Zanzibar 2020 Kwaheri ya kuonana CCM

Zanzibar 2020 Kwaheri ya kuonana CCM

Zanzibar ya upinzani hoja kadhaa eti...
Skuli zote zitakua za ghotofa
Nitafuta madeni yote...
Dah, babu kachoka kwa kweli maana hapa hata mtoto wa darasa la pili B humdanganyi..
Za chama tawala je?

Miaka 50+ ya CCM bado watu wanalalmika umeme, Elimu, Hospital na madawa, Maji, na mengine mengi.

Una habari kama kina kipande Tunguu ambacho hakizidi kilomita moja na ni njia ambayo rais anatumia kwenda kwake kila Ijumaa na kurudi mjini jumatatu kina miaka 10+ hakijatiwa lami? Na hio ndio njia kuu ya kwenda kusini.

CCM wana hoja gani kwamba wazanzibari watawaunga mkono? usidanganywe na zile Altezza zinazoekewa mafuta ukaona vijana wanamuunga mkono Mtalii. mafuta yanatumika kwenye drifting 😀
 
Zanzibar hatutoboi ....na tukitoboa basi basi itakuwa si salama tena. Kule CCM nzito haibebeki kabisa.

Baada ya kukosa watu ikabidi tupige campaign za mtaa kwa mtaa.
Sijawahi kuona Mwinyi akihutubia mikutano ya nje kilikoni

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kuona Mwinyi akihutubia mikutano ya nje kilikoni

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Yupo na anahutubia kwa muda mfupi sana na akimaliza tu huondoka watu wote akabakia yeye na baba yake na viti na kuna wanawake wawili watatu,juzi na ndivyo inavyotokea ,inawezekana ni itifaki yao,ila nijuavyo mgombea wa kiti cha Uraisi hupewa nafasi ya mwanzo kuondoka na baadae hufuata wengine.

Juzi nilitamani kutoka machozi alibakia yeye na baba yake na viti vitupu watu wote wa CCM wameondoka ,ulikuwa mkutano wa Bumbwini.
uangalie huo mkutano.
 
Mbona hawarushi live popote si youtube wala tv?

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Salaam kutoka Zenji ,kuna uhakika kutoka kila pembe kuwa sasa ni rasmi CCM imeshazikwa Zanzibar,hilo halina mjadala ,jukwaa la CCM Zanzibar CCM huchawanyika na kumuwacha/chia baba na mwana kwenye jukwaa.
Huyu baba ameenda kufanya nini mbona anamharibia mwanawe ? Husein unahisi ana ukakasi fulani ,huwezi kurapu ukaeleweka kama mzee wako yupo pembeni.

Ukweli ni kuwa CCM haipo imeshafutika kwa wananchi ambao ndio wapiga kura,kila lifanywalo na kupangwa na kina Bashiru kutoka Tanganyika huwekwa uwanjani,mipango na mbinu zote zinajulikana na wananchi sasa kama wananchi au tuseme WaZanzibari walio wengi wanajipanga kupambana na hila hizo ovu,

CCM ijue Zanzibar watu wao wanauelewa wa uraia wao na hawababaiki na mambo ya siasa wanaangalia zaidi muelekeo wa Nchi yao na hatari inayoikabili ,kusema kweli CCM wamevuruga kumuweka Husein Mwinyi,wangeweka nokoa yeyote yule Mzanzibari kuliko kumuweka mtu ambae hata mitaa ya Zanizibar haielewi,na kusema kweli wamempa wakati mgumu sana Husein Mwinyi ,sasa hajui achague nini kati ya dini na dunia.

Mipango ya Bashiru au tuseme CCM yote ipo njenje na inaeleweka tena inaeleweka hatua kwa hatua,kuna ulazima gani kulazimisha ushindi ? Kwamba ni lazima CCM ishinde,wakati haikushinda chaguzi zilizopita ambapo kulikuwa na wagombea waZanzibar atakuja kushinda huyu ambae CCM wenyewe wametifuana ndani wenyewe kwa wenyewe na hawajakaa sawa hadi leo.

CCM acheni mbinu chafu mtaumbuka na mpira utakuja kuwaangukia watumika.
Ulivyomaliza kuanadika ukajiridhisa kuwa ulichoandika ni sahihi kisha unaenda kupumzika na kudhani umetoa wazo madhubuti?
Sasa endelea kulala usingizi siku ukiamka utajua kuwa wazenji hawaihitaji usultani wa matapeli.
 
Zanzibar ya upinzani hoja kadhaa eti...
Skuli zote zitakua za ghotofa
Nitafuta madeni yote...
Dah, babu kachoka kwa kweli maana hapa hata mtoto wa darasa la pili B humdanganyi..
Kila mvuvi atapata boat yenye radio call na televisheni, ahadi zingine bwana. Maalim apumzike kwakweli amechoka na hana jipya. Sera yake ya kuvunja muungano imebuna na itapewa jibu mujarabu Tar 28 na Wananchi
 
Tatizo umetawaliwa na ujinga na CCM wakipata watu kama nyinyi hufurahi sana, Kwa taarifa yako kuna nchi kama boti yako ya uvuvi haina redio call huruhusiwi kuivamia bahari,leo mnajengewa pedestrian bridge mnatangaza dunia nzima na Raisi ndio anaenda kufungua dalaja.

na hilo alilolisema ni jambo la zamani ,ila huku bado tupo mbali sana ndio hivyo njia za madaraja gumzo la nchi nzima ,CCM mwisho wa kudumaza wananchi unakaribia,yaani watanzania wa miaka ya siku hizi wote wafupi,tumedumaa kiakili mpaka kuzaliwa.
 
sasa maalim anahangaika na nini kama mnalijua hilo
Anahangaika na kuepusha shari ,wananchi hawatokubali upumbavu huo wa CCM ,ushenzi huo wafanyiane CCM hukohuko kwenye kamati zao wanapoteuana na kuteuliwa na wajumbe.
Anaehangaika ni yule anaetaka kuficha na kila anapoficha anakurupushwa ,sasa hivi masanduku hayo yakipita watu wanayazomea,maana yanapotolewa,yanapohamishwa habari zinaenea wakati huo huo. Ni aibu ,sasa hivi washaanza kutupiana kila mmoja anaogopa kuwa dhamana,unajua mambo yakiwa leak,kila unavyopanga leakage inatokea .wikiliki ,CCM zanzibar imeshavurugika hakuna siri nani atakamatwa na mkia ndio mwizi.
 
Huko Visiwani CCM imebaki kwenye maandishi ya khanga kofia na tisheti ila kwenye mioyo ya Wazanzi imetoweka kabisa
 
Zanzibar hatutoboi ....na tukitoboa basi basi itakuwa si salama tena. Kule CCM nzito haibebeki kabisa.

Baada ya kukosa watu ikabidi tupige campaign za mtaa kwa mtaa.
Nimeshangaa kuona mgombea wa urais Zanzibar tena CCM kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba
 
Hii ya wafanyakazi wa Zanzibar kupiga kura tarehe 27.10.2020 badala ya 28.10.2020 inatakiwa iangaliwe upya japo iko kwenye utaratibu wa ZEC.

Kaisome tena nadhani hujaielewa. Sio kupiga tarehe 27 pekee bali anatakiwa lupiga tarehe 27 kwa ajili ya zanzibar na kurudi kupiga tena tarehe 28 kwa ajili ya muungano
 
Mwaka huu hata wabara tumeamka kuhusu Zanzibar na tunaiomba sana CCM isivipake vyombo vyetu vya ulinzi na usalama damu nyingine isiyo na hatia kwa jina la kuulinda muungano na KUMUENZI BABA WA TAIFA!
NB: MUACHENI BABA WA TAIFA APUMZIKE KWA AMANI MAANA HATA WA KUBEBA VIATU VYAKE SIMUONI!
😅
👊 ✌️✌️✌️💥
 
..sijui kwanini ccm walichagua mgombea goigoi asiye na mvuto kama Hussein Mwinyi.

..CCM-Znz walitakiwa wamsimamishe Prof.Makame Mbarawa ndiye angeweza kuchangamsha kampeni na kuvutia wapiga kura.
 
Back
Top Bottom