Kwako Mwakalebela

Kwako Mwakalebela

Riz king

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
276
Reaction score
549
Kimsingi nataka nikueleze kuwa unaanza kuishi maisha ya kuongoza soka kizamani. Umejitia aibu sana na ndo hapo sishangai Msigwa kukucharaza mwaka2015.
Mwakalebela kama umeshindwa kuiongoza Yanga uache mipasho. Tuachie timu yetu, na ndiyo maana unafanya mambo ya hovyo pale Yanga ili Dr Msolla aonekane ni mpuuzi kwa sisi wanachama. Umeshindwa kuelewana na Msolla na siyo siri bifu mlilonalo na Msolla wewe ndo sababu. Na hata wajumbe wa kamati ya utendaji kujiuzulu ni wewe ndo uliongoza fitna dhidi ya GSM. Shukuru korona lakini sisi wanachama tutakukataa tu subiri hili janga lipite. Haujatushinda Wana Yanga tumbo wewe
 
Ameitia aibu Yanga anafanya utani kwenye mambo serious hafai kabisa ni bora ajiuzulu kabisa ni bora angekuwa kimya tu Hii ni aibu kubwa kwa kiongozi mkubwa kama wewe sisi mashabiki tutakuamini vipi tena ukija kuongea tena jambo lingine linalohusu klabu. Mambo ya utani waachie wakina Jimmy Kindoki na Nugaz hufai kabisa nimeanza kuelewa kuwa ndio maana kule Iringa ulipigwa chini ubunge hufai kabisa bora mabadiliko ya uendeshaji ya klabu yafanyike haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wapenzi wa yanga huko insta wanaonekana vilaza sana wa mpira?
Wanamtia kiburi eti asipaniki kwa vile kulikuwa na utani kama huo juu ya shishimbi!

Wangekuwa wanaingia hapa ningewaambia kuwa sheria haikatazwi kumnunua mchezaji hata kama ana mkataba wa miaka sita.Ila zipo taratibu zinazotakiwa kufuata kama kanuni inavyosema.

Club au mtu yeyote haruhusiwi kuongea na mchezaji moja kwa moja kwa nia ya kumshawishi ajiunge na timu yao akiwa na mkataba isipokuwa kama wana nia ya kumpata,watapeleka ofa kwa club anayochezea.Iwapo club hiyo itaridhia,wataruhusiwa kumsajili kwa kuuvunja mkataba aliokuwa nao.

Mazingira pekee wanaporuhusiwa kuongea na mchezaji,ni pale ambapo mkataba wake umebakiza chini ya miezi sita kumalizika.

Sasa niwaulize maswali,ni kiongozi gani wa Simba alikiri kuongea na shishimbi kwa nia ya kumshawishi ajiunge na Simba?

Shishimbi alikuwa amebakiza muda gani wa mkataba wake?

Mbona hamkuchukua hatua iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za soka?
Hii ni yanga ama utopolo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifafa cha tar 8 march hakijaisha kwa mikia mtanyooka mwaka huu
 
Back
Top Bottom