Kwahiyo Mbeya na Songwe utaratibu ni kupaki barabarani kupeana zamu ya kupita?

Kwahiyo Mbeya na Songwe utaratibu ni kupaki barabarani kupeana zamu ya kupita?

Inyala pasikieni tu ila lile eneo ni hatari. Mwaka 2019 nimepoteza jamaa yangu pale kwa ajali gari ilifeli brake bomba la mafuta ikaenda kuchegama kwenye kingo za bomba la mafuta. Jamaa ndio ivyo alikufa akiwa bado kijana.

Pamechukua uhai wa watu wengi sana.
 
Hiyo iwe hatua ya muda mfupi sana. Serikali inatakiwa itengeneze hilo eneo. Fedha wanazo lakini hawajali. Kazi kusafiri kwenye business class na kukaa hotel kubwa kubwa. Na kuendesha magari ya kifahari.
Mkuu ipo plan ya kupanua hii barabara kutoka Igawa mpaka Tunduma njia nne. Ila hiyo ni plan ya muda mrefu sijui utekelezaji wake utachukua muda gani.

Kiukweli hii barabara ya Igawa-Tunduma ni aibu
 
Inyala pasikieni tu ila lile eneo ni hatari. Mwaka 2019 nimepoteza jamaa yangu pale kwa ajali gari ilifeli brake bomba la mafuta ikaenda kuchegama kwenye kingo za bomba la mafuta. Jamaa ndio ivyo alikufa akiwa bado kijana.

Pamechukua uhai wa watu wengi sana.
Pole sana mkuu
 
Mkuu ipo plan ya kupanua hii barabara kutoka Igawa mpaka Tunduma njia nne. Ila hiyo ni plan ya muda mrefu sijui utekelezaji wake utachukua muda gani.

Kiukweli hii barabara ya Igawa-Tunduma ni aibu
Asante mkuu kwa taarifa. Ila ilitakiwa iwe jambo la dharura kwani kulingana na maelezo ya jamaa, watu wanapoteza muda mrefu hapo. Fedha zipo ila ni mpango mbovu tu wa vipaumbele. Au hata wangeanza na sehemu zilizo korofi.
 
Mkuu unachosema ni kweli lakini serikali yetu unaifahamu vizuri too formalities. Barabara tu ya Nsalaga mpaka Ifisi walishawekeana sahihi ianze kujengwa toka mwanzoni mwa mwaka huu 2023 mpaka leo hakuna kinachoendelea.
 
Mpango wa muda mrefu ni serikali kujenga barabara nyingine Kwa maana ya kuipanua ili iwe njia nne na tayari kazi imeanza. Mpangomwa dharura ili kunusuru maisha ya watu kuwa na zamu ya foleni kati ya magari makubwa (malori) na magari ya abiria. Tangu utaratibu huu uanze hali ya ajali imepungua sana.
Mbeya ilitakiwa iwe jiji mwaka 2030
 
Huko ndiko huko kwao huyu ChoiceVariable ambaye anasema ni bora kuliko Dodoma, Tanga na Arusha!
We Kwa akili Yako ya kinyumbu unaweza linganishwa maisha ya Mbeya na takataka za Mikoa gani ukiacha Iringa?
20231117_135542.jpg
 
Babu nakuaminia lala nayo...hapo ndio mahala pake
 
Kitonga sasa hivi hawaruhusu ku overtake, foleni yake ni masaa mawili wakati wa kupanda zile km 8.

Siku ukisafiri uje useme kama lile ni jambo zuri.
Hapo waboreshe!!! Kupanda zipande lanes zote mbili kushuka hivyo hivyo.

Pia serikali ifikirie kutengeneza barabara ya andaki kwa kutoboa mlima huo au iweke njia nne hizo kilomita 8!
 
Hapo waboreshe!!! Kupanda zipande lanes zote mbili kushuka hivyo hivyo.
Ukifanya hivi watu watasubiria sana maana km 8 sio mchezo kwa malori.
Pia serikali ifikirie kutengeneza barabara ya andaki kwa kutoboa mlima huo au iweke njia nne hizo kilomita 8!
Kutoboa sijui gharama zitakuwaje. Wana plan ya kuwa na barabara nyingine inayopitia ifakara na haitapita mikumi wala kitonga.
 
Ukifanya hivi watu watasubiria sana maana km 8 sio mchezo kwa malori.

Kutoboa sijui gharama zitakuwaje. Wana plan ya kuwa na barabara nyingine inayopitia ifakara na haitapita mikumi wala kitonga.
Hiyo Ifakara kama itafupisha safari litakuwa jambo jema. Lakini, kule Kuna mlima wa kupanda kUelekea Kwiro Secondary...mlima hatari sana huo...unahitaji maarifa mengi!
 
Afrika hatuna akili za kutatua changamoto zetu. Unaweza kukuta hapo ufumbuzi ni kidogo sana ila hiyo akili hadi tusubiri mtaalamu wa kichina au kizungu aje kuturekebishia.

Hapo utakuta wahusika wamekaa vikao vingi sana vyakulipana posho kuja na huo ufumbuzi ambao kimsingi hauwezi kua ufumbuzi wa kudumu.
Nakuunga mkono mkuu. Hakuna kitu kibaya kama uvivu wa kufikiri.
 
Hiyo Ifakara kama itafupisha safari litakuwa jambo jema. Lakini, kule Kuna mlima wa kupanda kUelekea Kwiro Secondary...mlima hatari sana huo...unahitaji maarifa mengi!
Sipafahamu ifakara ila inawezekana umbali ukaongezeka.
 
Back
Top Bottom