Kwako Jemedari Said, JefLea na Collegemate Wilson Oruma

Bodi watajua hizo points tatu watampa nani maana hakuna mechi itachezwa kwa uhuni waliofanya..
 
Bodi watajua hizo points tatu watampa nani maana hakuna mechi itachezwa kwa uhuni waliofanya..
Simba waligoma kucheza mechi, kilichokuwa kimebaki ni Bodi kuweka utaratibu Yanga apewe alama 3. Bodi kwa makusudi wakagoma kuweka utaratibu huo. Yanga atapewa alama 3 na mamlaka zingine zilizo juu
 
Subiri utasikia wazee wa "busara itumike" toka tiefuefu na wizara
 
Kwa hiyo timu ikisema kwa barua rasmi kuwa haitaenda uwanjani, lakini ikaenda na kushinda mechi au kupata sare, bado timu pinzani inatakiwa ipewe point 3 kwa kuwa ile ilishatoa tamko la kutokwenda?
Kama kugoma kwao lakini baadaye wakaenda hakuvunji kanuni yoyote, matokeo yatakuwa halali
 
Haya ni maoni yako kama yalivyo ya hao uliowataja yote hayasaidii kitu kwa bongo hii niijuayo ...rejea msala wa feisal utajua kama hujui nchi inavyo endeshwa!
 
Kwa hiyo mchezo uliopangwa kuchezwa katika tarehe nyingine ambao Yanga wameandika rasmi kutoenda uwanjani kuucheza, Yanga nao wanyang'anywe point hata kabla ya tarehe, muda na uwanja kujulikana?
Tumia akili kidogo,,bodi aiwezi kupanga tarehe ya mchezo mwingine wakati Kuna kesi ya madai mezani kwao ya kupinga utaratibu wa kuahirisha mechi ya kwanza,,mpaka bodi iwajibu yanga ni kanuni na Sheria Gani waliitumia kuahirisha mechi ya kwanza,,yanga wasiporidhika wanaendelea na kesi yao ngazi inayofata,,kwa maana iyo automatically akuna mechi nyingine kwa sasa mpaka hoja na madai ya yanga yajibiwe na bodi na kesi ikifika mwisho na bodi ikaonekana Iko sahihi ndio watakuwa na uwezo wa kutangaza tarehe nyingine ya mechi na sio vinginevyo!
 
Timu zikishafanya pre match meeting ni hatua ya kurasimisha mchezo

Kwamba Simba na Yanga zilitokea kwenye pre match meeting na zikatamka kuwa ziko tayari Kwa mchezo na watakuwepo bila kipingamizi

Baada ya pre match meeting hakuna mambo ya kuhairishwa match

Yanga haiwezi kuzuiwa kucheza Kwa taarifa za Instagram
Yanga haiwasiliani na bodi ya ligi kupitia Instagram
 
Ayo maswali ndio umeshaambiwa kisheria kosa alihalalishi kosa! Bodi ya ligi walifanya kosa la kiufundi kutopeleka waamuzi uwanjani,,waamuzi walitakiwa waende uwanjani na taratibu zote zifatwe,,Simba pia walifanya kosa kikanuni kugomea mechi na kutoa official statement ambayo itatumika kama reference ya kile ambacho bodi ilikiamua,,statement Ile ni kama iliwaelekeza bodi cha kufanya na bodi ikafata vile vile,,kwa maana iyo bodi ilipangiwa maamuzi na Simba na sio matakwa ya kikanuni!
 
Kama haya maelezo yako ni kweli basi hakuna point tatu za mezani kwa Yanga
Point zitapatikana tu unajua mashabiki mlio wengi amuelewi Aya mambo yanavyokwenda lakini mtakuja kuelewa ni suala la muda tu!
 
We ndugu nahisi sio mtu wa mpira na huelewi unachoandika.

Timu moja kugomea mechi haimaanishi kuwa mchezo haupo.

Simba iliandika barua rasmi kugomea mchezo huo saa nane usiku masaa kadhaa kuelekea mchezo husika pamoja na barua hiyo rasmi ya Simba Sc mchezo bado ulikuwa upo palepale.

Barua ya bodi ya ligi iliyotolewa mchana wa siku ya mechi husika ndio iliyokuja kughairisha mchezo huo hivyo kuondoa uhalali wa yoyote kunufaika na matokeo ya mchezo huo maana haupo kwa siku husika

Bila barua hiyo ya bodi ya ligi mchezo wa derby uliendelea kuwepo hata kama Simba Sc wangesusia kwenda uwanjani bado tararibu zote za mechi zingefuatwa na aliyefika uwanjani kwa maana ya Yanga Sc wangepewa points zao 3 na magoli 3.

Barua ya Simba Sc haikuwa ya kughairisha mechi ni ya kugomea mechi, klabu yoyote haina mamlaka ya kughairisha mechi halali isipokuwa bodi ya ligi pekee ndio wana mandate hiyo.
 
Msizunguke zunguke sana ni kwamba bodi ya ligi iliamua kubeba msalaba wa Simba,,kesi iliyopo hapa ni baina ya yanga na bodi ya ligi,,bodi ya ligi iliingia kwenye mtego aidha kwa kujua ama kutokujua,,Sasa wao bodi ndio watajua wanawapaje yanga point zao inazozitaka,,huu ni mtego ambao niliwai kusema kwamba bodi ameingia pabaya!
 
Hamna namna yoyote Yanga atapewa points 3 za hiyo mechi zaidi ya kuzitafuta uwanjani, mechi haikuwepo siku wanaenda uwanjani na hakukuwa na taratibu zozote za kimichezo siku wapo uwanjani ni sawa walienda kufanya training tu wao kama timu hivyo hawatapewa kamwe points za mezani kama wanavyotamanj
 
KAMA BADO KUNA MTU BADO ANAAMINI VITU VYA KITANZANIA VIKO SAWA SAWA BASI AKILI ZETU NI ZA KUCHUNGUZWA.
 
Haya ni maoni yako kama yalivyo ya hao uliowataja yote hayasaidii kitu kwa bongo hii niijuayo ...rejea msala wa feisal utajua kama hujui nchi inavyo endeshwa!
Hawana kumbukumbu, ni nchi ambayoWENGI WA wananchi wake WANAZIDIWA MAARIFA NA MBUZI,Wao Kila kitu kwao ni kubishana.Wakibadilisha mbinu mbalimbali za ubishanaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…