Kwako Jemedari Said, JefLea na Collegemate Wilson Oruma

Kwako Jemedari Said, JefLea na Collegemate Wilson Oruma

Bodi watajua hizo points tatu watampa nani maana hakuna mechi itachezwa kwa uhuni waliofanya..
 
Bodi watajua hizo points tatu watampa nani maana hakuna mechi itachezwa kwa uhuni waliofanya..
Simba waligoma kucheza mechi, kilichokuwa kimebaki ni Bodi kuweka utaratibu Yanga apewe alama 3. Bodi kwa makusudi wakagoma kuweka utaratibu huo. Yanga atapewa alama 3 na mamlaka zingine zilizo juu
 
Kwa hiyo timu ikisema kwa barua rasmi kuwa haitaenda uwanjani, lakini ikaenda na kushinda mechi au kupata sare, bado timu pinzani inatakiwa ipewe point 3 kwa kuwa ile ilishatoa tamko la kutokwenda?
Kama kugoma kwao lakini baadaye wakaenda hakuvunji kanuni yoyote, matokeo yatakuwa halali
 
Watajwa hapo juu tangu juzi hadi leo baada ya habari ya Yanga kuandika barua kuomba pointi 3 kutoka Bodi ya Ligi, Mmekuwa kwa kujiamini mkidai kuwa Yanga hawezi kupata pointi hizo kwakuwa Mechi iliahirishwana na Bodi ya Ligi na Simba asingeweza kupeleka timu uwanjani wakati mchezo umeahirishwa.

Lakini mnasahau mambo yafuatayo.

1. Simba kwa barua rasmi aliutarifu umma kuwa hachezi mchezo ule. Kwahiyo Simba aligoma kucheza mchezo, yaliyofuata yote baada ya hapo hayabadilishi chochote kwenye hilo. Hivyo, mtu anaweza kusema Bodi ya Ligi hakuna walichoahirisha kwakuwa hadi wanakaa kikao Simba haikuwa imebadilisha msimamo. Hivyo iko wazi kikao cha Bodi ya Ligi na maamuzi yake yalikuwa juu ya kitu ambachi hakipo. They decided on nothing. Mechi iliisha kwa barua ya Simba hadi wanakaa mechi ilikuwa hamna. Huwezi kiahirisha mchezo ambao tayari upande mmoja umeshasema haupo tena kwa barua rasmi.

2. Baada ya barua ya mgomo ya Simba, Bodi wakafanya Kosa la kuitisha kikao na kufanya boko la kiahirisha mechi ambayo tayari haikuwepo kwakuwa Simba walikuwa wameshasema hawachezi na kwa barua rasmi.
3. Bodi wakacheza Boko la tatu, wakaacha kupeleka Maafisa wa mechi Ili kukamilisha utaratibu wa kuwapa Yanga Pointi 3 kwa mjibu wa Kanuni. Yanga kwa kulijua hilo wakapeleka timu uwanjani.

Kwakuwa Simba waligoma kucheza mchezo, ilikuwa ni wajibu wa Bodi kuendelea na taratibu. Sasa basi, kwakuwa Simba alikosea, Bodi ya Ligi nayo ikakosea, mtu hawezi kusema kuwa makosa ya Bodi ya Ligi yanaifaidisha Simba. Simba ataadhibiwa kwa kugoma kucheza mchezo bila sababu, Bodi ya Ligi itaadhibiwa kwa kushindwa kuwema taratibu za kuipa Yanga pointi 3 kwa mjibu wa kanuni. Na baada ya hayo, yatatoka maelekezo ya yanga kupewa haki yake kwa mjibu wa sheria. Yanga hawezi kunyimwa haki yake kwa makosa ya Bodi ya Ligi kushindwa kutafsiri Sheria.
Haya ni maoni yako kama yalivyo ya hao uliowataja yote hayasaidii kitu kwa bongo hii niijuayo ...rejea msala wa feisal utajua kama hujui nchi inavyo endeshwa!
 
Kwa hiyo mchezo uliopangwa kuchezwa katika tarehe nyingine ambao Yanga wameandika rasmi kutoenda uwanjani kuucheza, Yanga nao wanyang'anywe point hata kabla ya tarehe, muda na uwanja kujulikana?
Tumia akili kidogo,,bodi aiwezi kupanga tarehe ya mchezo mwingine wakati Kuna kesi ya madai mezani kwao ya kupinga utaratibu wa kuahirisha mechi ya kwanza,,mpaka bodi iwajibu yanga ni kanuni na Sheria Gani waliitumia kuahirisha mechi ya kwanza,,yanga wasiporidhika wanaendelea na kesi yao ngazi inayofata,,kwa maana iyo automatically akuna mechi nyingine kwa sasa mpaka hoja na madai ya yanga yajibiwe na bodi na kesi ikifika mwisho na bodi ikaonekana Iko sahihi ndio watakuwa na uwezo wa kutangaza tarehe nyingine ya mechi na sio vinginevyo!
 
Timu zikishafanya pre match meeting ni hatua ya kurasimisha mchezo

Kwamba Simba na Yanga zilitokea kwenye pre match meeting na zikatamka kuwa ziko tayari Kwa mchezo na watakuwepo bila kipingamizi

Baada ya pre match meeting hakuna mambo ya kuhairishwa match

Yanga haiwezi kuzuiwa kucheza Kwa taarifa za Instagram
Yanga haiwasiliani na bodi ya ligi kupitia Instagram
 
Mimi nikikiri kituo Cha polisi kuwa nimeiba au nimetenda kosi haimanishi kuwa kesi imeishia hapo. Lazima taratibu zingine za kisheria zifuatwe ikiwa pamoja na kufikishwa mahakaman.
Kwahyo Simba kusema hatupeleki timu uwanjan haimanishi kuwa Yanga apewe point 3, ilitakiwa taratibu za mechi zifuatwe mpaka mwisho. Waamuzi ilitakiwa wawepo uwanjan, Yanga wakaguliwe, waingie uwanjan, kuna dakika za kusubiri na ikiwa mpinzan hajatokea refa anamaliza michezo na timu husika unapewa ushindi.

Je, tarehe 8 hizo hatua zilifuatwa?
Ayo maswali ndio umeshaambiwa kisheria kosa alihalalishi kosa! Bodi ya ligi walifanya kosa la kiufundi kutopeleka waamuzi uwanjani,,waamuzi walitakiwa waende uwanjani na taratibu zote zifatwe,,Simba pia walifanya kosa kikanuni kugomea mechi na kutoa official statement ambayo itatumika kama reference ya kile ambacho bodi ilikiamua,,statement Ile ni kama iliwaelekeza bodi cha kufanya na bodi ikafata vile vile,,kwa maana iyo bodi ilipangiwa maamuzi na Simba na sio matakwa ya kikanuni!
 
Hiyo ni tafsiri yako mkuu, tafsiri yangu mimi Bodi waliahirisha mchezo ambao tayari haupo. Simba waligoma kucheza mechi na kwa maandishi na barua ya kugoma ipo na hajawahi kutenguliwa. Bodi hakuna walichoahirisha. Waaahirishe wasihahirisha mchezo ulikuwa tayari haupo kwakuwa Simba walikuwa wameshagoma. Ni kweli Bodi walipaswa wafanye huo utaratibu. Kutokufanya huo utaratibu maana yake Bodi walikiuka kanuni, kama ndivyo, ukiukwaji huo wa Kanuni hauwezi kufanya Yanga ikose haki yake.
We ndugu nahisi sio mtu wa mpira na huelewi unachoandika.

Timu moja kugomea mechi haimaanishi kuwa mchezo haupo.

Simba iliandika barua rasmi kugomea mchezo huo saa nane usiku masaa kadhaa kuelekea mchezo husika pamoja na barua hiyo rasmi ya Simba Sc mchezo bado ulikuwa upo palepale.

Barua ya bodi ya ligi iliyotolewa mchana wa siku ya mechi husika ndio iliyokuja kughairisha mchezo huo hivyo kuondoa uhalali wa yoyote kunufaika na matokeo ya mchezo huo maana haupo kwa siku husika

Bila barua hiyo ya bodi ya ligi mchezo wa derby uliendelea kuwepo hata kama Simba Sc wangesusia kwenda uwanjani bado tararibu zote za mechi zingefuatwa na aliyefika uwanjani kwa maana ya Yanga Sc wangepewa points zao 3 na magoli 3.

Barua ya Simba Sc haikuwa ya kughairisha mechi ni ya kugomea mechi, klabu yoyote haina mamlaka ya kughairisha mechi halali isipokuwa bodi ya ligi pekee ndio wana mandate hiyo.
 
Msizunguke zunguke sana ni kwamba bodi ya ligi iliamua kubeba msalaba wa Simba,,kesi iliyopo hapa ni baina ya yanga na bodi ya ligi,,bodi ya ligi iliingia kwenye mtego aidha kwa kujua ama kutokujua,,Sasa wao bodi ndio watajua wanawapaje yanga point zao inazozitaka,,huu ni mtego ambao niliwai kusema kwamba bodi ameingia pabaya!
 
Hamna namna yoyote Yanga atapewa points 3 za hiyo mechi zaidi ya kuzitafuta uwanjani, mechi haikuwepo siku wanaenda uwanjani na hakukuwa na taratibu zozote za kimichezo siku wapo uwanjani ni sawa walienda kufanya training tu wao kama timu hivyo hawatapewa kamwe points za mezani kama wanavyotamanj
 
Simba kusema hachezi mchezo kulikuwa hakujaghairisha mchezowa dabi, Bila taarifa ya bodi ya ligi taratibu nyingne zote za mchezo zingefuata na refarii wa mchezo angefika pale na timu iliyofika kwa maana ya Yanga wangepewa haki yao ya points 3 na magoli 3
Kilichotokea ni bodi kughairisha mechi hapo haina uhusiano tena na simba baada ya hiyo barua ya bodi hata simba na yanga wote wangeenda uwanjani hakuna matokeo yaliyokuwa yanatambulika na bodi
KAMA BADO KUNA MTU BADO ANAAMINI VITU VYA KITANZANIA VIKO SAWA SAWA BASI AKILI ZETU NI ZA KUCHUNGUZWA.
 
Haya ni maoni yako kama yalivyo ya hao uliowataja yote hayasaidii kitu kwa bongo hii niijuayo ...rejea msala wa feisal utajua kama hujui nchi inavyo endeshwa!
Hawana kumbukumbu, ni nchi ambayoWENGI WA wananchi wake WANAZIDIWA MAARIFA NA MBUZI,Wao Kila kitu kwao ni kubishana.Wakibadilisha mbinu mbalimbali za ubishanaji.
 
Back
Top Bottom