Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nieleweshe dini ni niniWewe hata dini huelewi ni nini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nieleweshe dini ni niniWewe hata dini huelewi ni nini.
Fungulia uzi jukwaa la dini.Nieleweshe dini ni nini
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَNaamini kabisa wanaozifanya hizi dini zionekane mara ushoga mara ugaidi ni viongozi wa dini kupotosha baadhi ya maneno labda kwa manufaa yao...nakumbuka siku moja nilipanda gari ya ya mizigo kutoka dodoma naelekea mtwara baada ya muda wale jamaa ambao ni dereva na utingo wake ambao ni warangi wakaweka mahubiri ya roggo yale yanayodai wakristo wauawe popote pale na huku anadai vijana wa kenya waislamu waende Somalia kupigana jihadi kiukweli nilibishana nao sana wao wakawa wanadai wasio waislamu inabidi wauawe bila huruma,,,nikajua viongozi wa dini baadhi wanapotosha hizi imani
Utamaduni unaweza kubadilishwa.Nadhan kila timu Ina tamaduni na mapokeo yake, mazembe wao huanzia kanisani kwa Ibada ya Misa na msimu ukiisha huwaga wanarud kushukuru bila kujali matokeo, kwa hapa kwetu simba na yanga wamekua na utamaduni wa kufanya dua ya kiislamu kitu ambacho si dhambi, kwa mtu anaejua historia ya vilabu hivi, kule Argentina timu ya taifa inajiita "timu ya papa" na hakuna shida yoyote, basi kwa vile sote ni ndugu na Mungu wetu ni mmoja, hakuna haja ya kulumbana, kikubwa dua/Sala/maombi yamefanyika, sote tuseme "Amina" "Bwana asikie maombi yetu"
Na ndivyo ilivyo ni ukweli mtupu mkuu.Kama Membe vile aliyesema hata msaada ukitoka kwa shetani tutaupokea tu kwa sababu sisi ni masikini 🤣
Yanga forever 💛💚[emoji23][emoji23][emoji23]
Nakubali Half american mtu wa nguvu
Umeleta dini kwenye uzi wa michezo, umetia aibu sana!Fungulia uzi jukwaa la dini.
yap, wangeita mchungaji hapo akataja Jina la Yesu, wangeruka mapepo hao na majini yangegoma kufanya kazi.Dini zingine hazipo compatible na majini
Umeona kichwa cha habari na habari za huu uzi au umekurupuka tu?Umeleta dini kwenye uzi wa michezo, umetia aibu sana!
Hukusoma angalizo kwenye uzi?Umeona kichwa cha habari na habari za huu uzi au umekurupuka tu?
Kama ni hivyo mpeni Mristo achinje ili awakilishe dini zingineLengo ni Dua
Dua ya dini moja imewakilisha zote ukitaka kila mwenye dini yake yafanyike maombi si patakeshwa Mkuu
Nimeusoma uzi wote. Ndiyo maana nikaweka sawa kuwa dini ni moja tu, Uislam. Zingine zote ni biashara.Hukusoma angalizo kwenye uzi?
uislamu kwa tafsiri ya unyenyekevu hata mimi pia ni muislamuWaislam
Ni sura gani umeinukuu?الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ
Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a´mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.
Waliopewa kitabu ni wakiristo na wayahudi,ikiwa vyakula vyao na wanawake wao wema ni halali,Hilo la kuwaua linatoka wapi!?
Sasa inatakiwa uamini Mwenyezi mungu mmoja tu unaemnyenyekea.uislamu kwa tafsiri ya unyenyekevu hata mimi pia ni muislamu
Hata biblia inaeleza hivyo kuwa Mungu ni mmojaSasa inatakiwa uamini Mwenyezi mungu mmoja tu unaemnyenyekea.
Uamini na Mitume ya Mwenyezi Mungu.Hata biblia inaeleza hivyo kuwa Mungu ni mmoja
Utamuaminije Mungu bila kuwaamini na aliowatuma?Uamini na Mitume ya Mwenyezi Mungu.
Hiyo ni Suratul Maida aya ya tano. Qur'an 5:5.Ni sura gani umeinukuu?