Nafikiri approach ya Rais Samia italisaidia hili shirika. Hajasema life bali libakie kwenye business ya Mkonga na kusimamia makampuni mengine ya simu lakini wao waache biashara ya simu.
Lakini kabla ya hizi changes tunahitaji kama taifa tufanye research reviews kuona kwanini tunashindwa kuendesha haya mashirika. Kama hata ku manage national stadium tumeshindwa itafikia hata tukiyabinafsisha tutaibiwa tu!
Mama amesema hata bandari zikaribishwe sekta binafsi lakini ni vizuri ufanyike uchunguzi wa kutosha na huru. Wakwamishaji wengi ni hawa hawa wakubwa! Hata hizi proposals usikute ni ramani za hao wakubwa.
Tuliona reli ilikufa vipi na kulipuka makampuni ya usafirishaji! Tunajua nini kilitokea UDA! Tunajua hata viwanda vyetu maarufu viliv,yochezewa michezo! Unfortunately tunacheza michezo ile ile ya vibaka wa Manzese! Ukiibiwa ukapiga kelele unapata wa kukusaidia wengi kumbe hao hao ni sehemu ya vibaka!
Sent from my SM-A315F using
JamiiForums mobile app
I like you MTAZAMO unafikiri very positive na huwa waleta productive thoughts as always.
Lakini analysts kama Ernst Young, PWC si wapo?
Serikali iamue kama wenzetu India ambao shirika la reli lamilikiwa na serikali lakini laongozwa na wizara ya reli kabisa no problem.
Baada ya hapo ndipo yaibuka makampuni ya reli ambayo hukodi njia za reli hivyo hulipia huduma hiyo ya kutumia reli.
Mwisho kuna kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia zote za reli yaani railway network.
Hivyo utaiona kwamba shirika la reli lipo chuini ya wizara lakini inasimia shughuli zaote za reli ila uendeshaji ni makampuni ya reli ambayo asilimia kubwa ni makampuni binafsi.
Hii kwanza yaleta ufanisi katika uzimamizi na pia yapanua soko la ajira kwani kampuni hizi zitaajiri watu wao wataofanya kazi katika reli hizo.
Pia kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia za reli nayo inakuwa na wale sub-contractors ambao wote wanapata ajira hivyo kupanua zaidi soko la ajira.
Huduma za reli tu Tanzania yaweza kuinua uchumi na sko la ajira maana watu wataarijiwa katika sehemu mbalimbali ukatishaji tiketi, usafi, huduma ndani ya garimoshi, udereva uongozaji na mengine lukuki.
Sasa hata kama kuna watu wahitaji kuendesha biashara ya mabasio waweza kufanya hivyo bila shida maana huduma ni usafiri ni huria na watu wana uchaguzi aina ipi ya usafiri watumie.
Air India CEO wake ni raia wa New Zealand na jana alitetea kwanini Air India yailipa Russoa kutumia anga lake ili kupunguza gharama za kuzunguruka mamaili kibao kutafuta viwanja vya ndege Ulaya.
Huyu CEO na Managing Director (Campbell Wilson) amesimamia mashirika ya ndege ya Singapore, Canada, Hong Kong na Japan hivyo ana uzoefu mkubwa.
Wenzetu India sasa hivi wapiga hatua kubwa sana kiuchumi na kwa kila sekta.
Eeeh Mola wetu, tusikie kilio chetu wana wa nchi ya Tanzania.