Kwako Ndugu Kinana: Kama kweli mmedhamiria kupambana na rushwa kwenye chaguzi za CCM basi anzeni na Kihongosi Katibu mkuu wa UVCCM
Ha ha haa
Tafakari yetu, yaani CCM ipambane na rushwa! Acha utani ndugu yangu au labda huijui CCM, unaisikia tu.
Kwa CCM rushwa ndio hewa ya oxygen, sasa si heri ungewashauri tu wajitundike kamba wajinyonge? Eti wapige vita rushwa, thubutu!
Kwa CCM rushwa ni msingi uliolibeba dude hilo, sasa wewe kama unataka waubomoe msingi si heri uwaambie tu wanywe/wameze sumu!
Kwa CCM rushwa ndio tawi lililowabeba, sasa kuwaambia wakate hilo tawi, ili iweje? Si heri wajirushe kutoka juu ya lile gorofa lao Lumumba!
Acha utani ndugu yangu, kwa CCM wala rushwa wakishughulikiwa nakuapia hapatabakia hata harufu ya mtu toka mdogo hadi mkubwa.
CCM ni ile ile, watu ni wale wale, rushwa iko pale pale!
Myu yeyote anayeishabikia CCM ni mla rushwa mtarajiwa>