Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

tangu ianzishwe lini uliona ina sura ya udini, kampeni zake watu wakikaa kidini? CHADEMA ni chama cha wote hakina udini

90% ya viongozi wake ni wagalatia halafu unasema hakina udini? au udini huwa unakuja kwa waislamu tu?
 
Kwan
Wakuu Heshima mbele.

Mimi binafsi kwanza niseme ni mtu ambaye napenda sana kusoma historia tofauti tofauti. Nimekuwa nikivutiwa na mzee wangu Mohamed Said katika maandiko yake mengi, mzee Mohamed saidi ni mtu ambaye mara nyingi ameweza kuielezea historia Ya Tanganyika tangu harakati za uhuru zinapoanza mwanzoni kabisa, mzee Mohamed ameweza kuelezea ni kwa namna gani wazee Wa mwanzoni kabisa wa TANU ambao wengi wakiwa ni waislamu na wakaweza kumpokea mwalimu kwa upendo wote.

Mzee Mohamed Said mimi ni mtu ambaye napenda sana unachoandika. Lakini mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakimshutumu mbali na kipaji na talanta kubwa aliyonayo ya kuandika, historia zake mara nyingi huwa zinaambatana na udini ( ZEALOTISM).

Mfano; katika moja ya komenti zake nitamnukuu hapa chini

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Hio ni moja ya komenti aliyoiandika mzee wangu Mohamed kuhusu uwiano kati ya waislamu Na wakristo. Na akaendelea chini kwa kusema kwamba:

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

Kama takwimu hizi ni za kweli mzee wangu Mohamed Said unafikiri ni nini kinasababisha kuendelea kuwepo kwa Mizani kutoku-balance?

Katika kitabu cha Kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. Umetuonyesha ni jinsi gani makubaliano Baina ya waziri mkuu wa Kenya Ndg. Jommo kenyata na waziri mkuu wa Zanzibar Ndg. Mohamed shamte hayakufanikiwa na kupelekea kunyanga’nywa Kwa waislamu Taasisi ya (MIOME) mombasa institute of muslims education.

Mzee wangu Mohamed si mtu mwenye nia mbaya akijaribu kueleza kwa namna gani historia ya TANU haikuwa sawa kwa kiasi fulani, hivyo anajaribu kutufumbua macho zaidi. Lakini ni kama vile waislamu bado ni watu ambao kwa maandishi yake hakuna uwiano sawa na wakristo.

Mzee wangu Mohamed Said mimi naomba kufahamu kutoka kwako mbali na yote , ni kipi kifanyike ili kutengeneza uwiano sawa baina ya waislamu na wakristo katika Ngazi zote za nchi yetu? Haswa katika kipindi hichi tulichonacho elimu inatolewa kwa usawa bila kujali dini zetu.

NB. This is not intended to divisive or inflammatory only for learning purpose.
Kwani vigezo vya kazi vinaangalia dini? Mnatumia vigezo gani kudhibitisha dini ya mtu au imani?
 
Nafauatilia huu mjadala nimegundua mambo kadhaa

1. Tukisema udini tz ni dini ya kiislam kwanini? Kwasababu taratibu zake ni za kijamaa haziendani na dini nyingine ndio maana waislam wanaandamwa au kuonekana tofauti na wa dini nyingine

2. Ukiristo umeimarika na una nguvu za kidola. Hapa ni kwanzia ngazi ya kimataifa ambapo ndio mataifa yenye nguvu duniani kwaiyo wakiristo wanajiamini na kuforce kutokuelewa agenda zinazofanywa na wakiristo wenzao kwakuwa ndio wenye mamlaka. Kwa waislam salini sana dola yenu ya kiislam irudi tena kama enzi za ottoman ndiyo mtaeleweka

3. Humu jamii forum wengi ni wakiristu na wachache waislam ambao hawana uelewa wa dini ya kiislam kwaiyo kuendesha mada za kiislam kwa wagaratia huwezi eleweka hata kidogo pole kwa mzee wetu Mohamed said vumilia tu hauna namna.

4. Hakuna mtu atakae kubali nduguye aonelewe au ashambuliwe kwa namna yoyote ile ndio maana unapolishambulia kwa hoja kundi lingine, lingine litakuja na hoja mbadala kwaiyo tuvumiliane tu dunia haijaumbwa sawa
 
90% ya viongozi wake ni wagalatia halafu unasema hakina udini? au udini huwa unakuja kwa waislamu tu?
hii nchi kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani aipendayo. Unaweza kubadili dini ili tu upate fursa kwa walizo nazo. Badili dini uwe mgalatia nawe uongeze hiyo asilimia upate uteuzi kama umeona hiyo ndiyo tija
 
Kwa nini mnataka kuleta uwiano kwa jambo ambalo ndani yake hakuna uwiano?

Hata ukikataa kwa takwimu zako Uchwara, idadi ya wasomi Wakristo ni kubwa mara tatu ya idadi ya Waislamu wasomi.

Sasa, kwa nini kundi dogo lipewe kipaumbele katika teuzi kwa minajili ya kuleta uwiano sawa wa kidini? Unataka mtu apewe nafasi kwa sababu tu ni wa dini fulani ili kuleta balansi? Kufanya hivyo tutakuwa tunatengeneza taifa la hovyo.

Lakini ukweli ulio wazi pia ni kuwa, idadi ya Wakristo Tanzania ni kubwa zaidi ya waislamu. Pamoja na kujitahidi kwao kuzaa ovyo ili kupata wafuasi wengi, lakini bado idadi yao ni ndogo mno. Na kuzaa huko kunazalisha idadi ya wahuni wengi wa dini husika.

Kwa nini tulete balansi kwenye sehemu penye uwiano usio sawia?

Mzee wangu Mohammed aache inferiority complex.
Leaking...
Naomba nifamishe maana ya "complex" na "inferiority" kwa Kiswahili ili nielewe hoja yako.
 
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.
Ingefaa kwa hizo nafasi Mohamed Said au mtoa mada mtuwekee hapa data za uteuzi kwa awamu hii ya 6 tuone..
Mohamed Said
 
Leaking...
Naomba nifamishe maana ya "complex" na "inferiority" kwa Kiswahili ili nielewe hoja yako.
"Inferiority complex" ni ile hali ya kujihisi mnyonge au dhaifu kwenye mambo fulani hata kama kiuhalisia siyo kweli. Kutojiamini
 
Achana na huyo mzee, hoja yake ni mfu kwa 100%.
Mimi nitakusaidia kukujibu na kumkosoa vikali mzee Mohamed Said.

1. Nchi yetu haina dini, hivyo huwezi kutumia kigezo cha dini katika kuajili na kuteua nafasi mbali mbali za utumishi wa umma.

2. Dini ni suala la moyoni na sio jambo la lazima kubakia moyoni mwa mtu siku zote (inawezekana wakati nateuliwa nilikuwa Mkristo, wakati naapa nikawa Muislamu na wakati natumbuliwa nilikuwa mpagani), huwezi kujua dini halisi ya mtu mpaka uingie moyoni mwake. Kutazama majina ya mtu, haitoshi kujua imani yake halisi ya kidini.

3. Jamii imegawanyika katika mambo mbalimbali yakiwemo Imani, Kabila, Jinsia, Kipato, Taaluma, Makazi. Kama serikali itaamua kuteua watu kwa misingi yao ya kijamii basi uwiano wa kidini pekee hautoshi kuwawakilisha hao watu.

4. Rais atateua watu kutoka katika bwawa (pool) la watu wenye sifa stahiki kwake, hakuna mtu anajua hilo bwawa analotumia Rais kuchagua watu wake lina uwiano gani kidini. Unaweza kukuta ndani yake lina waislamu wachache sana, hivyo litaishia kuteua waislamu wachache.

5. Mamlaka ya uteuzi iko ndani ya utashi na uhuru wa Rais aliyepo madarakani, anawajibika kwake mwenyewe, hivyo huwezi kujenga hoja ya kuwepo uwiano wa kidini katika kuteuliwa.
Ingawa wkt unaanza hoja yako ulisema unamkosoa mzee Saidi vikali lkn nilichokiona ni hadithi ya kusadikika na umeamua kujiridhisha mwenyewe

Unapoongelea kwamba dini ni swala la moyoni kwahiyo mhusika ndo anajua mwenyewe hii ni hadaa kubwa,,,sijui kama waislamu wangekuwa wengi kuliko wakristo ungethubutu kusema hivyo?

Pili umezungumzia kwamba kuna pool ambalo huenda wateule wanachukuliwa humo,je ni nafasi gani ambazo zinakosa wasomi wa kiislamu?
 
Wakuu Heshima mbele.

Mimi binafsi kwanza niseme ni mtu ambaye napenda sana kusoma historia tofauti tofauti. Nimekuwa nikivutiwa na mzee wangu Mohamed Said katika maandiko yake mengi, mzee Mohamed saidi ni mtu ambaye mara nyingi ameweza kuielezea historia Ya Tanganyika tangu harakati za uhuru zinapoanza mwanzoni kabisa, mzee Mohamed ameweza kuelezea ni kwa namna gani wazee Wa mwanzoni kabisa wa TANU ambao wengi wakiwa ni waislamu na wakaweza kumpokea mwalimu kwa upendo wote.

Mzee Mohamed Said mimi ni mtu ambaye napenda sana unachoandika. Lakini mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakimshutumu mbali na kipaji na talanta kubwa aliyonayo ya kuandika, historia zake mara nyingi huwa zinaambatana na udini ( ZEALOTISM).

Mfano; katika moja ya komenti zake nitamnukuu hapa chini

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Hio ni moja ya komenti aliyoiandika mzee wangu Mohamed kuhusu uwiano kati ya waislamu Na wakristo. Na akaendelea chini kwa kusema kwamba:

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

Kama takwimu hizi ni za kweli mzee wangu Mohamed Said unafikiri ni nini kinasababisha kuendelea kuwepo kwa Mizani kutoku-balance?

Katika kitabu cha Kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. Umetuonyesha ni jinsi gani makubaliano Baina ya waziri mkuu wa Kenya Ndg. Jommo kenyata na waziri mkuu wa Zanzibar Ndg. Mohamed shamte hayakufanikiwa na kupelekea kunyanga’nywa Kwa waislamu Taasisi ya (MIOME) mombasa institute of muslims education.

Mzee wangu Mohamed si mtu mwenye nia mbaya akijaribu kueleza kwa namna gani historia ya TANU haikuwa sawa kwa kiasi fulani, hivyo anajaribu kutufumbua macho zaidi. Lakini ni kama vile waislamu bado ni watu ambao kwa maandishi yake hakuna uwiano sawa na wakristo.

Mzee wangu Mohamed Said mimi naomba kufahamu kutoka kwako mbali na yote , ni kipi kifanyike ili kutengeneza uwiano sawa baina ya waislamu na wakristo katika Ngazi zote za nchi yetu? Haswa katika kipindi hichi tulichonacho elimu inatolewa kwa usawa bila kujali dini zetu.
NB. This is not intended to divisive or inflammatory only for learning purpose.
Hawa ndiyo wale vijana wa hovyo walio zeeka nasema uongo nduguzangu?
Cc Mohamed Said
 
Hiki kizee kiwekwe kwenye orodha ya magaidi hatari.Ningekuwa mimi jiwe kusingekuwa hata na hizo sijui 10%,5% au 20%,zingekuwa zinasoma 1%,0.5% nk ili kukipa hiki kizee presha kukiua kabisa na presha maana kinapenda sana ubaguzi
Evil...
Kuna mtu siku chache zilizopita alinitukana kwa kuniita ''Kibabu.''
Soma hapo chini majibu yangu kwake:

''Mimi ninapoona mtu analeta kejeli, matusi na "name calling" huwa namkwepa simjibu.

Ila nakujibu wewe kutaka kukuongezea maarifa ili uelimike na ukipendezewa ujifunze adabu.

Mimi ukiniita "Kibabu," katika msamiati wetu watu wa Pwani unakuwa umekosea ikiwa nia yako ilikuwa kunitukana.

Ungeniita, "Kizee."
Ungefanya hivyo ungekuwa umenitukana kama ulivyokusudia.

Kikwetu, "Kibabu," ni jina anapewa mtoto mchanga wa kiume ambae bado hajapewa jina na akiwa mwanamke anaitwa, "Kibibi."

Wewe tusi lako umepatia kuniita ''Kizee.''
Hakika mimi ni mzee nina miaka 72 sasa.

Ikiwa Allah ataniongezea umri basi sasa ndiyo nakimbilia kuwa ''Kizee.''
Hunifahamu laiti ungrnijua labla ungefanya staha.

Mimi si mbaguzi laiti ningrkuwa mbaguzi nisingeweza kuingiliana na vyuo, vyombo vya habari na wachapaji vitabu walichapa kazi zangu.

Hali kadhalika hata hapa JF nisingeheshimika:

1715771895694.jpeg

1715771947159.png

Back
Top Bottom