The introvert
JF-Expert Member
- Sep 15, 2023
- 1,508
- 3,136
Hii ni kwako wewe mfanyakazi unaejitafuta kimaisha na kwa wote wanaofanya au kutarajia kufanya kazi ya kupokea mishahara
Kama mshahara wako ni shilingi laki moja, waambie nduguzo unalipwa elfu 60 na watu baki waambie unalipwa elfu 40.
Namba hazitakiwi kuwa halisi, ukitaja kiwango halisi wataongeza 'vizinga.'
Maana watacheza na shida zao kulingana na mshahara wako.
Usipokaa sawa utaanza zile, "kila nikishika hela shida haziishi...huyu anasema hivi, na yule anataka vile."
Hawana shida hivyo, ni vile wanajua kipato chako na mbaya zaidi mmoja hajui kama mwingine 'kakulabua' So, wanaweza kuja kwako watu zaidi ya mmoja kwa nyakati tofauti.
Na hata kama wana shida kweli, iwe wewe au bila wewe wata-survive tu.
Huwezi kumaliza shida za kwenu. Amua kwa hekima!
Usisahau, tulikubaliana mwaka huu tunajichagua kwanza.
✍🏿 The introvert