Kwahiyo Dua za Yanga ni za upande mmoja tu, Waluteri na Wakatoliki au hata Mwamposa hawamo?

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَنْ يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ
Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a´mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.

Waliopewa kitabu ni wakiristo na wayahudi,ikiwa vyakula vyao na wanawake wao wema ni halali,Hilo la kuwaua linatoka wapi!?
 
Nadhan kila timu Ina tamaduni na mapokeo yake, mazembe wao huanzia kanisani kwa Ibada ya Misa na msimu ukiisha huwaga wanarud kushukuru bila kujali matokeo, kwa hapa kwetu simba na yanga wamekua na utamaduni wa kufanya dua ya kiislamu kitu ambacho si dhambi, kwa mtu anaejua historia ya vilabu hivi, kule Argentina timu ya taifa inajiita "timu ya papa" na hakuna shida yoyote, basi kwa vile sote ni ndugu na Mungu wetu ni mmoja, hakuna haja ya kulumbana, kikubwa dua/Sala/maombi yamefanyika, sote tuseme "Amina" "Bwana asikie maombi yetu"
 
Utamaduni unaweza kubadilishwa.
 
Ni sura gani umeinukuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…