Kwako Single Mother, naomba nafasi tulee huyo mtoto, nitakuwa baba bora mwenye upendo hutoamini

Kwako Single Mother, naomba nafasi tulee huyo mtoto, nitakuwa baba bora mwenye upendo hutoamini

Unataka ugundue nn mjomba single mother ni hatar sanaa weka mbal na watoto.ila labda mm nahc ww jogoo linawika ila sperms mbovu xo unatafta kichaka uzibe aibu sabb kwa m2 kweny akil timamu huwez panga kuoa single mother labda itoke2 tyuu siku umegonga au kukutana nae ukanogewa nae ndo ukaoa ila sio kihivyo unavyopanga ww unless you are kidding

Ebu balehe kwanza ndo uchangie nyuzi kama hizi
 
Kilichonileta humu ni kutoa langu la moyoni kwa yeyote ambae nafsi yake itaguswa na hitaji langu. Natumaini ninayo haki kikatiba, kidini na kijamii kuchagua aina ya mwenza ambaye nafsi na moyo wangu havitakuja kupungukiwa na upendo juu yake pamoja na wote anaowaheshimu na kuwathamini katika maisha yake.

Natafuta Single Mother (mwanamke aliyezaa mtoto/watoto lakini hajaolewa: Yamkini aliolewa akatoka kweye ndoa au alizaa kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Ieleweke kuwa mimi sina matatizo yoyote ya kiuzazi na ni mwanaume rijali mwenye heshima ndani ya jamii inayonizunguka, najitegemea na ni mlipa kodi serikalini.

Pia ieleweke kuwa ninatambua kuna sehemu za ibada, mtaani na hata kazini ambapo ningeweza kutafuta mwenza ninayemtaka, lakini JamiiForums binafsi nina iheshimu kwasababu wanachama sio maroboti, ni watu hao hao walio kwenye jamii nilizozitaja hapo juu. Kwahiyo nina imani 100% kuwa nitampata mwenza wa sifa niliyoitaja.

Mwanamke huyo nitampenda kabisa kwa hali zote bila kujali amekubali tuoane au tubaki kwenye uhusiano wa kawaida. Pia mtoto/watoto wake nitawapenda hatoamini, na wala sitakuwa na kinyongo juu ya mwenza wangu kuwasiliana na baba wa watoto (wa damu), na tutamkaribisha kuwa anakuja kuwasalimia (kama mwenzangu akitaka).

Akili yangu imejawa na mawazo safi na chanya, hivyo siamini kuhusu baba wa damu kuendeleza uhusiano wa kimapenzi wakati halei watoto, au hata kama analea (ina maana tutakuwa sasa tunasaidiana kulea), nadhani ataniheshimu mimi kama mume halali wa huyu mwanamke.

Kama ni wewe ndio mke wangu mtarajiwa (Single Mother) au kuna Single Mother unamfahamu, tafadhari njoo inbox kwa maongezi zaidi.

Asante JamiiForums.

N.B. Nadhani nimejieleza vyema na sitarajii Interview (maswali yasio na mwelekeo wa swala langu au kejeli). Ni vizuri ukaja inbox kama una hoja, unless you are a potential Single Mother unaehitaji nikufafanulie zaidi.

Asanteni.
Wakija wote tunafanyaje? Maana ni wengi sana! 🤗
 
Back
Top Bottom