Kwako Mzee Wangu Mohammed Said

Sasa kama mzani haujabalansi tangu kwa idadi ya waliosoma Rais yeye atawatoa wapi? Wewe angalia kwenye 100 Waslamu wako 10 wenye elimu dunia nzuri waliobaki ni madrasatul sasa Rais atafanyaje hapo?
 
hata kabla mohamed hajakujibu,kuweka uwiano sawa ni kuteua kwa kuzingatia usawa wa kidini kwani kwa sasa dini zote watu wake wamesoma
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1700665386000.jpg
    8.1 KB · Views: 1
Huyu Mohamed Said ni mdini tu anaetapatapa. Ukitaka kujua hilo soma vitabu vyake vyote uone na articles zake, mahojiano anayifanyiwa, utagundua huyu ni activist wa Islamic ingefaa apewe nafasi pale bakwata.
 
hata kabla mohamed hajakujibu,kuweka uwiano sawa ni kuteua kwa kuzingatia usawa wa kidini kwani kwa sasa dini zote watu wake wamesoma
Why iwe kidini?
Kwanini isiwe kikabila, kimaeneo/kikanda, kijinsia, kitaaluma, kiuchumi?
Hizo takwimu za uwiano wa wasomi kidini umezitoa wapi?
Mwisho kabisa, kuteua kwa uwiano wa kidini kuna mchango gani katika kuongoza watu?
 
Media wanapofanya mahojiano naye wanamuita mwandishi na mwanahistoria kana kwamba anayoyaandika ni mazuri kwa wote kumbe ni mchochezi, anaandika kuonesha jamii ya imani yake haipewi haki kwenye masuala mbalimbali ya maamuzi ya nchi akidai jamii yake ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kuleta uhuru wa nchi hii dhidi ya wakoloni. Anajifanya hajui kuwa jamii yake haikuwapokea watangulizi wa ukoloni na iliwaonesha maeneo ya mbali na wao kukumbatia utamaduni wa dini yao waliyoipokea toka kwa wafanyabiashara wa kiarabu waliotoka uarabuni. Angeandika athari zilizosabishwa na dini ya wafanyabiashara hao kwa jamii yake kuwahadaa na miungu yao mpakaa wakadumaa kifikra huku jamii zingine zikisoma elimu ya wamisionari wa kizungu angeonekana ni wa maana ila kilio chake kikuu ni kutaka watu wa dini yake waonekane ni wengi katika teuzi za nchi.
 
Katika mazingira ambayo karibu kila dhehebu/makundi ya dini ya Kikristo wanamiliki mashule ya kutosha na vyuo, unategemea cream ya viongozi itatokea dini gani ikiwa tutatumia usomi kama sifa za kuteuliwa?
 
Kama anaona jamii ya dini yake haipewi uteuzi wa kuridhisha aanzishe chama cha siasa chenye sura kamili ya dini yake na lengo kuu iwe ni hayo mambo anayoyaandika. Uhuru upo ajaribu kuanzisha chama hicho tuone kama atapata wanachama wengi wa kukiunga mkono chama chake kwa hizo sera za kidini za kubagua watu wa nchi moja
 
Mzee huyu ni Cuf au ACT nadhani,yuko sahihi kwa baadhi ya mambo ila ni muoga sana kipindi cha JPM alikuwa anaandika kwa tahadhari akiogopa kushughulikiwa,sasa anajiachia tu
Mdukuzi,
Sijapatapo kuacha kuandika wakati wowote.

Sijapatapo kushikwa na hofu nikaacha kuandika.

Angalia hapa niko katika jina langu kwa sura na sauti.

Wewe ndiye muoga uliyeficha jina lako.

Niandikayo yote yako hapa yapitie na lete ushahidi kuwa mimi muoga.
 
Huyu Mohamed Said ni mdini tu anaetapatapa. Ukitaka kujua hilo soma vitabu vyake vyote uone na articles zake, mahojiano anayifanyiwa, utagundua huyu ni activist wa Islamic ingefaa apewe nafasi pale bakwata.
Peaky...
Ukiwa "mdini" unakusudia Uislam umesema kweli kabisa.

Naupenda sana Uislam.

Ukiwa kuniita "activist wa Islamic," unakusudia kushughulika na Waislam na Uislam hakika umesema kweli.

Kwani haya hayaruhisiwi mtu kufanya?

Hili la kupewa nafasi BAKWATA nakuomba unifafanulie nafasi ya BAKWATA nikafanye kazi gani?
 
Zanzibar...
Unataka kufanya mnakasha na Mohamed Said kwa uandishi huu ulioweka hapa?
 
Kupitia comment yako sasa naamini kwamba kumbe kuna watu huwa mnawasingizia wana id mbili kumbe uzushi tu
kwani we huwa hugundui hilo? Mtu anakula ban kisha anaibuka na nyingine. Sio mbili tu hata tatu na zaidi watu wanazo kwa malengo yao. Kuna wale verified wanajulikana kabisa majina yao ni halisi na sura zao tunazijua, we unadhani wataacha kuwa na ID zingine zitakazowapa uhuru wa kuandika maoni yao tofauti na tunavyowajua misimamo yao?
 
ni chama cha siasa chenye element za udini. Ndio cuf ya wakati ule, hawakuona aibu kuji brand kwa dini ile katika mikao ya mikutano yao ya kampeni sura ilikuwa ni ya kidini
Loth...
Unaijua historia ya chama cha TANU kuanzia African Association 1929 hadi TANU 1954?

Ungeweza kuiweka TANU Dar-es-Salaam mbali na Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam waTanganyika)?

Hujui kwa nini ilikuwa vile?
 
Min...
Kipaumbele cha Waislam baada ya uhuru kupatikana ilikuwa elimu.

Mwaka wa 1962 kukaitishwa Muslim Congress agenda kuu kujenga shule na Chuo Kikuu kupitia EAMWS.

Shule zikaanza kujengwa na ilipofika mwaka wa 1968 EAMWS ikaanza ujenzi wa Chuo Kikuu.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS na kuunda BAKWATA.

Huijui historia hii?
 
Hiki kizee kiwekwe kwenye orodha ya magaidi hatari.Ningekuwa mimi jiwe kusingekuwa hata na hizo sijui 10%,5% au 20%,zingekuwa zinasoma 1%,0.5% nk ili kukipa hiki kizee presha kukiua kabisa na presha maana kinapenda sana ubaguzi
 
Min...
Hujui yaliyokuwa yakifanyika NECTA hadi Waislam wakafanya maandamano mwaka wa 2012?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…