Usiongee usichojua, mkongo ndo sababu unaandika JF, ukipata hitilafu hutaweza kitu.Mkongo wa Taifa wenyewe umesha washinda.....
Miaka sijui Saba bila matokeo ya kuonekana, naona wanapotezea tu serikali mapato kwa kuto kuunganishia wahitaji ili Serikali ikusanye kodi. Dar peke yake hawajaweza kuunganishia watu wanaohitaji hata nusu, lini wataweza kufika mikoani?
Maana yake TTCL inauzwa kwa Airtel tenayule jamaa aliuza hisa akazipeleka SA awamu ile, then karudi kivingine kawanunua wale wawili kawaunganisha.. Yule wa monduli zile hisa zake pale Voda sijui zimekaaje naye.
Hawa wavetcong inafahamika nani mdosi pale.. Wale wadosi wa kino~ Moroco inafahamika kuanzia mpokea kodi wa ule mjengo na Big banana ni nani..
TTCL ilikwapuliwa na wale jamaa wa Kino Moroco then yule jamaa wa Chato akairudisha pamoja na zile hisa pale Moroco Kino, sasa wale jamaa waKino Morroco wanataka lidude lao hapo ndio TTCL inapofia kwa muuza supu pale kino.
Kuna Uzi humu unauliza, Hii nchi ni mali ya nani?
Maana mizigo ingetolewa bandarini fasta kupitia reli wanaikuta MbeyaMimi nilisema Starlink haiwezi kupewa ruhusa Tz watu wakawa wanabisha, same reason hawafufui mfumo wa reli ambao ungesafirisha mizigo kwa gharama nafuu sababu mabosi ndo wamiliki wa malori.
Mashirika mengi ya serikali yanafanya uzembe wa makusudi sababu serikali ndiyo inalipa mishahara.Solution sio kuitoa serikalini bali ni kuuza hisa ili management iwe inaidhinishwa kitaalamu na shareholders kuliko hivi sasa raisi anateua.
Miaka ya Magufuli wakati wa kupokea gawio binafsi nilisema serikali ina mzaha sana kwenye kuendesha biashara; taasisi aina ata net profit hilo gawio linatokea wapi.
Kipindi hiko kwenye financial statement yao shirika lilikuwa linatengeneza gross profit, tatizo ni admin expenses wanatumia sehemu kubwa sana ya mapato yao kwenye kulipa mishahara kushinda ata washindani wao na hapo ndio faida yote inapopotea. Jumlisha na haya mashirika ya serikali kweny overstating ya matumizi mengine ni jambo la kawaida through dodgy tenders.
Hilo shirika mtu yeyote makini akipewa kuliendesha kitu cha kwanza kitakachofanyika hapo ni downsizing of the workforce; inachukua sehemu kubwa ya mapato.
Kwa kifupi huko serikalini wanahitajika financial analysts, matatizo yao ni obvious ukisoma statements zao. Halafu ukiangalia na everyday operation ni wazi faida aiwezikani hapo miaka 800, ajabu shirika linalotengeneza hasara juzi tu limetoa millions in charity hivi unadhani kungekuwa na shareholders wangekubali; mkutano unaofuata mkurugenzi angekuwa voted out yeye na body nzima ya management.
Sidhani kama serikalini kuna watu wengi waliosoma finance kwenye nafasi za ushauri. Otherwise hayo mashirika yanaendeshwa ovyo sana to external observers; yote sio TTCL tu.
Hao wakurugenzi ukiwasikiliza tu unaona ata uelewa wao wa maswala ya biashara unapwaya, sasa wanashangaa kitu gani yanapotengeneza hasara wakati ni vitu obvious kulingana na uongozi wenyewe.
Nenda Fly emirates, Fly Dubai, Saudi Air, Riyadhi Air, Etihad CEO wote ni Wazungu na faida inaonekana.I like you MTAZAMO unafikiri very positive na huwa waleta productive thoughts as always.
Lakini analysts kama Ernst Young, PWC si wapo?
Serikali iamue kama wenzetu India ambao shirika la reli lamilikiwa na serikali lakini laongozwa na wizara ya reli kabisa no problem.
Baada ya hapo ndipo yaibuka makampuni ya reli ambayo hukodi njia za reli hivyo hulipia huduma hiyo ya kutumia reli.
Mwisho kuna kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia zote za reli yaani railway network.
Hivyo utaiona kwamba shirika la reli lipo chuini ya wizara lakini inasimia shughuli zaote za reli ila uendeshaji ni makampuni ya reli ambayo asilimia kubwa ni makampuni binafsi.
Hii kwanza yaleta ufanisi katika uzimamizi na pia yapanua soko la ajira kwani kampuni hizi zitaajiri watu wao wataofanya kazi katika reli hizo.
Pia kampuni inoshughulika na matengenezo na uboreshaji wa njia za reli nayo inakuwa na wale sub-contractors ambao wote wanapata ajira hivyo kupanua zaidi soko la ajira.
Huduma za reli tu Tanzania yaweza kuinua uchumi na sko la ajira maana watu wataarijiwa katika sehemu mbalimbali ukatishaji tiketi, usafi, huduma ndani ya garimoshi, udereva uongozaji na mengine lukuki.
Sasa hata kama kuna watu wahitaji kuendesha biashara ya mabasio waweza kufanya hivyo bila shida maana huduma ni usafiri ni huria na watu wana uchaguzi aina ipi ya usafiri watumie.
Air India CEO wake ni raia wa New Zealand na jana alitetea kwanini Air India yailipa Russoa kutumia anga lake ili kupunguza gharama za kuzunguruka mamaili kibao kutafuta viwanja vya ndege Ulaya.
Huyu CEO na Managing Director (Campbell Wilson) amesimamia mashirika ya ndege ya Singapore, Canada, Hong Kong na Japan hivyo ana uzoefu mkubwa.
Wenzetu India sasa hivi wapiga hatua kubwa sana kiuchumi na kwa kila sekta.
Eeeh Mola wetu, tusikie kilio chetu wana wa nchi ya Tanzania.
Mwanzo waliulizwa Bungeni wana marubani wangapiSasa huoni wapi twaonyesha ujinga wetu?
Weye una ndege 6, mfano wa marubani 147 wa nini?
Huo si ndo upigaji tunozungumzia?
Zantel kafidiwa na nani?Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?
Tunaitakia kila la heri.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Zantel ni shirika la nani?Zantel kafidiwa na nani?
Ntakupa scenario moja..!!Nini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
raisi bado hajamjua tu mchawi wa TTCL?mbona anakaa nao mezani bado tu hashtuki.ttcl wanaonewa na kulaumiwa bure wakati mchawi anajulikana.tumwache mchawi azidi kuwaroga labda na wao wataanza kuroga.Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.
Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.
Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?
Tunaitakia kila la heri.
Wewe ni mbuzi tu tena asiye na mkiaNchi ya mambuzi hii
Labda utapeli wa tuma kwa namba hii utapungua maana matapeli walikuwa wanatumia line za TTCLPole mkuu, hiyo line fanya kuihifadhi tu na kuwa kumbu kumbu kuwa kuliwahi kuwa na line za TTCL
Ili mradi wasitufungie huduma za WEST UNIONNa posta nayo shida ipo
Ukiritimba tu maana jiwe aliwaaminisha kuwa wao ndiyo wezawa kama kwa ATCLNini hasa kinafanya TTCL isiendeshwe kwa faida kulinganisha na makampuni mengine ya simu!? Ni kukosa uongozi, kushindwa kufanya maamuzi ya kibiashara kwa wakati, wafanyakazi wasio na weledi au!?
Jiwe hajawahi kufanikiwa kwenye project zakeCha kuongezea, nchi hii inakwamishwa kwa kila Rais kuja na maamuzi yanayokinzana na aliyepita kana kwamba wanatoka vyama tofauti.
Magufuli (R.I.P) alipigania kuifufua TTCL, huyu wa sasa anakuja na maoni tofauti, tuelewe nini!?
Kingine, vipi kuhusu ATCL? Imepiganiwa sana kiasi cha kuletewa ndege mpya, je, ina ufanisi wowote mpaka sasa!? Au imekuwa ni kaburi la pesa za mlipa kodi!?
Nitafanya sherehe kama atatupiwa virago yule jeuri aliyewaambia watanzania wahame nchi yao kisa tozoKwa heri MWIGULU na Kadogosa
Yaani kuanzia juzi nakjaribu kununua bando la internet wanasema kunatatizo la kiufundi. Basi tena hivi nivyochati natumia bila kujiunga basi tena 5000 iishe tu nijue mojaMimi ni mtumiaji mkubwa wa TTCL na hii ni zengwe iliotengenezwa kwanzia JPM aage dunia, leo itakuwa hitimisho tu.
Kipindi cha Magu 2gb kwa 500 na 10gb kwa kitu kati ya 1000 mpaka 2000 nadhani usiku kucha! Shusha torrent za kufa raia. Hizo ni za usiku tu achilia zile za kawaida.
Kwa wanaotumia landline (simu za mezani) wanajua usumbufu walioupata kipindi hiki cha awamu ya sita. Nilikuwa nikihisi kuna kitu kinapikwa na kweli leo kimeiva!
Sekta ya mitandao ya simu kwa sasa inaendeshwa kibepari kwa tafsiri yaba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!!!