Kwanza naomba kukupongeza kwa kuendelea kuaminiwa kwako kutumikia serikakli yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia awamu ya nne hadi leo awamu ya sita hongera sana.Naomba kuzungumza na wewe leo wakati huu unapoenda kushika madaraka ya wizara mpya lakini kwa kweli nikili wazi kuwa kwako kitu kinachoitwa uwaziri sio kitu kigeni kabisa hivyo wewe ni mzoefu wa kazi hii.
Mheshimiwa waziri naomba kukuomba jambo moja ikikupenda ulifanyie kazi nalo ni; MALIPO YA MAPUNJO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA HASA WALIMU.
Watumishi waliopanda madaraja mwaka elfu 2012 na 2015, wengi wao wanadai stahiki zao,sijazungumzia madeni ya mwaka 2019 kwa sababu madeni haya serikali ya awamu ya sita inaendelea kuyalipa, na watumishi wanafurahi, na wana matumaini makubwa na serikali yao ya awamu ya sita hongereni sana kwa hili.
Nimeona nifikishe kwako mheshimiwa waziri kilio hiki cha watumishi cha muda mrefu kwani madeni ya mwaka 2012 na 2015, serikali ya awamu ya tano iliyakataa kwa kuutangazia umma wa watanzania kuwa ilishalipa yote ilihali hawakulipa madeni yote kwa wakati huo unaweza kufanya uchunguzi mheshimiwa waziri ili ujiridhishe na hiki nilichokiandika hapa.
Hata hivyo nikukumbushe pia kuwa kuna madeni ya mwaka elfu 2021 yaliyotengenezwa kwa makusudi na baadhi ya maafisa utumishi wa halmashauri zetu nchuni kwa kuchelewa kukamilisha zoezi kwa wakati kama walivyotakiwa na wizara yako hapo mwaka jana - 2021 june,haya malimbiki pia naomba uyashughulikie ikikupendeza.
Mwisho kwa umhimu wake naiomba serikali kupitia wizara yako ilipe madeni haya automatically kwa kuwa data (taarifa) za watumishi wanazo huko wizarani kuwa huyu hakulipwa stahiki zake kwani changamoto kubwa wanayokumbana nayo huku chini katika halmashauri zetu, maafisa utumishi wanaficha au kupoteza form nyingi za watumishi wenye madai. Hivyo matokeo yake majina hayafiki wizarani huku watumishi wanabaki kuilalamikia serikali pasipo na ulazima. Ni hayo tu kwa leo mheshimiwa waziri ninakutakia kazi njema na heri ya mwaka mpya 2022,Kazi iendelee.