Mimi ni muumini mzuri wa Tanzania Kwanza. Nakuomba sana:
Mungu ibariki sana Tanzania. Mungu ibariki Afrika.
- Fungulia makanisa yote haraka mno.
- Mwachie polepole wakosoaji wako, waache waongee tu. Hawana madhara kwenye maamuzi yako. Mfano, Dr. Slaa wakati wa Kikwete aliongea na kukosoa sana, Kubenea aliandika mno.
- Wakati wa Mkapa, Jenerali Ulimwengu alimkosoa Mkapa mpaka ikasemekana wana bifu binafsi, lakini hakufungwa. Mtikila naye alikosoa. Kwa hiyo wakosoaji lazima wawepo. Wasikilize mema, chuki binafsi puuzia.
- Maandamano no, maandamano no.
- CCM kama chama dola kifanye fundraising ya kuwafidia kada wake na wananchi waliopoteza mali zao kutokana na wahuni waliochoma na kuiba. Kwa wale wenye insurance, serikali isimamie wafidiwe haraka ili msiwavunje moyo kuwa mwana CCM ni risk.
Mungu ibariki sana Tanzania. Mungu ibariki Afrika.