Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Mkongo wa Taifa wenyewe umesha washinda.....
Miaka sijui Saba bila matokeo ya kuonekana, naona wanapotezea tu serikali mapato kwa kuto kuunganishia wahitaji ili Serikali ikusanye kodi. Dar peke yake hawajaweza kuunganishia watu wanaohitaji hata nusu, lini wataweza kufika mikoani?
Usiongee usichojua, mkongo ndo sababu unaandika JF, ukipata hitilafu hutaweza kitu.
 
yule jamaa aliuza hisa akazipeleka SA awamu ile, then karudi kivingine kawanunua wale wawili kawaunganisha.. Yule wa monduli zile hisa zake pale Voda sijui zimekaaje naye.
Hawa wavetcong inafahamika nani mdosi pale.. Wale wadosi wa kino~ Moroco inafahamika kuanzia mpokea kodi wa ule mjengo na Big banana ni nani..

TTCL ilikwapuliwa na wale jamaa wa Kino Moroco then yule jamaa wa Chato akairudisha pamoja na zile hisa pale Moroco Kino, sasa wale jamaa waKino Morroco wanataka lidude lao hapo ndio TTCL inapofia kwa muuza supu pale kino.

Kuna Uzi humu unauliza, Hii nchi ni mali ya nani?
Maana yake TTCL inauzwa kwa Airtel tena
 
Solution sio kuitoa serikalini bali ni kuuza hisa ili management iwe inaidhinishwa kitaalamu na shareholders kuliko hivi sasa raisi anateua.

Miaka ya Magufuli wakati wa kupokea gawio binafsi nilisema serikali ina mzaha sana kwenye kuendesha biashara; taasisi aina ata net profit hilo gawio linatokea wapi.

Kipindi hiko kwenye financial statement yao shirika lilikuwa linatengeneza gross profit, tatizo ni admin expenses wanatumia sehemu kubwa sana ya mapato yao kwenye kulipa mishahara kushinda ata washindani wao na hapo ndio faida yote inapopotea. Jumlisha na haya mashirika ya serikali kweny overstating ya matumizi mengine ni jambo la kawaida through dodgy tenders.

Hilo shirika mtu yeyote makini akipewa kuliendesha kitu cha kwanza kitakachofanyika hapo ni downsizing of the workforce; inachukua sehemu kubwa ya mapato.

Kwa kifupi huko serikalini wanahitajika financial analysts, matatizo yao ni obvious ukisoma statements zao. Halafu ukiangalia na everyday operation ni wazi faida aiwezikani hapo miaka 800, ajabu shirika linalotengeneza hasara juzi tu limetoa millions in charity hivi unadhani kungekuwa na shareholders wangekubali; mkutano unaofuata mkurugenzi angekuwa voted out yeye na body nzima ya management.

Sidhani kama serikalini kuna watu wengi waliosoma finance kwenye nafasi za ushauri. Otherwise hayo mashirika yanaendeshwa ovyo sana to external observers; yote sio TTCL tu.

Hao wakurugenzi ukiwasikiliza tu unaona ata uelewa wao wa maswala ya biashara unapwaya, sasa wanashangaa kitu gani yanapotengeneza hasara wakati ni vitu obvious kulingana na uongozi wenyewe.
Mashirika mengi ya serikali yanafanya uzembe wa makusudi sababu serikali ndiyo inalipa mishahara.

Haya mashirika yameajiri watu wabovu ajira za kudumu.

Ukienda ttcl kuna wazee wengi sana wasio na msaada, hawa walitakiwa wastaafishwe kwa lazima.

Haya mashirika yana wafanyakazi wengi kuliko utendaji kazi wao

TTCL inajenga makao makuu Dodoma wakati haitengenezi kitu.

Airtel wameipa serikali gawio la Bilion 39, kwa hisa 49%

Ukija kwa atcl huko napo pamejaa ujinga mtupu

ATCL ina marubani 147 kwa ndege 6 zinazofanya kazi kwa sasa

Ina hosts zaidi ya 300 kwa ndege 6 zinazofanya kazi

Shirika lina wafanyakazi zaidi ya 600 kwa ndege 6 afu tutegemee kupata faida

TRC wanajiibia wenyewe, wanashindwa kuwa wabunifu.

Hawajawahi tangaza wala kutafuta tender ya kusogeza makontena
 
I like you MTAZAMO unafikiri very positive na huwa waleta productive thoughts as always.

Lakini analysts kama Ernst Young, PWC si wapo?

Serikali iamue kama wenzetu India ambao shirika la reli lamilikiwa na serikali lakini laongozwa na wizara ya reli kabisa no problem.

Baada ya hapo ndipo yaibuka makampuni ya reli ambayo hukodi njia za reli hivyo hulipia huduma hiyo ya kutumia reli.

Mwisho kuna kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia zote za reli yaani railway network.

Hivyo utaiona kwamba shirika la reli lipo chuini ya wizara lakini inasimia shughuli zaote za reli ila uendeshaji ni makampuni ya reli ambayo asilimia kubwa ni makampuni binafsi.

Hii kwanza yaleta ufanisi katika uzimamizi na pia yapanua soko la ajira kwani kampuni hizi zitaajiri watu wao wataofanya kazi katika reli hizo.

Pia kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia za reli nayo inakuwa na wale sub-contractors ambao wote wanapata ajira hivyo kupanua zaidi soko la ajira.

Huduma za reli tu Tanzania yaweza kuinua uchumi na sko la ajira maana watu wataarijiwa katika sehemu mbalimbali ukatishaji tiketi, usafi, huduma ndani ya garimoshi, udereva uongozaji na mengine lukuki.

Sasa hata kama kuna watu wahitaji kuendesha biashara ya mabasio waweza kufanya hivyo bila shida maana huduma ni usafiri ni huria na watu wana uchaguzi aina ipi ya usafiri watumie.

Air India CEO wake ni raia wa New Zealand na jana alitetea kwanini Air India yailipa Russoa kutumia anga lake ili kupunguza gharama za kuzunguruka mamaili kibao kutafuta viwanja vya ndege Ulaya.

Huyu CEO na Managing Director (Campbell Wilson) amesimamia mashirika ya ndege ya Singapore, Canada, Hong Kong na Japan hivyo ana uzoefu mkubwa.

Wenzetu India sasa hivi wapiga hatua kubwa sana kiuchumi na kwa kila sekta.

Eeeh Mola wetu, tusikie kilio chetu wana wa nchi ya Tanzania.
Nenda Fly emirates, Fly Dubai, Saudi Air, Riyadhi Air, Etihad CEO wote ni Wazungu na faida inaonekana.

Cha kwanza haya mashirika yasitoe ajira za kudumu, wajilipe mishahara kutokana na mapato yao, huwezi nambia Fastjet alikuwa analipa mishahara nje ya mapato au alikua na ajira za kudumu.
Ndege zake zilikuwa zinafanya kazi haswa, Ndege 3 zinazunguka Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Zimbabwe, South Afrika
 
Sasa huoni wapi twaonyesha ujinga wetu?

Weye una ndege 6, mfano wa marubani 147 wa nini?

Huo si ndo upigaji tunozungumzia?
Mwanzo waliulizwa Bungeni wana marubani wangapi
Wakasema wanao 107
Watanzania 106

Juzi wametangaza ajira za marubani 35
Ukiangalia hapo unaona kabisa hili shirika linaongozwa na wapumbavu ambao wanatakiwa wachinjwe bila huruma
 
Walipomteua Mkurugenzi mkuu kuwa Muhaya walitegemeaga nini?!

Alikuwa ni Bwana mmoja akiitwa "Kazaura" hivi sasa yuko "E.A.C" Arusha.

Wahaya na wachaga wasipewe madaraka! Ni jamii hatari sana!
 
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
Ntakupa scenario moja..!!
Kwa makampuni binafsi ya simu, mhandisi wa kwenye minara anapewa gari, mafuta, laptop na toolbox. Kwa mfano, mhandisi huyu anaishi, Say, Temeke Dar na minara aliyogawiwa kuihudumia incase ina tatizo ipo Kuanzia Mbagala, kuelekea direction ya Ikwiriri na hadi Utete. Mtu huyu kama kuna tatizo kwenye backborne site yoyote, say Mwalusembe, ambayo kuzima kwake kunamaanisha Lindi, Mtwara na Tunduru mawasiliano yanakata. Akipewa taarifa hiyo hata usiku wa manane. anawasha gari safari kuelekea Mwalusembe na anaiwasha site inarudi kwenye utaratibu wake wa kawaida na watu wanaendelea kuwasiliana.

Tuje kwa TTCL..!! Huku ni hatari. Gari analo dereva, ambaye atamfuata Mhandisi anayejua minara pindi mnara fulani unapozima. Sasa zamani, makampuni ya simu yote, kutoa mawasiliano Dar na kuyafikisha nje ya Dar, wengi walikuwa wanakodi tower space kwa TTCL, ground space na transmision zao kwenye minara yao mbalimbali nchini. Sasa waza sehemu kama Mkuranga ambapo, let say airtel, wamekodi nilivyovitaja hapo juu kwa TTCL. Sasa mnara wa TTCL ukizima, kwa airtel wao, ina maanisha Lindi, Mtwara na Tunduru kunazima koteee..!!! Sasa kwenye mazingira kama hayo, atatafutwa dereva wa TTCL, awashe gari na kumfutana mhandisi aliko, halafu ndiyo waende eneo la tukio. Bila kusahau dereva naye lazima apate ruhusu toka kwa bosi wake (wa logistics). Bila hivyo hawashi gari.

Kumbuka wakati hayo yote yanafanyika, wateja wa Airtel hawawasiliani and hence REVENUE LOSS KWA AIRTEL. Kwa delays walizokuwa wanazisababisha, airtel towers zinakuwa chini kwa muda mrefu. Kwa sababu hii na nyinginezo;

1. Makampuni binafsi ya simu yakajijengea towers zake. Hence TTCL wakapoteza mapato makubwa sana ya kila mwezi toka kwenye kukodisha tower space, ground space na transmission.

2. Baada ya makampuni binafsi kujiondoa kwenye miundombinu ya TTCL, wao hawakubadirika, waliendelea na uzembe huo huo, kiasi kwamba walikosa wateja.

3. Hadi leo hii, market share ya TTCL ni less than 1.5%. Na si ajabu, kuna watu hata humu JF hawazijui hata codes za TTCL. Mfano, mtu akisema namba yangu ni 0784xxxxxx unajua ni airtel, au 0713yyyyyy unajua nitiGo etc

NB. KWA MAKAMPUNI BINAFSI, KUMPA MTU GARI LA KUZUNGUKA NALO MINARANI NA HUKU AKIWA ANAKAA NALO NYUMBANI LIKI NA FULL TANK, NI GHARAMA NDOGO KULIKO KUZIMA BACKBORNE SITE KWA LISAA LIMOJA.

KWA TTCL, GARI ANAKUWA NALO BOSI AU DEREVA. MHANDISI KUWA NA GARI NI ANASA
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
raisi bado hajamjua tu mchawi wa TTCL?mbona anakaa nao mezani bado tu hashtuki.ttcl wanaonewa na kulaumiwa bure wakati mchawi anajulikana.tumwache mchawi azidi kuwaroga labda na wao wataanza kuroga.
 
Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
Ukiritimba tu maana jiwe aliwaaminisha kuwa wao ndiyo wezawa kama kwa ATCL
 
Cha kuongezea, nchi hii inakwamishwa kwa kila Rais kuja na maamuzi yanayokinzana na aliyepita kana kwamba wanatoka vyama tofauti.

Magufuli (R.I.P) alipigania kuifufua TTCL, huyu wa sasa anakuja na maoni tofauti, tuelewe nini!?

Kingine, vipi kuhusu ATCL? Imepiganiwa sana kiasi cha kuletewa ndege mpya, je, ina ufanisi wowote mpaka sasa!? Au imekuwa ni kaburi la pesa za mlipa kodi!?
Jiwe hajawahi kufanikiwa kwenye project zake
 
Yaani kwa sababu shirika limepata hasara unakwenda kuua shirika?- Samia anafikiria nini?

Hii dhambi ya kuua TTCL itamwandama Samia kama dhambi ya kuua NBC ilivyomuandama Mkapa

Yaani unataka nchi itegemee akina voda na Tigo?

Samia acha mama, hili unalotaka kugusa ni fupa tena fupa gumu mno
 
Mimi ni mtumiaji mkubwa wa TTCL na hii ni zengwe iliotengenezwa kwanzia JPM aage dunia, leo itakuwa hitimisho tu.
Kipindi cha Magu 2gb kwa 500 na 10gb kwa kitu kati ya 1000 mpaka 2000 nadhani usiku kucha! Shusha torrent za kufa raia. Hizo ni za usiku tu achilia zile za kawaida.

Kwa wanaotumia landline (simu za mezani) wanajua usumbufu walioupata kipindi hiki cha awamu ya sita. Nilikuwa nikihisi kuna kitu kinapikwa na kweli leo kimeiva!

Sekta ya mitandao ya simu kwa sasa inaendeshwa kibepari kwa tafsiri yaba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!!!
Yaani kuanzia juzi nakjaribu kununua bando la internet wanasema kunatatizo la kiufundi. Basi tena hivi nivyochati natumia bila kujiunga basi tena 5000 iishe tu nijue moja
 
Back
Top Bottom