Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Peaky...Huwezi kuwa na jibu kwa vile madai yako hayana msingi. Kulalamika lalamika kama mtoto haitawasaidia waislam wenzako. Ukijikita kuwahamasisha na kuwapa mbinu wafanyeje ili nao wa dominate utakuwa umewasaidia.
Peaky...Nimekujibu hawakuwa na impact.
Walitoa tu mchango wao.
Adili...Nakumbuka nimeanza kusoma nakala zako mwanzoni mwa 1990's. Hata ktk zile zilizo zikirudufiwa na typewriter mwisho ukiandika jina lako.
Naikumbuka "Mwinyi's Dilemma" nadhani ulikuwa ukimjibu Christopher Mtikila.
Nakushukuru si haba umetufungua macho si haba
Ungejibu hoja tuPeaky...
Silalamiki.
Hapa mimi na wewe tuko katika mjadala na wala wewe hulalamiki katika kunijibu ila tunajadiliana.
Naona lugha yako imekuwa na hamaki.
Huna ukweli wowote, kazi yako ni kueneza chuki ya waislam dhidi ya Wakristo.Adili...
Kazi yangu ni kuandika ukweli.
Tuko ktk ulimwengu wa hoja, thibitisha uenezi huo wa chuki kwa hoja na ushahidiHuna ukweli wowote, kazi yako ni kueneza chuki ya waislam dhidi ya Wakristo.
Wewe ni Mohamed Said ?Tuko ktk ulimwengu wa hoja, thibitisha uenezi huo wa chuki kwa hoja na ushahidi
Peaky...Ungejibu hoja tu
Mimi niko tayari kufanya mjadala na wewe kuhusu hilo la dini kutumika kama sifa katika uteuzi, hapo juu nimejibu hoja zako kupita thread ya mleta mada.Zanzibar...
Unataka kufanya mnakasha na Mohamed Said kwa uandishi huu ulioweka hapa?
Peaky...Wewe ni Mohamed Said ?
Kama sio wewe acha ajibu mwenyewe maana anajua ninachokisema na hatujaanzia hapa leo. Namfahamu toka yuko university of wales.
Kwani mimi nimekuletea kejeli na jeuri?Peaky...
Najitahudi kukujibu kadri ya uwezo wangu na bila kuandika kejeli na jeuri.
Ikiwa hurudhiki ni bahati mbaya kwako.
Zanzibar...Mimi niko tayari kufanya mjadala na wewe kuhusu hilo la dini kutumika kama sifa katika uteuzi, hapo juu nimejibu hoja zako kupita thread ya mleta mada.
Kama una hoja, pangua majibu yangu.
Peaky...Kwani mimi nimekuletea kejeli na jeuri?
😀😀😀Peaky...
Jibu unalo wewe mwenyewe.
Huyu jamaa si ndio kaoa wake wa4,na anajisifia wanapendana.
Nadhani tuna wahindu,budha na wengine wengi tu......swala la uteuzi nadhani linazingatia zaidi uwezo na uzoefu katika baadhi ya maeneo......kitu kizuri maraisi wengi wamepita nchi wakiwa na tofauti za Imani ......hili jambo sio zuri kulizungumzia hasa Imani za watu maana hata ukristo wenyewe haufanani......Wakuu Heshima mbele.
Mimi binafsi kwanza niseme ni mtu ambaye napenda sana kusoma historia tofauti tofauti. Nimekuwa nikivutiwa na mzee wangu Mohamed Said katika maandiko yake mengi, mzee Mohamed saidi ni mtu ambaye mara nyingi ameweza kuielezea historia Ya Tanganyika tangu harakati za uhuru zinapoanza mwanzoni kabisa, mzee Mohamed ameweza kuelezea ni kwa namna gani wazee Wa mwanzoni kabisa wa TANU ambao wengi wakiwa ni waislamu na wakaweza kumpokea mwalimu kwa upendo wote.
Mzee Mohamed Said mimi ni mtu ambaye napenda sana unachoandika. Lakini mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakimshutumu mbali na kipaji na talanta kubwa aliyonayo ya kuandika, historia zake mara nyingi huwa zinaambatana na udini ( ZEALOTISM).
Mfano; katika moja ya komenti zake nitamnukuu hapa chini
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:
Mawaziri na Manaibu: 30.
Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.
Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.
Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.
Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.
Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.
Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.
Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.
Wakurugenzi mbalimbali: 249.
Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.
Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.
Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.
Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.
Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33
Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.
Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.
Jumla Kuu ya Uteuzi:
Waislamu asilimia 20%.
Wakristo asilimia 80%.
Hio ni moja ya komenti aliyoiandika mzee wangu Mohamed kuhusu uwiano kati ya waislamu Na wakristo. Na akaendelea chini kwa kusema kwamba:
Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.
Kama takwimu hizi ni za kweli mzee wangu Mohamed Said unafikiri ni nini kinasababisha kuendelea kuwepo kwa Mizani kutoku-balance?
Katika kitabu cha Kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. Umetuonyesha ni jinsi gani makubaliano Baina ya waziri mkuu wa Kenya Ndg. Jommo kenyata na waziri mkuu wa Zanzibar Ndg. Mohamed shamte hayakufanikiwa na kupelekea kunyanga’nywa Kwa waislamu Taasisi ya (MIOME) mombasa institute of muslims education.
Mzee wangu Mohamed si mtu mwenye nia mbaya akijaribu kueleza kwa namna gani historia ya TANU haikuwa sawa kwa kiasi fulani, hivyo anajaribu kutufumbua macho zaidi. Lakini ni kama vile waislamu bado ni watu ambao kwa maandishi yake hakuna uwiano sawa na wakristo.
Mzee wangu Mohamed Said mimi naomba kufahamu kutoka kwako mbali na yote , ni kipi kifanyike ili kutengeneza uwiano sawa baina ya waislamu na wakristo katika Ngazi zote za nchi yetu? Haswa katika kipindi hichi tulichonacho elimu inatolewa kwa usawa bila kujali dini zetu.
NB. This is not intended to divisive or inflammatory only for learning purpose.
kwa muktadha huu hao waanzilishi wa AA lengo lao ilikuwa ni kupigania uhuru wa dini na ukipatikana nchi iwe ya kidini? Ndio kusema tanganyika ingekuwa nchi ya kiislam na Tanzania inapaswa kuwa jamhuri ya kiislam kwa kuwa hao waasisi walikuwa ni waislam?Loth...
Soma historia ya uhuru ndiyo uje hapa ufanye mjadala.
Hawa ndiyo waasisi wa African Association: Kleist Abdallah Sykes, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson.
Ushapata hata siku moja kuyasikia majina haya katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
ni chama cha siasa chenye element za udini. Ndio cuf ya wakati ule, hawakuona aibu kuji brand kwa dini ile katika mikao ya mikutano yao ya kampeni sura ilikuwa ni ya kidini
Achana na huyo mzee, hoja yake ni mfu kwa 100%.
Mimi nitakusaidia kukujibu na kumkosoa vikali mzee Mohamed Said.
1. Nchi yetu haina dini, hivyo huwezi kutumia kigezo cha dini katika kuajili na kuteua nafasi mbali mbali za utumishi wa umma.
2. Dini ni suala la moyoni na sio jambo la lazima kubakia moyoni mwa mtu siku zote (inawezekana wakati nateuliwa nilikuwa Mkristo, wakati naapa nikawa Muislamu na wakati natumbuliwa nilikuwa mpagani), huwezi kujua dini halisi ya mtu mpaka uingie moyoni mwake. Kutazama majina ya mtu, haitoshi kujua imani yake halisi ya kidini.
3. Jamii imegawanyika katika mambo mbalimbali yakiwemo Imani, Kabila, Jinsia, Kipato, Taaluma, Makazi. Kama serikali itaamua kuteua watu kwa misingi yao ya kijamii basi uwiano wa kidini pekee hautoshi kuwawakilisha hao watu.
4. Rais atateua watu kutoka katika bwawa (pool) la watu wenye sifa stahiki kwake, hakuna mtu anajua hilo bwawa analotumia Rais kuchagua watu wake lina uwiano gani kidini. Unaweza kukuta ndani yake lina waislamu wachache sana, hivyo litaishia kuteua waislamu wachache.
5. Mamlaka ya uteuzi iko ndani ya utashi na uhuru wa Rais aliyepo madarakani, anawajibika kwake mwenyewe, hivyo huwezi kujenga hoja ya kuwepo uwiano wa kidini katika kuteuliwa.