Kwahiyo Mbeya na Songwe utaratibu ni kupaki barabarani kupeana zamu ya kupita?

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Pale Inyala unapoteza dakika 30 wanasema mnasubiria malori yanapita muda wake tofauti na magari mengine.

Pale mteremko wa Mbalizi ni hivyohivyo halafu tena ukiingia mkoa wa Songwe kuna sehemu utaratibu ni huo.

Chakushangaza barabara ni nzima kabisa ila wameweka huo utaratibu kwasababu kuna ajali ziliwahi kutokea.

Nimechukia kupoteza muda njiani.
 
Afrika hatuna akili za kutatua changamoto zetu. Unaweza kukuta hapo ufumbuzi ni kidogo sana ila hiyo akili hadi tusubiri mtaalamu wa kichina au kizungu aje kuturekebishia.

Hapo utakuta wahusika wamekaa vikao vingi sana vyakulipana posho kuja na huo ufumbuzi ambao kimsingi hauwezi kua ufumbuzi wa kudumu.
 
Barbara ni nzimaa? Daah mkuu umeshindwa hataa kujuaa kwamba maeneo hayo yana miteremko mikali na Malory y'ako mengi? Tumia simu y'ako vizur utaijua sababu mkuu.
Hujaona kwamba nimeandika wanasema ni ajali zilitokea?
 
Afrika hatuna akili za kutatua changamoto zetu. Unaweza kukuta hapo ufumbuzi ni kidogo sana ila hiyo akili hadi tusubiri mtaalamu wa kichina au kizungu aje kuturekebishia.

Hapo utakuta wahusika wamekaa vikao vingi sana vyakulipana posho kuja na huo ufumbuzi ambao kimsingi hauwezi kua ufumbuzi wa kudumu.
Mkuu umenena vema,barabara zetu hazina vipimo vinavyotakiwa, hizi pass zote including kitonga pass,mzungu angepasua line nyingine, zinazoshuka Zina line yake na kupanda pia,na hizi pass ni muhimu mno tujenge Arrester ili brake zikifeli driver aelekezee huko, mbona wenzetu wanazo?,down za kwenda chirundu border (Zambia/Zimbabwe),kuna Arrester mbili kwenye ile pass upande wa zambia, na zinasaidia mno
 
Afrika hatuna akili za kutatua changamoto zetu. Unaweza kukuta hapo ufumbuzi ni kidogo sana ila hiyo akili hadi tusubiri mtaalamu wa kichina au kizungu aje kuturekebishia.

Hapo utakuta wahusika wamekaa vikao vingi sana vyakulipana posho kuja na huo ufumbuzi ambao kimsingi hauwezi kua ufumbuzi wa kudumu.
Tena yale malori wakiyaruhusu yapite halafu zifuate gari ndogo inakuwa tabu tupu kuyapita tena maana yanakuwa yamepangana. Yanaisha masaa mawili.

Hawa viongozi akili zao ni chache sana.
 
Ungekua unaijua hiyo bara bara usingeandika ulichoandika watu wanataka upite kwa usalama wewe unaona dk 30 ni muhimu kuliko Afya yako madereva wa mjini bhana mna vituko sana...
Mbeya niliwahi kukaa zaidi ya miaka 10 na huo upuuzi haukuwepo. Kwanini wasijenge barabara ya kupanda iwe tofauti na kushuka na ziwe mbilimbili?
 
Hela imetoka sasa hivi Mkuu hayo maeneo yana ajali za ajabu mno ndio maana wanafanya hivyo wacha tusubiri tuu maana usalama kwanza wakijenga hizo mambo zitakua hazipo...
 
Inyala kuna njia mbadala ilikuwa inajengwa upande wa kushoto kama unaelekea Mbeya, pengine haijakuwa tayari...(short term plan)

Kuna plan ya kupanua hiyo barabara tokea Igawa hadi Tunduma (long term plan)
 
Njia mbadala waliyoijenga ni kituko cha mwaka maana haisaidii lolote, eneo lenye mlima bado lipo na njia moja halafu huku juu ndio zipo mbili ambazo tena zimeungana baada ya mita chache.

Yaani aliyefanya ule upuuzi anapaswa kunyongwa.
 
Pale Inyala unapoteza dakika 30 wanasema mnasubiria malori yanapita muda wake tofauti na magari mengine.

Pale mteremko wa Mbalizi ni hivyohivyo halafu tena ukiingia mkoa wa Songwe kuna sehemu utaratibu ni huo.

Chakushangaza barabara ni nzima kabisa ila wameweka huo utaratibu kwasababu kuna ajali ziliwahi kutokea.

Nimechukia kupoteza muda njiani.
Duuh yani unalalamika badala ya kupongeza!!!
 
Back
Top Bottom