Leo nimekuja kuwaaga hapa rasmi kwa sababu hiki ndicho kijiwe changu humu JF.
Likizo yangu imeisha. Natoweka JF kuanzia kesho mpaka mwaka 2020, ndipo tutakapokutana rasmi. Naenda kukabiliana na majukumu kadhaa mazito, likiwemo la kujiandaa kugombea Urais wa JMT mwaka 2020. Huo mwaka, nitaingia rasmi kwa kishindo katika siasa za Tanzania, nikiwa na lengo la kuunyakua Urais ifikapo mwaka 2025.
Nimeamua kuandika ili kupunguza maswali yatakayojitokeza kutokana na mimi kutokuwepo humu kwa muda mrefu, pia kuzima uzushi wa aina yoyote, kama mjuavyo, jf kuna kila aina ya uzushi, maana wapo wanaoweza kuzusha kuwa simo humu kwa sababu zisizo za kweli.
Simplicity.