Kwahiyo ninyi Walokole mliona pombe ndiyo dhambi kubwa kuliko zote?

Kwahiyo ninyi Walokole mliona pombe ndiyo dhambi kubwa kuliko zote?

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Salamu kwa wanajukwaa wote.

Jana nimepata mwaliko wa kuhudhuria sherehe ya send off. Nikajiandaa vizuri na kuwasili eneo la tukio. Shughuli ilianza vizuri na kila mgeni mualikwa alikuwa na uso wa bashasha. Wakati wa ufunguzi ulipowadia, MC alimkaribisha Mwinjilisti kwa ajili ya kufungua sherehe hiyo kwa sala.

Mwinjilisti aliposimama, badala ya kuomba na kufungua sherehe, alianza kuhutubia akidai hawezi kufungua sherehe ambayo ina pombe. Wote tulishangaa hoja ya Mwinjilisti yule, maana ni Mwinjilisti wa Kanisa la KKKT.

Kanisa la KKKT si linajulikana ndani yake wamo walevi. Je, kwa nini hamkatai sadaka zao? Mbona hao walevi kanisani mnawaruhusu kushiriki meza ya Bwana? Halafu huku nje mnataka kujifanya wa kiroho zaidi.

Kama kweli hamfungamani na pombe, basi tunaomba uongozi wa KKKT Taifa utoe mwongozo wa kuwazuia walevi kuingia kanisani mwao ili wakajue wapi pa kuabudu. Vinginevyo mnawagawa waumini wenu.

Ijulikane kuwa mimi situmii pombe na wala siungi mkono ulevi.
 
Binafsi nina experience sio nzuri na wafia dini.. ni watu wamejaa unafki sanaa, wanajifanya kupinga pombe wakati wao wanafanya usengenyaji, uongo, unafiki, uzinzi nk… dhambi ni dhambi… ukikemea kemea zote
 
Back
Top Bottom