Kwako Rais Mwinyi; Bandari ya Zanzibar unaiua kwa haya mambo unayoyafanya

Kwako Rais Mwinyi; Bandari ya Zanzibar unaiua kwa haya mambo unayoyafanya

Kuna point umeigusia hapo na hiyo ndio inayosababisha wapiga deal walielie.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
unaongea bila kujua unachoongea, mambo haya yalikuweko wakati Magufuli, mpaka kina Sabaya walikua wanapita madukani kudai kodi, matokeo yake biashara nyingi zikafungwa au zikafa. sasa hivi Sabaya yuko Mahakamani na Serikali pamoja na tra wamemkana.
huwezi kuweka viwango vikubwa halafu ukalazimisha watu walipe ukategemea matokeo chanya.
 
Nadhani wewe ndio unaongelea kwa ushabiki ama kwakuwa wewe ni mnufaika mojawapo wa wanao banwa sasa. Zanzibar umwinyi ulikuwa umezidi, watu walikuwa wanatoa mizigo sawa na bure kisa ni mtu fulani. Nimeishi Zanizbar mika 7 hivyo bafahamu vizuri sana jinsi mambo yanavyoenda huko

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Kama shamba la bibi lete basi na wewe mzigo wako halafu utoe kama sanduku la harusini
Mwinyi anataka mapato ili kuwe na maendeleo, yawezekana wewe hutaki serikali ikusanye ili uwe na fedha nyingi na serikali isiwenazo
 
Nadhani wewe ndio unaongelea kwa ushabiki ama kwakuwa wewe ni mnufaika mojawapo wa wanao banwa sasa. Zanzibar umwinyi ulikuwa umezidi, watu walikuwa wanatoa mizigo sawa na bure kisa ni mtu fulani. Nimeishi Zanizbar mika 7 hivyo bafahamu vizuri sana jinsi mambo yanavyoenda huko

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Aisee mimi naongelea uhalisia, sikatai Umwinyi Zanzibar upo na unasababishwa na hao hao vigogo wa chama na Serikali, lakini tukiachilia hayo hali imekua ngumu mno.

Mheshimiwa Rais Mwinyi alipoapishwa tu alipandisha ushuru wa bidhaa mbali mbali, hii ikapelekea vitu kupanda bei , lakini pia alianzisha tozo za kilimo katika bidhaa kama maziwa na kuku, na watu wakalipa. Lakini hali ilivyo sasa ni tofauti , sasa hivi kuna harrassment bandarini, hichi kipindi sote tunajua dunia nzima mazingira ya biashara yamekua magumu na nauli za meli zimepanda maradufu kutokana na COVID 19.

Sasa unapoongeza tena vikwazo badala ya ku retreat mpaka hali itakapo kaa sawa manaake unafanya situation iwe very worse. and later on you wont have any one to squeeze
 
Mwinyi anataka mapato ili kuwe na maendeleo, yawezekana wewe hutaki serikali ikusanye ili uwe na fedha nyingi na serikali isiwenazo
nyie watu mnaongea kwa kuwa mna maslahi binafsi, kama anataka mapato kwa nini asidhibiti matumizi ya Serikali pamoja na upotevu wa fedha za umma. Wewe ni mwenyewe ni Shahidi Mheshimiwa Rais kila siku analalamika fedha za Serikali zinavyoibiwa. Mfano ripoti ya CAG inaonyesha katika fedha tsh bilioni kumi za matengenezo ya barabara ni bilioni moja tu ilitumika , bilioni 9 hazijulikani zilipo , kuna Wizara zimegoma kabisa kukaguliwa kama Wizara Ya Fedha , kuna taasisi zimegoma kuorodhesha mali za serikali, achilia mbali magari ya kifahari wanayotembelea watendaji wa serikali. Taasisi za serikali zinatumia magari ya milioni 100-250 wakati gari za milioni 30-40 zipo tena nzuri na ndio wananchi wa kipato cha juu wanaoziendesha

Sasa kama mnataka kuleta maendeleo mbona pesa mnazila huko halafu mnasingizia watu hawalipi kodi.? Acheni hizo
 
Back
Top Bottom