Ntakupa scenario moja..!!
Kwa makampuni binafsi ya simu, mhandisi wa kwenye minara anapewa gari, mafuta, laptop na toolbox. Kwa mfano, mhandisi huyu anaishi, Say, Temeke Dar na minara aliyogawiwa kuihudumia incase ina tatizo ipo Kuanzia Mbagala, kuelekea direction ya Ikwiriri na hadi Utete. Mtu huyu kama kuna tatizo kwenye backborne site yoyote, say Mwalusembe, ambayo kuzima kwake kunamaanisha Lindi, Mtwara na Tunduru mawasiliano yanakata. Akipewa taarifa hiyo hata usiku wa manane. anawasha gari safari kuelekea Mwalusembe na anaiwasha site inarudi kwenye utaratibu wake wa kawaida na watu wanaendelea kuwasiliana.
Tuje kwa TTCL..!! Huku ni hatari. Gari analo dereva, ambaye atamfuata Mhandisi anayejua minara pindi mnara fulani unapozima. Sasa zamani, makampuni ya simu yote, kutoa mawasiliano Dar na kuyafikisha nje ya Dar, wengi walikuwa wanakodi tower space kwa TTCL, ground space na transmision zao kwenye minara yao mbalimbali nchini. Sasa waza sehemu kama Mkuranga ambapo, let say airtel, wamekodi nilivyovitaja hapo juu kwa TTCL. Sasa mnara wa TTCL ukizima, kwa airtel wao, ina maanisha Lindi, Mtwara na Tunduru kunazima koteee..!!! Sasa kwenye mazingira kama hayo, atatafutwa dereva wa TTCL, awashe gari na kumfutana mhandisi aliko, halafu ndiyo waende eneo la tukio. Bila kusahau dereva naye lazima apate ruhusu toka kwa bosi wake (wa logistics). Bila hivyo hawashi gari.
Kumbuka wakati hayo yote yanafanyika, wateja wa Airtel hawawasiliani and hence REVENUE LOSS KWA AIRTEL. Kwa delays walizokuwa wanazisababisha, airtel towers zinakuwa chini kwa muda mrefu. Kwa sababu hii na nyinginezo;
1. Makampuni binafsi ya simu yakajijengea towers zake. Hence TTCL wakapoteza mapato makubwa sana ya kila mwezi toka kwenye kukodisha tower space, ground space na transmission.
2. Baada ya makampuni binafsi kujiondoa kwenye miundombinu ya TTCL, wao hawakubadirika, waliendelea na uzembe huo huo, kiasi kwamba walikosa wateja.
3. Hadi leo hii, market share ya TTCL ni less than 1.5%. Na si ajabu, kuna watu hata humu JF hawazijui hata codes za TTCL. Mfano, mtu akisema namba yangu ni 0784xxxxxx unajua ni airtel, au 0713yyyyyy unajua nitiGo etc
NB. KWA MAKAMPUNI BINAFSI, KUMPA MTU GARI LA KUZUNGUKA NALO MINARANI NA HUKU AKIWA ANAKAA NALO NYUMBANI LIKI NA FULL TANK, NI GHARAMA NDOGO KULIKO KUZIMA BACKBORNE SITE KWA LISAA LIMOJA.
KWA TTCL, GARI ANAKUWA NALO BOSI AU DEREVA. MHANDISI KUWA NA GARI NI ANASA