500 na 10gb kwa kitu kati ya 1000 mpaka 2000 nadhani usiku kucha! Shusha torrent za kufa raia. Hizo ni za usiku tu achilia zile za kawaida.

Kwa wanaotumia landline (simu za mezani) wanajua usumbufu walioupata kipindi hiki cha awamu ya sita. Nilikuwa nikihisi kuna kitu kinapikwa na kweli leo kimeiva!

Sekta ya mitandao ya simu kwa sasa inaendeshwa kibepari kwa tafsiri yaba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!!!
Itakuwa ama Bharti Airtel wataka warudi au wamerudi kwa jina jingine au ameandaliwa mnunuzi mpya.

Suala ni kumiliki mali za nchi kama TTCL ambapo katika nchi zote duniani mashirika haya hutasikia yakimilikiwa na watu binafsi kama inavyotokea hapa kwetu Tanzania.

Yana mwisho yote haya.
 
Tulishafahamu hili tena limechelewa.

Wanaomiliki makampuni ya simu wanashirikiana na TCRA, wengine wanatetea hawa mbweha hadi bungeni kupandisha bei ya bando na wizi wa makampuni ya simu kwa wateja, wanafahamika wote.

Walizuia starlink kuleta huduma ya internet Tanzania, ndio hao hao wanahujumu TTCL.

TTCL tishio kwao sababu huduma ya internet ni nafuu zaidi ya hao wengine, wameona heri kuifuta.
 
Back
Top Bottom