Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Mkuu Min,

Hoja si serikali haina dini, hoja ya mzee Mohamed ni Kwanini uwiano uwe na tofauti kubwa? Anafikiri kuna mahala hakupo sawa kwa mamlaka katika chaguzi katika ngazi tofauti tofauti za uongozi.

Unafikiri nini kinasababisha mbali na kuwepo Raisi muislamu, waziri Mkuu muislamu lakini bado hapana mlinganyiko unaokaribiana?
Sasa kama mzani haujabalansi tangu kwa idadi ya waliosoma Rais yeye atawatoa wapi? Wewe angalia kwenye 100 Waslamu wako 10 wenye elimu dunia nzuri waliobaki ni madrasatul sasa Rais atafanyaje hapo?
 
Wakuu Heshima mbele.

Mimi binafsi kwanza niseme ni mtu ambaye napenda sana kusoma historia tofauti tofauti. Nimekuwa nikivutiwa na mzee wangu Mohamed Said katika maandiko yake mengi, mzee Mohamed saidi ni mtu ambaye mara nyingi ameweza kuielezea historia Ya Tanganyika tangu harakati za uhuru zinapoanza mwanzoni kabisa, mzee Mohamed ameweza kuelezea ni kwa namna gani wazee Wa mwanzoni kabisa wa TANU ambao wengi wakiwa ni waislamu na wakaweza kumpokea mwalimu kwa upendo wote.

Mzee Mohamed Said mimi ni mtu ambaye napenda sana unachoandika. Lakini mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakimshutumu mbali na kipaji na talanta kubwa aliyonayo ya kuandika, historia zake mara nyingi huwa zinaambatana na udini ( ZEALOTISM).

Mfano; katika moja ya komenti zake nitamnukuu hapa chini

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Hio ni moja ya komenti aliyoiandika mzee wangu Mohamed kuhusu uwiano kati ya waislamu Na wakristo. Na akaendelea chini kwa kusema kwamba:

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

Kama takwimu hizi ni za kweli mzee wangu Mohamed Said unafikiri ni nini kinasababisha kuendelea kuwepo kwa Mizani kutoku-balance?

Katika kitabu cha Kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. Umetuonyesha ni jinsi gani makubaliano Baina ya waziri mkuu wa Kenya Ndg. Jommo kenyata na waziri mkuu wa Zanzibar Ndg. Mohamed shamte hayakufanikiwa na kupelekea kunyanga’nywa Kwa waislamu Taasisi ya (MIOME) mombasa institute of muslims education.

Mzee wangu Mohamed si mtu mwenye nia mbaya akijaribu kueleza kwa namna gani historia ya TANU haikuwa sawa kwa kiasi fulani, hivyo anajaribu kutufumbua macho zaidi. Lakini ni kama vile waislamu bado ni watu ambao kwa maandishi yake hakuna uwiano sawa na wakristo.

Mzee wangu Mohamed Said mimi naomba kufahamu kutoka kwako mbali na yote , ni kipi kifanyike ili kutengeneza uwiano sawa baina ya waislamu na wakristo katika Ngazi zote za nchi yetu? Haswa katika kipindi hichi tulichonacho elimu inatolewa kwa usawa bila kujali dini zetu.

NB. This is not intended to divisive or inflammatory only for learning purpose.
hata kabla mohamed hajakujibu,kuweka uwiano sawa ni kuteua kwa kuzingatia usawa wa kidini kwani kwa sasa dini zote watu wake wamesoma
 
Mimi nafikiri taasisi mbalimbali za katholic na Lutheran hutoa wasomi mahiri katika nyanja mbalimbali , kuliko taasisi za kiislamu na madhehebu mengine hasa ya kilokole , ndio maana wakiitajika watu mahiri kwenye ngazi mbalimbali za kiutawala asilimia kubwa hukuta ni watu wa dini hizo , wala sifikiri kama kuna ubaguzi wowote .
FB_IMG_1700665386000.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1700665386000.jpg
    FB_IMG_1700665386000.jpg
    8.1 KB · Views: 1
Mkuu Etugrul Bey

Mzee Mohamed anasema chaguzi hizi zinakinzana na katiba ibara ya 13 (4) (5)
Ambacho kinasema kuhusu ubaguzi wa aina yoyote ile.

Katika maneno yake mzee Mohamed inaonyesha dini ya kikristo inapendelewa zidi ya dini ya kiislamu.

Swali ni kwamba kulingana na kifungu hicho cha katiba serikali inatazama ufanisi na elimu ya mtu katika teuzi au inatazama Dini pasi na sababu hizo zingine kuwepo?

Lakini pia Mkuu;

Mbali na kuwepo kwa Raisi muislamu na waziri mkuu, mbali na kuwepo kwa usawa wa kupata elimu unafikiri ni Kwanini tatizo hili bado lipo?
Huyu Mohamed Said ni mdini tu anaetapatapa. Ukitaka kujua hilo soma vitabu vyake vyote uone na articles zake, mahojiano anayifanyiwa, utagundua huyu ni activist wa Islamic ingefaa apewe nafasi pale bakwata.
 
hata kabla mohamed hajakujibu,kuweka uwiano sawa ni kuteua kwa kuzingatia usawa wa kidini kwani kwa sasa dini zote watu wake wamesoma
Why iwe kidini?
Kwanini isiwe kikabila, kimaeneo/kikanda, kijinsia, kitaaluma, kiuchumi?
Hizo takwimu za uwiano wa wasomi kidini umezitoa wapi?
Mwisho kabisa, kuteua kwa uwiano wa kidini kuna mchango gani katika kuongoza watu?
 
Media wanapofanya mahojiano naye wanamuita mwandishi na mwanahistoria kana kwamba anayoyaandika ni mazuri kwa wote kumbe ni mchochezi, anaandika kuonesha jamii ya imani yake haipewi haki kwenye masuala mbalimbali ya maamuzi ya nchi akidai jamii yake ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kuleta uhuru wa nchi hii dhidi ya wakoloni. Anajifanya hajui kuwa jamii yake haikuwapokea watangulizi wa ukoloni na iliwaonesha maeneo ya mbali na wao kukumbatia utamaduni wa dini yao waliyoipokea toka kwa wafanyabiashara wa kiarabu waliotoka uarabuni. Angeandika athari zilizosabishwa na dini ya wafanyabiashara hao kwa jamii yake kuwahadaa na miungu yao mpakaa wakadumaa kifikra huku jamii zingine zikisoma elimu ya wamisionari wa kizungu angeonekana ni wa maana ila kilio chake kikuu ni kutaka watu wa dini yake waonekane ni wengi katika teuzi za nchi.
 
Katika mazingira ambayo karibu kila dhehebu/makundi ya dini ya Kikristo wanamiliki mashule ya kutosha na vyuo, unategemea cream ya viongozi itatokea dini gani ikiwa tutatumia usomi kama sifa za kuteuliwa?
 
Kama anaona jamii ya dini yake haipewi uteuzi wa kuridhisha aanzishe chama cha siasa chenye sura kamili ya dini yake na lengo kuu iwe ni hayo mambo anayoyaandika. Uhuru upo ajaribu kuanzisha chama hicho tuone kama atapata wanachama wengi wa kukiunga mkono chama chake kwa hizo sera za kidini za kubagua watu wa nchi moja
 
Mzee huyu ni Cuf au ACT nadhani,yuko sahihi kwa baadhi ya mambo ila ni muoga sana kipindi cha JPM alikuwa anaandika kwa tahadhari akiogopa kushughulikiwa,sasa anajiachia tu
Mdukuzi,
Sijapatapo kuacha kuandika wakati wowote.

Sijapatapo kushikwa na hofu nikaacha kuandika.

Angalia hapa niko katika jina langu kwa sura na sauti.

Wewe ndiye muoga uliyeficha jina lako.

Niandikayo yote yako hapa yapitie na lete ushahidi kuwa mimi muoga.
 
Huyu Mohamed Said ni mdini tu anaetapatapa. Ukitaka kujua hilo soma vitabu vyake vyote uone na articles zake, mahojiano anayifanyiwa, utagundua huyu ni activist wa Islamic ingefaa apewe nafasi pale bakwata.
Peaky...
Ukiwa "mdini" unakusudia Uislam umesema kweli kabisa.

Naupenda sana Uislam.

Ukiwa kuniita "activist wa Islamic," unakusudia kushughulika na Waislam na Uislam hakika umesema kweli.

Kwani haya hayaruhisiwi mtu kufanya?

Hili la kupewa nafasi BAKWATA nakuomba unifafanulie nafasi ya BAKWATA nikafanye kazi gani?
 
Achana na huyo mzee, hoja yake ni mfu kwa 100%.
Mimi nitakusaidia kukujibu na kumkosoa vikali mzee Mohamed Said.

1. Nchi yetu haina dini, hivyo huwezi kutumia kigezo cha dini katika kuajili na kuteua nafasi mbali mbali za utumishi wa umma.

2. Dini ni suala la moyoni na sio jambo la lazima kubakia moyoni mwa mtu siku zote (inawezekana wakati nateuliwa nilikuwa Mkristo, wakati naapa nikawa Muislamu na wakati natumbuliwa nilikuwa mpagani), huwezi kujua dini halisi ya mtu mpaka uingie moyoni mwake. Kutazama majina ya mtu, haitoshi kujua imani yake halisi ya kidini.

3. Jamii imegawanyika katika mambo mbalimbali yakiwemo Imani, Kabila, Jinsia, Kipato, Taaluma, Makazi. Kama serikali itaamua kuteua watu kwa misingi yao ya kijamii basi uwiano wa kidini pekee hautoshi kuwawakilisha hao watu.

4. Rais atateua watu kutoka katika bwawa (pool) la watu wenye sifa stahiki kwake, hakuna mtu anajua hilo bwawa analotumia Rais kuchagua watu wake lina uwiano gani kidini. Unaweza kukuta ndani yake lina waislamu wachache sana, hivyo litaishia kuteua waislamu wachache.

5. Mamlaka ya uteuzi iko ndani ya utashi na uhuru wa Rais aliyepo madarakani, anawajibika kwake mwenyewe, hivyo huwezi kujenga hoja ya kuwepo uwiano wa kidini katika kuteuliwa.
Zanzibar...
Unataka kufanya mnakasha na Mohamed Said kwa uandishi huu ulioweka hapa?
 
Kupitia comment yako sasa naamini kwamba kumbe kuna watu huwa mnawasingizia wana id mbili kumbe uzushi tu
kwani we huwa hugundui hilo? Mtu anakula ban kisha anaibuka na nyingine. Sio mbili tu hata tatu na zaidi watu wanazo kwa malengo yao. Kuna wale verified wanajulikana kabisa majina yao ni halisi na sura zao tunazijua, we unadhani wataacha kuwa na ID zingine zitakazowapa uhuru wa kuandika maoni yao tofauti na tunavyowajua misimamo yao?
 
ni chama cha siasa chenye element za udini. Ndio cuf ya wakati ule, hawakuona aibu kuji brand kwa dini ile katika mikao ya mikutano yao ya kampeni sura ilikuwa ni ya kidini
Loth...
Unaijua historia ya chama cha TANU kuanzia African Association 1929 hadi TANU 1954?

Ungeweza kuiweka TANU Dar-es-Salaam mbali na Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam waTanganyika)?

Hujui kwa nini ilikuwa vile?
 
Waislam wasomi wapo kwa kiasi chake tena ni wabobezi kwenye fani zao nawasio penda kuyumbishwa , sema tatzo la Tanzania mikoa mingi yenye jamii za Waislam wengi walikua nyuma kidgo kwenye mambo ya kielimu, apo tatizo sio dini tatizo ni vipaumbele vya jamii husika .

Mfano kwenye jamii ya wachaga hasa wamachame kuna jamii kubwa tu ya waislamu ila ni waislamu wabobezi kwenye nyanja ya elimu na mahiri sna kwenye biashara na maendeleo binafsi tofauti na jamii ya wazaramo au warangi ambapo pia kundi kubwa ni Waislam , unaona apo tatzo sio dini tatzo ni kipaumbele cha jamii husika.
Min...
Kipaumbele cha Waislam baada ya uhuru kupatikana ilikuwa elimu.

Mwaka wa 1962 kukaitishwa Muslim Congress agenda kuu kujenga shule na Chuo Kikuu kupitia EAMWS.

Shule zikaanza kujengwa na ilipofika mwaka wa 1968 EAMWS ikaanza ujenzi wa Chuo Kikuu.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA.

Huijui historia hii?
 
Hiki kizee kiwekwe kwenye orodha ya magaidi hatari.Ningekuwa mimi jiwe kusingekuwa hata na hizo sijui 10%,5% au 20%,zingekuwa zinasoma 1%,0.5% nk ili kukipa hiki kizee presha kukiua kabisa na presha maana kinapenda sana ubaguzi
 
Mimi nafikiri taasisi mbalimbali za katholic na Lutheran hutoa wasomi mahiri katika nyanja mbalimbali , kuliko taasisi za kiislamu na madhehebu mengine hasa ya kilokole , ndio maana wakiitajika watu mahiri kwenye ngazi mbalimbali za kiutawala asilimia kubwa hukuta ni watu wa dini hizo , wala sifikiri kama kuna ubaguzi wowote .
Min...
Hujui yaliyokuwa yakifanyika NECTA hadi Waislam wakafanya maandamano mwaka wa 2012?
 
Back
Top Bottom