Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Nafikiri approach ya Rais Samia italisaidia hili shirika. Hajasema life bali libakie kwenye business ya Mkonga na kusimamia makampuni mengine ya simu lakini wao waache biashara ya simu.

Lakini kabla ya hizi changes tunahitaji kama taifa tufanye research reviews kuona kwanini tunashindwa kuendesha haya mashirika. Kama hata ku manage national stadium tumeshindwa itafikia hata tukiyabinafsisha tutaibiwa tu!

Mama amesema hata bandari zikaribishwe sekta binafsi lakini ni vizuri ufanyike uchunguzi wa kutosha na huru. Wakwamishaji wengi ni hawa hawa wakubwa! Hata hizi proposals usikute ni ramani za hao wakubwa.

Tuliona reli ilikufa vipi na kulipuka makampuni ya usafirishaji! Tunajua nini kilitokea UDA! Tunajua hata viwanda vyetu maarufu vilivyochezewa michezo! Unfortunately tunacheza michezo ile ile ya vibaka wa Manzese! Ukiibiwa ukapiga kelele unapata wa kukusaidia wengi kumbe hao hao ni sehemu ya vibaka!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Cha kuongezea, nchi hii inakwamishwa kwa kila Rais kuja na maamuzi yanayokinzana na aliyepita kana kwamba wanatoka vyama tofauti.

Magufuli (R.I.P) alipigania kuifufua TTCL, huyu wa sasa anakuja na maoni tofauti, tuelewe nini!?

Kingine, vipi kuhusu ATCL? Imepiganiwa sana kiasi cha kuletewa ndege mpya, je, ina ufanisi wowote mpaka sasa!? Au imekuwa ni kaburi la pesa za mlipa kodi!?
Unampiganiaje mtu ambaye hajielewi?

TTCL wameshindwa sambaza vocha

TTCL minara yake inajizima

TTCL customer care mbovu

Hapo utamlaumu vipi?
 
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa apigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
Nafikiri kama sikosei Waziri KIndamba alikuwa anapambana kweli ila naona wanasiasa wetu kwa sasa hawana habari nalo kabsa
 
Nafikiri approach ya Rais Samia italisaidia hili shirika. Hajasema life bali libakie kwenye business ya Mkonga na kusimamia makampuni mengine ya simu lakini wao waache biashara ya simu.

Lakini kabla ya hizi changes tunahitaji kama taifa tufanye research reviews kuona kwanini tunashindwa kuendesha haya mashirika. Kama hata ku manage national stadium tumeshindwa itafikia hata tukiyabinafsisha tutaibiwa tu!

Mama amesema hata bandari zikaribishwe sekta binafsi lakini ni vizuri ufanyike uchunguzi wa kutosha na huru. Wakwamishaji wengi ni hawa hawa wakubwa! Hata hizi proposals usikute ni ramani za hao wakubwa.

Tuliona reli ilikufa vipi na kulipuka makampuni ya usafirishaji! Tunajua nini kilitokea UDA! Tunajua hata viwanda vyetu maarufu vilivyochezewa michezo! Unfortunately tunacheza michezo ile ile ya vibaka wa Manzese! Ukiibiwa ukapiga kelele unapata wa kukusaidia wengi kumbe hao hao ni sehemu ya vibaka!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Haya mashirika yanakufa sababu mishahara inalipwa na serikali,
Wafanyakazi wana uhakika wa maisha, hivyo hata wasipofanya kazi wana uhakika wa kila kitu.

Haya mashirika yalitakiwa yatengeneze faida, kupitia mapato yao ndo yajilipe mishahara kulingana na malipo ya serikali.

Mf ATCL ina marubani 147, kila rubani analipwa zaidi ya Milioni 3 kwa Mwezi, anagharamikiwa kusomeshwa kila miezi 6, ndege walizo nazo zinazopaa ni 6 pekee
Sasa jiulize kwa huo wingi wa watu utapata vp faida?
Je ATCL ingekuwa yajilipa kupitia pesa zake ingeajiri watu wote hao?
 
If
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa , na kueleza madudu ya TTCL , Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu , lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani , tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Ife tu Kenge hawa wameimaliza wenyewe. Vifurushi wamevifanyaje sijui mbuzi hawa
 
Tulishafahamu hili tena limechelewa.

Wanaomiliki makampuni ya simu wanashirikiana na TCRA, wengine wanatetea hawa mbweha hadi bungeni kupandisha bei ya bando na wizi wa makampuni ya simu kwa wateja, wanafahamika wote.

Walizuia starlink kuleta huduma ya internet Tanzania, ndio hao hao wanahujumu TTCL.

TTCL tishio kwao sababu huduma ya internet ni nafuu zaidi ya hao wengine, wameona heri kuifuta.
Hduma za ttcl nafuu kasem Nani?
 
Unampiganiaje mtu ambaye hajielewi?

TTCL wameshindwa sambaza vocha

TTCL minara yake inajizima

TTCL customer care mbovu

Hapo utamlaumu vipi?
Shida kubwa sana kwa mashirika ya umma watu wanaenda tu kazini bila malengo. Kuna siku nilikuwa nahitaji kununua kifaa cha internet (MI-FI) nikasema niwe kizalendo zaidi nikaingia duka la TTCL pale M/city nikakuta mdada anavutia kwelikweli namuuliza bei pamoja na ofa walizonazo za hivyo vifaa vyao, nikamwambia hebu nipatie nione kilivyo ananiambie kwan hukijui hapo zilizopo zimefungwa zote Mpka ununue ndo utakiona. Hebu fikiria mtu na pesa Yako unakumbana na mujibu hayo kweli nikaona nitoke zangu nikaenda kununua cha mtandao mwingine ila nilisikitika sana sio siri mujibu hata mtu ambae hajapita darasani anauza biashara yake pembezoni mwa barabara hawezi kukujibu.
 
Itakuwa ama Bharti Airtel wataka warudi au wamerudi kwa jina jingine au ameandaliwa mnunuzi mpya.

Suala ni kumiliki mali za nchi kama TTCL ambapo katika nchi zote duniani mashirika haya hutasikia yakimilikiwa na watu binafsi kama inavyotokea hapa kwetu Tanzania.

Ya mwisho yote haya.
Inasikitisha kwakweli hili ni kweli walikuwa na unau flani sasa unashindwa kuelewa hujuma hizi zote wakuu wanashindwa kung'amua au Udo kila mtu na urefu wa kamba yake inchi inafunguliwa?
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa , na kueleza madudu ya TTCL , Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu , lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani , tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Ufidiwe nini tena?
 
Unampiganiaje mtu ambaye hajielewi?

TTCL wameshindwa sambaza vocha

TTCL minara yake inajizima

TTCL customer care mbovu

Hapo utamlaumu vipi?
Kama raisi hatuwezi kumlaumu kwenye haya basi hatupaswi kumpongeza popote.

Wakati anaingia moja ya ahadi za ni kufumua mashirika haya na kuyafanya yawe na tija tukampongeza, akatengua Mkurugenzi akamteua mpya na kusema huyu yupo vizuri. Sasa hivi anakiri shirika halijiwezi tena, kwa nn tusimlaumu?
 
CAG alisema kuwa Watendaji waombe kazi

Rais kasema ni ushauri mzuri ila wanaweka watu wao kwa lengo la kupata taarifa za huko
 
Kuna sekta makampuni au mashirika ya serikali ni vigumu sana kufanya biashara na kushindana na makampuni binafsi bila kubebwa.
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
 
Back
Top Bottom