Kwako Mpendwa wetu Unique Flower

Kwako Mpendwa wetu Unique Flower

Sawa shemeji lkn kumfuata huko huko njema zaid ya hii
Ni vile tu Sipendi na siwezi hata iweje kuanika mazungumzo ninayo fanya na mtu. Hiki ni kiapo nilichojiapiza hata kama atanifanyia ubaya kiasi gani. Lakini huu uzi umesaidia wengi na yeye sidhani kama ni msomaji maana sio kwa sonona aliokuwa nayo
 
Mi naona still haja teleza au kuanguka Sana.
Na recall 2023 mwanzoni was the hardest time in my life.

Imagine you work hard, gets some few cash.
Ila amani hakuna, hata ukiona simu Ina ita ni msala mzito.

Hudaiwi na mtu, ila ni kama roho yako yenyewe iko jela.
Mi ni fan mkubwa wa vitabu, ila hata niki Soma sielewi kitu. Damn shit.

Aisee nili jipaga likizo nyingi mno, Kuna kipindi I was spending my vichenchi hovyo.
coz nili hisi muda sio mrefu navuta kamba🤓😄.

Guess what !!?, katikati ya Mwaka Jana, ndo nika kutana na 1 angel of mine.
AIsee thanks to her, my soul was saved.
 
Manyanza nimesoma post yako.
Sijakata tamaa mie yakupata mwanaume wakunioa kweli sio rahisi. Kuweka maagano hadi ndoa ndio ni ngumu ila mie sina stress za mapenzi hebu naomba mtaji wa ml 100 hilo tu nitakushukuru.

KWa sasa nawaza sana njia yakupata hela tu mengine hakunaga . Wanaume wapo tu na mtu akija kama amekuridhia mnaoana . Sina shida nawatu wananipenda ila sasa sina hamu ya kufanya tendo na sijafikia lengo .

Kama unataka kunisaidia nisaidie .
Mapenzi ni enzi za 2019 ndio ungeandika hii mesage .
Good day .
 
Habari yako Miss Unique Flower , nikiwa kama moja ya Wanachama wa JamiiForums nachukua nafasi kukupa ushauri huu hapa jamvini. Soma huu Uzi mara nyingi uwezavyo ili kuleta mabadiriko ya afya ya Akili yako.

NB: Wewe ni Mtu wa thamani sana acha kuwababaikia Wanaume , anayekupenda kweli atakufuta Mwenyewe lakini ukiwa unawashobokea watakutumia na kuzidi kukuvuruga akili yako na utajiona haufai.

Sisi sote tunapitia msongo wa mawazo kwa njia tofauti. Mara nyingi, tunaweza kushindwa kujua kuwa tunachopitia ni msongo wa mawazo. Ikiwa unapata mabadiliko haya, kuna uwezekano kuwa unakabiliwa na msongo wa mawazo.

1• Kupoteza hamu na tamaa ya kufanya yale mambo uliyokuwa furahia hapo mwanzo

2• Kuhisi kukata tamaa na kukosa tumaini

3• Kujihisi vibaya kujihusu Mwenyewe, au kuhisi kuwa umefeli maisha na kujiona hauna thamani.

4• Kujihisi mvivu au kuhisi kutotulia, kubabaika (Unakosa utulivu kwa Kila jambo ufanyalo)

5• Unawaza kwamba ni bora kufa au kujiumiza kwa njia yoyote ili upate faraja kutoka kwa watu wengine.


Je, unawezaje kudhibiti hisia za msongo wa mawazo?

Fanya haya ili kudhibiti Msongo wa mawazo

1. Mazoezi
Shughuli kama vile kukimbia, kucheza mpira wa miguu, kutembea, ni moja ya mambo yanayo saidia kuinua mhemko wako na kukusaidia kulala vizuri.

Kufanya mazoezi
mara kwa mara pia hukusaidia kusahau wasiwasi na shida zako na husaidia kusahau
mawazo ambayo yanasababisha msongo wa mawazo.


2. Kulala
Kulala hupunguza msongo wa mawazo sana. Kuwa na utaratibu wa kulala
husaidia kukutuliza, inaboresha hali yako na inakusaidia kufanya maamuzi bora.
Wataalamu wanapendekeza kulala kwa angalau masaa 8 kila usiku.

Jaribu kupata mpangilio bora wa kulala kwa kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa
pombe au kafeini (chai / kahawa) wakati wa kulala unapokaribia.


3. Lishe Bora
Ingawa chakula hakiwezi kuondoa hisia za kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo kabisa, lishe bora inaweza kuongeza mhemko wako, kupunguza shida za kuwa na shinikizo la damu, na kujenga kinga yako ya mwili. Kuna vyakula ambavyo vinaweza kupa utulivu wa msongo ikiwa unazijumuisha kwenye lishe yako ya kila siku. Hii ni pamoja na vyakula vyenye:


• Vitamini C na madini - matunda na mboga
• Protini kama mayai, nyama, na maharagwe.
• Vyakula vinavyotoa nishati kama mahindi, ngano na viazi vitamu.


4. Panga kazi yako na uorodheshe majukumu yako

Panga kazi zako za kila siku ukianza na kazi za haraka. Mwishoni mwa siku, zingatia majukumu ambayo umeweza kuyafanya. Hii itakusaidia kukumbana na hisia za kuzidiwa na shughuli zako za kila siku.

5. Wakati
Usibebwe sana na kasi ya maisha. Chukua muda kupumzika ili ufurahi na ufanye kitu unachofurahia kila siku. Hii haitaongeza burudani zako tu, lakini pia itakupa kitu cha kukupatia tumaini la baadae.


6. Zungumza na watu unaowaamini
Kuzungumza na kuwaambia watu wa karibu nawe shida zako kunaweza kusaidia kupunguza viwango vyako vya msongo wa mawazo, huku kujumuika na familia na marafiki wanaweza kukusaidia kuwa mtulivu na kupunguza msongo wa mawazo. Ni vizuri kuzungumza na wengine kwani watu wanaweza kukusaidia kupata suluhisho la kile kinachokusumbua. Kumbuka, kuna watu ambao wanaweza kuwa wamepitia hali kama wewe. Hata hivyo, ikiwa haufikiri kuzungumza, unaweza kuandika hisia zako.


7. Epuka njia mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo kunaweza kusababisha kuongezeka kwa kishawishi cha kutumia madawa ya kulevya kama vile pombe, sigara, na vitu vingine. Ingawa dawa hizi zinaweza kusaidia kwa muda lakini husababisha hatari kubwa kiafya.

Matumizi mabaya ya dawa za kulevya pia husababisha ulevi, kuongezeka kwa viwango vya msongo wa mawazo na athari mbaya za kitabia na kijamii.

Jihadhari na tabia zingine mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo kama vile kula sana na mazoea hatari ya uhusiano kama tabia hatari za kingono ambayo ni hatari kwa afya yako.

#Nikutakie Ijumaa Kariim
@Unique Flower anasoma huu uzi huku anahisi uchungu moyoni, usiubane na ukihisi kulia wewe lia tuu sumu ikutoke moyoni na ukimaliza jiambie nimejisamehe mwenyewe na nafsi yangu pia nisamehe. Alafu songa mbele dada maua
 
@Unique Flower anasoma huu uzi huku anahisi uchungu moyoni, usiubane na ukihisi kulia wewe lia tuu sumu ikutoke moyoni na ukimaliza jiambie nimejisamehe mwenyewe na nafsi yangu pia nisamehe. Alafu songa mbele dada maua
Nilie ili iweje??
 
Manyanza nimesoma post yako.
Sijakata tamaa mie yakupata mwanaume wakunioa kweli sio rahisi. Kuweka maagano hadi ndoa ndio ni ngumu ila mie sina stress za mapenzi hebu naomba mtaji wa ml 100 hilo tu nitakushukuru.
Kitu kinachokuja kwa urahisi hauwezi ukakithamini na kukitunza, ukipata hiyo 100 M utatumia vibaya na ikiisha utachanganyikiwa na kupata magonjwa ya sonona. Unawaza kunipa business plan yako inayochanganua ni namna gani hiyo hela utaiwekeza na kuleta faida? Kama una mchanganuo wenye akili nitumie kwenye email yangu.
manyanza@jamiiforums.com niusome kwanza halafu Kuna watu wa UAE nijaribu kuwashawishi
 
Kitu kinachokuza kwa urahisi hauwezi ukakithamini na kukitunza, ukipata hiyo 100 M utatumia vibaya na ikiisha utachanganyikiwa na kupata magonjwa ya sonona. Unawaza kunipa business plan yako inayochanganua ni namna gani hiyo hela utaiwekeza na kuleta faida?
Bwana mikopo upo?? Nitumie account ya email yako
 
Haupo serious ukitoa hii hela natembea na chupi kichwani walahi
Sitoi hela Mimi Ila hiyo hela bila kuwa na Business Plan hauwezi kuipata. Alafu masuala ya kuvaa Chup*** kichwani yanaingiaje hapa ? Na hapo huo unakuwa sio mkopo ni mpango biashara wako wa hela hiyo watu ndio wataweka hiyo pesa.
 
Sitoi hela Mimi Ila hiyo hela bila kuwa na Business Plan hauwezi kuipata. Alafu masuala ya kuvaa Chup*** kichwani yanaingiaje hapa ? Na hapo huo unakuwa sio mkopo ni mpango biashara wako wa hela hiyo watu ndio wataweka hiyo pesa.
Wee na wee to pesa hiyo..
Tuone mtu anaye tembea na pichu kichwani anafananaje 😂😂😂😂
 
Sitoi hela Mimi Ila hiyo hela bila kuwa na Business Plan hauwezi kuipata. Alafu masuala ya kuvaa Chup*** kichwani yanaingiaje hapa ? Na hapo huo unakuwa sio mkopo ni mpango biashara wako wa hela hiyo watu ndio wataweka hiyo pesa.
Sasa haupo serious nimehitaji account yako unanipa ya jami forum haupo serious
 
Back
Top Bottom