Kwako Rais Samia, fupa la ukwepaji Kodi Kwa wafanyabiashara wape wanunuaji wamalizane nalo lakini Serikali iwahamasishe kwa gawio katika manunuzi

Kwako Rais Samia, fupa la ukwepaji Kodi Kwa wafanyabiashara wape wanunuaji wamalizane nalo lakini Serikali iwahamasishe kwa gawio katika manunuzi

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Kwako Rais wa JMT Mhe.Samia Suluhu Hassan, ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe.Rais, kwa namna ya pekee pekee ninapenda kuchukua nafasi kukupongeza kwa kuwa kielelezo Cha safari ya mabadiliko makubwa kwenye nyanja mbalimbali katika Taifa letu na kubwa zaidi litakalokumbukwa ni kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025 kukiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Mhe.Rais, siku ya Jana katika Baraza la Eid ulitukumbusha wajibu wa wafanyabiashara kulipa Kodi Kwa Serikali inayostahili na sio kuidhulumu Serikali. Ni kweli Mhe.Rais suala Hilo la wafanyabiashara kuidhulumu mapato ya Kodi Serikali lipo sana na zaidi wanunuaji hawalipi umuhimu mkubwa. Kivipi?

Mnunuaji ndio alitakiwa kuwa mtu wa kwanza na WA mwisho kubanana na huyu mfanyabiashara kumpatia risiti hali ya mzigo alioununua lakini wanunuaji hawafanyi hivyo na ninaamini Serikali ikianza na wanunuaji , wafanyabiashara watatoa risiti halali Kwa kiasi Fulani itapunguza tatizo.

Kwenye suala la kupewa risiti Kuna mambo matatu:

Kwanza, Kuna wafanyabiashara wanatoa risiti pungufu au hawatoi kabisa Kwa kigezo Cha punguzo la Bei. Mnunuaji anapewa punguzo la Bei ili akubali kuandikiwa risiti pungufu au asipewe kabisa.

Pili, Kuna wafanyabiashara wanatoa risiti za kutembelea njiani Kwa wateja. Hapa mteja anapewa risiti hata ya wiki iliyopita ya mzigo tofauti ili tu atumie kutembelea njiani. Wanaotumia mbinu hii wakikutana na ukaguzi wanasema mzigo nilinunua wiki iliyopita lakini sikuuchukua ndio nimeuchuka Leo.

Tatu, Kuna wafanyabiashara wanatoa Bado risiti za mkono. Mashine ya EFD anakuwa nayo kama dharula ya ukaguzi ikiwepo lakini wateja anawaandikia risiti za mkono na ukiuliza juu ya risiti ya EFD anakuambia mashine ni mbovu , Kwa kuwa mteja anakuwa amekipenda hiko kitu na Bei ni nzuri anachukua tu risiti ya mkono.

Haya ndio makundi ya wafanyabiashara na risiti wanazotoa, hapa sijazungumzia wanaotoa risiti kamili na halali Kwa sababu kundi hili ni wazalendo.

Mhe. Rais ,wakati ukiwaapisha viongozi uliowateua karibuni ulitilia mkazo suala la namba moja ya utambulisho Kwa Kila mtu.

Nafikiri suala Hilo la namba moja ya utambulisho linaweza kutumika kudhibiti dhuluma ya mapato inayofanywa na wafanyabiashara kwenye suala la risiti za EFD.

Hivyo Mhe.Rais nashauri suala hili la risiti za EFD kutoka Kwa wafanyabiashara liachwe Kwa wanunuaji walishughulikie ila Serikali iwahamasishe wanunuaji Kwa gawio kidogo kutokana na manunuzi.

Kwa kuwa Leo hii mteja anayepewa punguzo la Bei na mfanyabiashara hatoona umuhimu wa kudai risiti kutokana na punguzo basi ninaamini gawio la Serikali litamchochea kudai risiti. Kwa kuwa itakuwa ngumu Serikali kujua Bei halisi mzigo wa mteja basi huyu mteja adai risiti hata ya punguzo ili apate gawio.

Kukiwa na gawio ,mnunuaji hatoridhishwa na jibu la mashine ya EFD ni mbovu hivyo inawezekana akaondoka bila kununua Kwa huyo mfanyabiashara na atafanya hima kumtafuta mfanyabiashara anayetoa risiti za EFD na pia suala la kupewa risiti za mkono litapungua kama sio kuisha kabisa maana risiti ya mkono Haina gawio mnunuaji akihamasika na gawio itamchochea zaidi na zaidi.

Kuhusu kupewa risiti za kutembelea njiani kukwepa ukaguzi basi nalo litakwisha kabisa ,mnunuaji atataka risiti halali ya mzigo alionao ili naye gawio lisimpite.

Kwa kuwa gawio hili litahusu manunuzi yote yanayofanywa ninaamini wanunuaji watahamasika bila kujalisha ukubwa au gharama za mzigo na hili litawakumbusha wanunuaji Kila mara kudai risiti za EFD.

THE WAY FORWARD: NINI KIFANYIKE?
Kwanza, namba ya utambulisho ambayo Mhe.Rais umekuwa ukisisitiza itumike. Kwa kuwa itakuwa ni namba maalumu Kwa Kila mtu hivyo Kila mtanzania atakuwa na usajili maalumu. Mashine za EFD ziwezeshwe sehemu ya kuweka hiyo namba ya utambulisho na kwenye Kila risiti hiyo namba ionekane.

Namba hiyo ndio itumike kama jina lako kuingia kwenye mfumo unapotaka kulitoa gawio lako.

Pili, elimu itolewe Kwa wingi juu ya gawio Hilo la Serikali katika manunuzi. Uelewa unapokuwa mkubwa unafanya utekelezaji uwe wa juu zaidi.

Tatu, utaratibu huo unaweza kuitwa GAWIO LA SERIKALI KWA WANUNUAJI/ KATIKA MANUNUZI.

Mwisho, ninaamini wanunuaji wakitumika vizuri Kwa kuwapa gawio kutokana na manunuzi wanayofanya watasaidia kudhibiti suala la ukwepaji Kodi kutoka Kwa wafanyabiashara.

Wako katika ujenzi wa Taifa,
 
kwa utitiri wa kodi, kiburi, ujuaji na tamaa za wafanyakazi wa TRA nakuapia wallah wafanyabiashara wataendelea kukwepa kodi kwa gharama zozote zile.

Kama umewahi kufanya biashara utaelewa kile nasema. TRA inakera na inahamasisha mazingira ya ukwepaji kodi kuliko kukusanya kodi.
 
Siyo kwamba wafanyabiashara hawapendi kulipa kodi au wanunuzi hawapendi kudai risiti, kinachonyong’onyesha watu nikuona kodi zenyewe zinatumiwa vibaya na wachache walio kwenye mfumo.

Ripoti za CAG kila mwaka ni ubadhirifu wa Hela!! Ukienda kwa hao wakusanya kodi wenyewe ndio balaa!

Vijana wadogo wana ukwasi wa kutisha mpaka unajiuliza hivi hawa wanalipwa mishahara kiasi gani?
 
Watu wakiwa hawana imani na matumizi ya kodi zao.
Hawawezi kuhamasika kulipa kodi.
 
Watu wakiwa hawana imani na matumizi ya kodi zao.
Hawawezi kuhamasika kulipa kodi.
Suala la kulipa Kodi ni lazima ndio maana zinawekwa taratibu za ukusanyaji na mara nyingine matumizi ya nguvu yanahitajika. Kigezo gani unatumia kusema hivyo?
 
Siyo kwamba wafanyabiashara hawapendi kulipa kodi au wanunuzi hawapendi kudai risiti, kinachonyong’onyesha watu nikuona kodi zenyewe zinatumiwa vibaya na wachache walio kwenye mfumo.

Ripoti za CAG kila mwaka ni ubadhirifu wa Hela!! Ukienda kwa hao wakusanya kodi wenyewe ndio balaa!

Vijana wadogo wana ukwasi wa kutisha mpaka unajiuliza hivi hawa wanalipwa mishahara kiasi gani?
Wafanyabiashara wengi ni wababaishaji kwenye kutoa risiti hili ni lazima ukubaliane nalo kwanza.

Ripoti za CAG sio ushahidi ,mara nyingi inakuwa ni Auditor Opinion ambapo sio mara zote ni sahihi.

Vijana wadogo kumiliki ukwasi ni jambo la ajabu?
 
Suala la kulipa Kodi ni lazima ndio maana zinawekwa taratibu za ukusanyaji na mara nyingine matumizi ya nguvu yanahitajika. Kigezo gani unatumia kusema hivyo?
Ni lazima ila wafanyabiashara na sisi wanunuzi tunashirikiana kukwepa kwa sababu asilimia kubwa inaishia mifukoni mwa vigogo na mamabo yasiyo na tija kwetu. Inakuwa lipa kodi kwa maisha bora ya kiongozi
 
Hoja dhaifu kabisa hiyo.
 
Mm sipendi unafiki kabisaaaa ...ni mzalendo mzuri tu ila kwa swala la kodi km napata mwanya wa kukwepa tena ndo nafurahi kabisaaaa maana kodi yangu siioni inafanya nn nikienda hosptali gharama ni kubwaaaa hatari mitaani barabara ni mbovuuu Mungu ndo anajua na kila siku unasikia mradi fulani hela ni za mkopo na bado unasikia watu wamepiga mabilioni huko lakini hakuna lolote wanalo fanywa leo hii mm nijitie kimbelembele kulipa kodi ahhhaaaa mtanisamehe
 
Hoja dhaifu kabisa hiyo.
Si dhaifu maana lengo la kodi ni kwa ajiri ya kutoa huduma za kijamii si kuishia mifukoni mwa watu wachache... Hili lina dhoofisha moyo wa kutoa kodi. Ndiyo maana mtu akienda dukani mfanya baishara akamwambia mzigo wa milion tatu aandike milion na lak 2 na ampe discount ya lak na nusu anakubali haraka. Maana unakuwa unaona hii kodi inaishia mifukoni mwa watu. Wakusanyaji kodi wenyewe wala rushwa mtu afisa tu ndani ya mwaka ana mali kufuru. so kama wanavyoiba wao, na wafanyabiashara na wanunuzi nasi tunatafuta jinsi ya kukwepa.
 
Unalipa Kodi ili mama Salma alipwe kiinua mgongo cha uwenza wa rais hapo hapo naye bado mbunge.

Nchi ngumu sana hii.
 
Naunga mkono hoja

Maana ili kuweza kufanikisha ni lazima huyo mtu aone nini kinamfaidisha yeye binafsi.

Kwa kuwa mbinu yako imetilia maanani ubinafsi basi inaweza kufanikiwa
 
Unalipa Kodi ili mama Salma alipwe kiinua mgongo cha uwenza wa rais hapo hapo naye bado mbunge.

Nchi ngumu sana hii.
Mama salma hakutoa hoja kujiangalia yeye au kuangalia nafasi yake ,kaangalia upande wa pili ambao wengine hatuufahamu.

Twende kwenye ukweli na uhalisia, hivi unataka mke wa Baba wa Taifa , mama Maria Nyerere aanze kulia Kwa watoto wake wamsaidie hela ya chumvi? Au aililie Serikali imsaidie?
 
Si dhaifu maana lengo la kodi ni kwa ajiri ya kutoa huduma za kijamii si kuishia mifukoni mwa watu wachache... Hili lina dhoofisha moyo wa kutoa kodi. Ndiyo maana mtu akienda dukani mfanya baishara akamwambia mzigo wa milion tatu aandike milion na lak 2 na ampe discount ya lak na nusu anakubali haraka. Maana unakuwa unaona hii kodi inaishia mifukoni mwa watu. Wakusanyaji kodi wenyewe wala rushwa mtu afisa tu ndani ya mwaka ana mali kufuru. so kama wanavyoiba wao, na wafanyabiashara na wanunuzi nasi tunatafuta jinsi ya kukwepa.
Timiza wajibu wako ipasavyo kabla ya kudai haki yako. Mfanyabiashara akitimiza wajibu wake Kwa kutoa Kodi inavyostahili ,wakusanya Kodi wa TRA wasingekuwa hivyo unavyosema ila hao wakusanyakodi ni wafanyabiashara waliowatengeneza. Unakuta mfanyabiashara anadaiwa milioni 500 ya Kodi lakini anamuomba mkadiriaji amkadirie iwe milioni 200 anasema sawa ,nitakukadiria hiyo unanipa ngapi? Anaahidiwa milion 30 , hapo tatizo limetengenezwa na nani?

Pia, unachosema nasema ni hoja dhaifu, Kwa nini? Kama ushahidi wa unachosema ni ripoti za CAG uko wrong, ripoti za CAG ni maoni ya mkaguzi na maoni hayo sio mara zote ni sahihi ila pia sikatai kwamba upigaji upo
 
IMG-20240409-WA0000.jpg
 
Wafanyabiashara wengi ni wababaishaji kwenye kutoa risiti hili ni lazima ukubaliane nalo kwanza.

Ripoti za CAG sio ushahidi ,mara nyingi inakuwa ni Auditor Opinion ambapo sio mara zote ni sahihi.

Vijana wadogo kumiliki ukwasi ni jambo la ajabu?
Wewe utakuwa mfanyakazi wa TRA au chawa wa samia
 
Back
Top Bottom